Mtu akifa anatakiwa azikwe wapi? Migogoro ya kuzika maiti

Kwahiyo ukifika wewe kumzika ndo atafufuka? Maiti azikwe haraka ndani ya masaa 24 ukifika utaonyeshwa kaburi
Kwa sisi Waislamau tunazika hivyo,kwa wale wanaomwamini Yesu kuwa bwana na mwokozi wao hawaamini hivyo.
Kila mtu azike atakavyo.
 
Kwa upande wetu mtu akifa anazikwa hiyo sehemu aliofia hakuna kuremba
Kuna watu wanataka wafu wazikwe kwao kwa sababu zao za kimila au matambiko
Ila mimi naona mtu azikwe anapofia tu
Hata mimi popote nitakapofia nizikwe hapo hapo
Kuna watu hawajali mtu ana shida gani mpaka umauti unamkuta, hata kwenda kumuona hospital au kumpa hata chakula au dawa
Ila wakisikia kafa ndio wataanza kukimbizana na kusema ooh asaforishwe kwa mamilioni wakati kaacha watoto
Hizo hela wapeni watoto na yeye azikwe hapo hapo
Wengine hata makaburi ya wapendwa wao hawajayazuru miaka Sasa mnagombania nini?

Halafu ninesoma bandiko paragraphs mbili tu
 
Kwa sisi Waislamau tunazika hivyo,kwa wale wanaomwamini Yesu kuwa bwana na mwokozi wao hawaamini hivyo.
Kila mtu azike atakavyo.
Yeah kwa wakristo ni sawa maiti kuendelea kucheleweshwa maana huwa wanaamini maiti kazimia na atazinduka.
 
Yeah kwa wakristo ni sawa maiti kuendelea kucheleweshwa maana huwa wanaamini maiti kazimia na atazinduka.
YEah, kila mtu aamini chake, sisi waislamu tunamwamini muhamadi na wao wanamwamini Yeus kristo mwana wa Mungu , ambaye alikufa kazikwa, akfufuka akapaa mbinguni na siku ya mwisho atakuja kuuhukumu ulimwengu.
 
YEah, kila mtu aamini chake, sisi waislamu tunamwamini muhamadi na wao wanamwamini Yeus kristo mwana wa Mungu , ambaye alikufa kazikwa, akfufuka akapaa mbinguni na siku ya mwisho atakuja kuuhukumu ulimwengu.
mungu alieuliwa na viumbe wake kwa kutundikwa juu ya mti
 
Tujifunze kuandika wosia wa wapi tuzikwe tukishakutwa na mauti
Ni muhimu woasia huo uzingatie mafunzo ya dini lakini pia uwezo wa familia yako.
Sio unaishi kigoma una andika ukazikwe Rombo huku unaona mfuko wa familia hauko sawa sawa....
 
Ni muhimu woasia huo uzingatie mafunzo ya dini lakini pia uwezo wa familia yako.
Sio unaishi kigoma una andika ukazikwe Rombo huku unaona mfuko wa familia hauko sawa sawa....
Uko sahihi mkuu
 
Mtu atamuacha babaye na mamaye na kuambatana na mumewe/mkewe na kuwa mwili mmoja, acheni ufitini aliewaambia nyie familia mnamamlaka ni nani?, babu yenu kafa hajatengana na mkewe nyinyi mnalazimisha. Huko walipo wanakula maisha kwa Upendo uliotukuka nyie endeleeni na fitina zenu.
 
(Luke 9:60)

Waache wafu wawazike wafu wao, wewe nenda kautangaze Ufalme wa Mungu.
 
Hivi Kunakuwa~ga na faida yyt maiti akizikwa upande fulani wa ndugu au jamaa?

