Mtu akikuomba ushauri kwa jambo kama hili utamjibu nini?

Ni heri useme roho mbaya tu lakini Mimi nakutana na wewe hayo ya watoto hayanihusu na Mimi nikiwa na watoto hayakuhusu tusipeane mizigo, ka ulizaa ulitegemea Nani akulelee kwa Zama hizi za watu kukimbizana kutafta hela mie nikae tu naelea mtoto wa mwingine arrrgh.

Sasa wengine mama kafariki sasa mwanamke unayejua uchungu wa mtoto unawezaje kushindwa kulea mtoto wa mwingine?

Hivi kwa attitude hiyo kwa mfano ukifa leo unataka watoto wako wakutane na wanawake wa akili km yako wateswe wapigwe bila sababu kisa mama zao hawapo?

Upo serious mwanamke unayejua uchungu wa mtoto unashindwa kulea mtoto innocent km huyo???

Maana ungekuwa mwanaume ningesema hujui mateso mwanamke anayopitia mpk kupata mtoto sasa wewe ni mwanamke na si ajabu labda tyr una mtoto,is it fair watoto wako wateswe kisa wanalelewa na mtu baki?

Najua una hasira na wanaume wanaozaa hovyo haya mahusiano yameisha mtoto kabaki na hapo ni lzm aende kwa mama au baba kwahiyo anapoenda akateswe tu au mkishakuwa na watoto mkiachana hamna mahusiano mapya??
 
Wewe umetoa povu tu bure bila kuelewa logic yangu Mimi case yangu nazungumzia watu walio hai na irresponsible, hata Kama kufa kwanini u force kulelewa mtoto wako.
 
Kifuatacho kinasikitisha sana dada angu. Hiyo roho ikatae kabisa.
Inaonesha hapo kwa jamaa umefuata pesa, kwani huna mvuto nae. Ipo sababu ya msinGi. Kama mtoto kafanana na baba ake ni wazi ungempenda Sana Kwan ungekuwa unamuona mumeo.
 
Azae mapema, akizaa atajua uchungu wa mtoto...

Huyo Hana roho mbaya, mwenye roho mbaya hajishtukii.. ni wivu tu
 
Huyo anamuonea wivu huyo mtoto kwa upendo anaoupata toka kwa baba yake.
Huyo dada anasumbuliwa na roho mbaya iliyopitiliza na wivu.
 
Wewe umetoa povu tu bure bila kuelewa logic yangu Mimi case yangu nazungumzia watu walio hai na irresponsible, hata Kama kufa kwanini u force kulelewa mtoto wako.

Ha force Mtoto si ana kwenda kwa baba ake ndugu
 
Mwambie aache kuolewa na huyo mwanaume tena anaempenda mtoto wake aolewe na mwanaume anaemchukia mtoto wake
 
Kitu ambacho ningeshauri mumeo akifanye kwa sasa ni kukupa ujauzito halafu ukifikia miezi sita amlete mtoto wake mwingine wa nje mdogo hapo nyumbani; Maisha yaendelee
 
KILA NIKIMUONA MTOTO WA MUME WANGU NAHISI KUCHANGANYIKIWA!

Kaka naomba tu unisaidie maana najikuta nashindwa haya maisha. Mimi nimeolewa ndoa yangu ina miezi minne sasa. Wakati nakutana na huyu mchumba wangu aliniambia kabisa kuwa ana mtoto ambaye amezaa na mwanamke mwingine, alishaachana na mwanamke na kaolewa hivyo yeye anaishi na mtoto wake kwani hataki mtoto wake kulelewa na Baba wa kambo.

Basi mimi sikua na shida, nilikua naenda kwake, namuona mtoto lakini wakati huo hata sikuona kuwa ni tatizo kwakua nilikua bado sijaolewa. Lakini Kaka baada ya kuingia kwenye ndoa, kuanza sasa kuishi na yule mtoto ndiyo sijui naonaje, mpaka nahisi kuchanganyikiwa. Katoto ni kakike, lakini ana sura ya Baba yake, yaani sijui nikuambieje Kaka, sio kwaba ni mtoto mabya, siwezi kusema hivyo lakini hatuendani naye kabisa.

Rafiki zangu wakija kunisalimia inabidi niseme tu ni mtoto wa ndugu yake na mume wangu lakini si mtoto wa mume wangu. Mtoto ana miaka mitano, ana akili, kachangamfu anajua kila kazi na ananiheshimu. Yaani kangekua katoto kazuri ningekapenda balaa kwani kana heshima sijui nikuambieje Kaka, lakini shida nashindwa, nikimuangalia wakati mwingine najiikuta na hasira tu nampiga hata bila sababu.

Hali hiyo inaniumiza kwani mwisho kanakuja kuniomba msamaha wakati hata hana kosa. Yaani kuna vitu vingine najikuta nagomba mpaka basi, nakua tu na chuki na mtoto. Wakati mwingine namfanyia visa tu ili kumpiga, mfano juzi nilimuwekea chakula kingi makusudi ili aache kula, basia liacha nikajikuta nampiga kuwa anachezea chakula basi nikamlazimisha kula na kweli alikula lakini alishindwa hata kunyanyuka yaani anapepesukapepesuka ila alimaliza na kuosha vyomboa akaosha.

Nilijisikia vibaya kwani sikupata faida yoyote, hali hii inanifanya nakua na kisirani, nakua mtu wa hasira hata kwa mume wangu. Sababu ya kuja kwako Kaka ni hivi, nataka kuongea na mume wangu amuondoe huyu mtoto ampeleke kwa Bibi yake. Mume wangu wazazi wake wamefariki lakini ana ndugu wengine, kuna Baba mdogo wake na wengine tu ambao wana uwezo.

Sio kama si mtaki moja kwa moja lakini aondoke tu ili niwe sawa maana nahisi naweza kumuua huyu mtoto. Shida ni kwamba mume wangu anampenda sana mtoto na kwakua yeye alilelewa na ndugu baada ya wazazi wake kufariki basi anasema kuwa mwanae hawezi kulelea na mtu mwingine yoyote na aliniambia kabla hata hatujaanza mahusiano, nisaidie kaka nifanye nini maana nahisi kuchanganyikiwa.

Je kama ni wewe ndio unaombwa ushauri kama huu, utamjibu nini, utamuacha salama kweli?

Nenda kaombewe huyo mtoto moyo wake amebeba maombi yako na baraka zako. Kamwe usimtese huyo mtoto omba sana na tubu mno
 
Moto ushuke kutoka mbinguni na kukuteketteza, na dubu watokee msituni na kukuraruaraua. Iwe kwako kama ilivyofanyika kwa wale watu waliowahi kumdhiahki Nabii wa Mungu, Eliya
 
Back
Top Bottom