Mtu akiniuliza kama nimeajiriwa naumia sana rohoni. Kuna mwingine ameshawahi experience hiki?

Mtu akiniuliza kama nimeajiriwa naumia sana rohoni. Kuna mwingine ameshawahi experience hiki?

Balqior

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2021
Posts
2,406
Reaction score
8,039
Sababu baada ya kumaliza chuo nimekosa ajira baada ya ku-apply sana Kazi sijaambulia kupata, sanasana naishiaga kwenye interview. Nimekaa mtaani mda mrefu, hivyo najishughulisha na temporary informal jobs ndogo ndogo.

Mtaani baadhi ya watu wanajua mimi ni mwanachuo, sasa sometimes utakuta mtu hamfahamiani, au jirani, mtu mzima mzee, anakuuliza ajira vipi, unafanya kazi wapi, au kazi fulani zimetoka mbona huja-apply, huwa napata uchungu moyoni.

Kuna ndugu mmoja Hadi sahiv namkwepa sababu kila nikiongea naye kwenye simu anapenda kuniuliza kuhusu kazi.

Je, nakosea nikiwakasirikia hao watu waloniuliza swali kama hilo?
 
Sasa hyo kero ipo San ila usjali mm huwa akinuukiza mwanamke hyo hbr najisikia vibya Sana unamtongoza mwanamke ati anakuambia unafanya Kaz wapi ole wako umuambie huna unatafuta Babu umei sha kbsa humpati huyo demu dawa yao danganya tu.
 
Kwani umeajiriwa?

Kuwa muwazi ukweli siku zote humuweka mtu huru we unaonekana ndo wale jamaa wanapretend life.
Inatakiwa ukiulizwa umeajiriwa unasema bado nipo nipo kama kuna mchongo tushtuane[emoji16]

Heshima itakuja tu muda wake ukifika usiogope kusema we ni jobless[emoji28][emoji28]
 
Sasa hyo kero ipo San ila usjali mm huwa akinuukiza mwanamke hyo hbr najisikia vibya Sana unamtongoza mwanamke ati anakuambia unafanya Kaz wapi ole wako umuambie huna unatafuta Babu umei sha kbsa humpati huyo demu dawa yao danganya tu

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
🤣🤣🤣🤣 Utaambiwa huna mbele wala nyuma kama mche wa sabuni
 
Hadi sahiv namkwepa sababu kila nikiongea naye kwenye simu anapenda kuniuliza kuhusu kazi.

Je nakosea nikiwakasirikia hao watu waloniuliza swali kama hilo

Bora hata hiyo yako

Maswali yanayonikera tukiwa baa na washkaji ni ile wanauliza "umejenga?","umeoa?"

Huwa sijibu maswali ya kipuuzi,najipigia tu funda za konyagi na kulipua embassy...
 
Kwani umeajiriwa?

Kuwa muwazi ukweli siku zote humuweka mtu huru we unaonekana ndo wale jamaa wanapretend life.
Inatakiwa ukiulizwa umeajiriwa unasema bado nipo nipo kama kuna mchongo tushtuane[emoji16]

Heshima itakuja tu muda wake ukifika usiogope kusema we ni jobless[emoji28][emoji28]
Haha definition yako ya mtu ku-pretend life Ni nini, mm naishi kulingana na kipato Kidogo nachokipata Moneytwister
 
Hii mindset yetu vijana kuhusu kazi inanichanganya sana, BTW pole mkuu
 
mkuu usichukulie kila kitu negative wengine wanakuuliza waone kama unaweza fit kwenye fursa walizonazo.
 
Angalia mtu na mtu na jinsi ya kumjibu.

Wengine wanauliza ili tu kukukebei wengine wana nia nzuri.

Ila pia maswali mengine ni too personal yahitaji busara sana kumuuliza mtu mfano: una kazi au umeajiriwa? ulipata division ngapi? Una umri gani? Mshahara wako kiasi gani? Utaoa au kuolewa lini? Umejenga? n.k
 
Mkuu pole Sana!Natamani kutoa michongo,ila Vijana wa Jf wa Me na Ke sio waaminifu huo ndio ukweli.Mkipewa connection maaribu Sana.Sio kwangu hata baadhi ya member maarufu tunaofahamiana nje ya Jf wengine Biashara zao chupu chupu kufa.

Vijana mnapaswa kubadirika.Kuna Mwingine nilipompeleka alipoona Ela anayo badala ya kusepa kistaarabu kaharibu.Niweke wazi ndio maana Pm sizijibu tunasaidiana lakini tatizo uaminifu.Pole ningekupa michongo lakino naogopa yasije yakatokea ya wenzio.
 
Huna haja ya kukasirika, we wapotezee endelea na mambo yako, wengi huwa wanauliza ili wajilinganishe.
 
Back
Top Bottom