Kuna hadithi ya mfalme aliyetaka kumuoza binti yake kwa mwanaume jasiri atakayeweza kuogelea kwenye bwawa la mamba mpk kulivuka na kufika upande wa pili .
Wakiwa wamejipanga pembeni ya bwawa mwanaume mmoja alisukumwa na mwanaume mwenzake. Yule mwanaume alidumbukia ndani ya bwawa na kwa bahati ya mtennde akabahatika kufika ng'ambo ya pili.
Alipofika ng'ambo ya pili alitarajiwa afurahie na azingatie ajenda ya kumuoa binti wa mfalme, badala yake akaanza kumtafuta aliyemsukuma mpaka kutumbukia kwenye bwawa la mamba. Alianza kupuyanga.
Hadith hii inatupa somo kubwa sana kuhusu viongozi wetu hawa wawili:- Magufuli na Samia. Wote hawa wameupata urais kwa bahati ya mtende.
Magufuli alipoupata akaanza kulipa visasi kwa yeyote aliyemhisi kuwa mbaya wake. Akajawa na hulka za ubinafsi na kupendelea kwao na wakwao (akawa mkabila na mkanda). Akatamani Kijiji cha Chato ndiyo kiwe jiji kubwa kuliko majiji yote hapa nchini.
Kama mnakumbuka aliagiza kuwa ndani ya Dar ni wilaya ya Ilala peke yake ndiyo iwe jiji. Lengo lake bila shaka alitaka kuhalalisha wilaya ya chato ikiwa jiji ndani ya mkoa wa Geita basi isishangaze watu. Alikuwa na mawazo ya ajabu sana mtu yule??!!
Magufuli ndiye mwanzilishi wa utamaduni mchafu wa kiongozi wa nchi kupendelea kwao na wakwao. Na huu ujinga hautakaa ukome mpk tutakapochapana na kuvunjana mikono na miguu.
Haikupita muda rais Samia akaukwaa urais kwa ndondokela. Naye tunaona anayafanya yale yale ya mtangulizi wake ya kupuyanga. Anaanza kupendelea wakwao na kwao. Ameuvaa uzanzibari zaidi ya utanganyika. Wazanzibari wamepata teuzi nyingi ktk awamu hii kuliko kipindi kingine chochote ktk historia ya taifa hili.
Hii nuksi ya upendeleo wa ukanda na ukabila iliyoanzishwa na Magufuli ni nani ataiondoa??