Ni faida zipi kwa mfano?
Kwa uhalisia kamili HAKUNA FAIDA yoyote ILA narudia tena ILA kwa kufanya tofauti au kukiuka maamuzi yaliyoamriwa kunaleta shida na usumbufu mkubwa sana baadaye kwa waliobaki. Jambo hilo litafungua milango kwa wenye nia mbaya kuanzisha fitna na kuihujumu familia au Ukoo kwa kutumia mwanya huo. Utasikia eti Oh hiyo ni laana ya marehemu, marehemu hajaridhika, ni lazima yafanyike maombi, lifanyike tambiko n.k n.k
 
Kuna kitu cha kujifunza kutoka uzi huu. Asante Robert kwa kudadavua karibu kila aina ya changamoto/kero/sintofahamu zinazoweza kuibuka mara tu baada ya mtu kufa na kinachotakiwa kifanyike ni maziko. Ni kweli yatajitokeza mengi na kweli usipojua au walau kuwa na fununu ya kinachotakiwa kifanyike mintaarafu maandalizi na mahali pa maziko ww kama mhusika katika suala la maziko utahangaishwa sana hadi unakaribia kuchanganyikiwa.
Kule Uchaggani kwa mfano; hoja hizo hujibiwa katika Kikao cha maandalizi ya mazishi na hapo itapangwa ni wapi, tarehe gani na kwa kawaida huwa kuna gharama (kama zilivyo sherehe zingine)na Gharama hiyo itafikiwaje na Nani awajibike wapi.
 
Ni ujinga na ulimbukeni wawaafrika. Kwa tunaoamini kuwa mtu akifa safari yake ya maisha imekoma, ule ni mzoga tu, hakuna shida tunazika popote. Shida inakuja kwa wanaoamini kuwa mtu akifa anaenda kuishi mahali fulani sijui peponi au purgatory, ndo wanateseka na modality za maziko. Kuna mapokeo mengi sana ya kishetani yamejazwa kwenye taratibu za mazishi ambayo ni ya kipagani. Huo muda na rasilimali zinazopotezwa kubishania azikwe wapi, au azikwe kwa modality ipi ungetumika kufanya mengine. Mimi siyo muislamu ila kwenye protokali za mazishi nawakubali sana waislamu hawana longolongo. Umekufa asubuhi swala ya adhuhuri unazikwa.
 
Umesema sawa; lakini kumbuka na uzingatie kwamba kama kuna utaratribu anaotakiwa ufuatwe, na wenzio wote hapo kwenye Jamii husika au Ukoo wako wanazingatia hizo taratibu, halafu ww ukajiona ni mwerevu na mwamba una akili zaidi, ukaukiuka Utaratibu huo uliokubalika kwa makusudi kwa madai eti ni Ujinga na Ulimbukeni; endapo Iitatokea la kutokea i.e. shida(na mara nyingi hutokea hivyo)baada ya Ukiukwaji huo wa makusudi kabisa; utafanyaje Utauweka wapi uso wako ukizingatia kwamba huwezi tena ku-rewind huo mkanda??? Kumbuka mtu kufa ni mwili (ambao ndo tunaita mzoga na ndio ukweli) lakini Roho /Nafsi ipo inaishi.
Lakini mkuu tunapokuwa na Amani iliyogharamiwa na waliotutangulia tunajisahau sana na kudhania hali huwa hivyo siku zote hamnaga shida. Inapotokea shida tunahangaika na hakuna rangi tutaacha kuona.
Watu wanatumia busara kwa kuona kwamba kwa nini nijiingize huko eti nakwepa gharama (napoteza muda na fedha) wanakubaliana na utaratibu na maamuzi yatakayofikiwa na maisha yanasonga mbele.
 
Muwe mnaacha na pesa za usafiri na za kuhudumia msiba. Sio ufie dar halafu unataka uzikwe bukoba na pesa huna wala familia yako haijiwezi. Jiandae kuzikwa na city 🤣
Tutajiuaje sasa kama nitakufa kesho? Ingekua hivyo watu wangekua wanajipanga mapema
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…