Upande wangu nina maoni tofauti sana, Ndoa ni ibada, kwa dini zote, hutaenda peponi ikiwa huna ndoa, ukifanya thawabu zote ukawa huna dhambi kabisa hata moja, lakini rijali Mungu atakuweka kati ya moto na pepo yaani hatakupa pepo ila hatakuingiza motoni.
Ana maana kua hukuingia katika kipimo kikuu alichokiweka kuoa, ukioa omba Mungu kila kukicha mkeo awe muadilifu katika ndoa maaana hakuna calculation ya kumfanya mwanamke au mwanaume atulie au awe wako daima ila Mungu anawezesha wengi kupata ndoa nzuri zenye faraja wanaomuomba, wengine wanapata nafuu.
tumewahi kumcheka jamaa yetu mmoja alioa baamed ndoa kamili ya kikristu, tena bwana alikua na pesa tu, tahamaki tukagundua amepata bahati kubwa ya ajabu, mwanamke yule aliiogopa mno ndoa yake, anajituhumu kila dakika ana hofu mumewe hatamuamini, haendi kwa jirani, haendi sokoni, haendi hovyo popote na akitaka kuondoka kwenda labda msibani ambapo pengine amekwisha mueleza mumewe tayari asubuhi, basi tabu, atampigia mumewe mpaka mara tatu kuomba ruhusa tena wakati huo ni ule ambapo,hakukua na simu ya mkononi, kwa hiyo ya mezani anapigs hivyo mpaka jamaa akawa anamuonea huruma fulani weee unaogopa hivyo nini, akawa anamjibu mimi kwangu chenye thamani ni ndoa. huku wake zetu wanakurupuka mpaka mara tisa kwa siku kwenda sokoni na saluni na madukani kwa masaa, mwenzetu hana wasiwasi, mwanamke alikua anatiliwa mashaka na wazazi wa mume mpaka wakadiriki wazazi wale baada ya miaka kadhaa, wakasema wana hamu walipe ngombe sio vihela vichache alivyolipa mtoto wao, wakasema mtoto wetu amepata mke, ambapo awali walisema mtoto wetu mjinga, mimi ni muislam naona mtihani wa ndoa ndio mgumu sana kuliko mitihani yoooooote, na hata wanaopata 0, wasihuzunike ni kawaida kabisa kupata 0, ila jitahidi uoe ukitoa talaka uoe tena au uoe wake wawili au watatu au wanne, mimi nina wivu kuishi na wake wengi wakiwa mbalimbali, lakini huo nasema ni mtihani mkuu wa dunia ukipata 0 kila ndoa pia sio ajabu jitahidi utapata 100 siku ya mwisho ya hukumu, ila usiwe chanzo cha matatizo ila uwe unatunza ndoa yako usiingilie za wengine.
Saudia Arabia huko maka na madina, ukifumwa una mwanamke ambae hujamuoa tu unauawa kwa panga, kwa hiyo kama hujaoa hutapata mwanamke maana anaogopa kuuawa u kupata hukmu, hukmu ya kiislam kule nidhamu ya ndoa ni 100%, na wako very serious, lakini ukienda wewe utaona ugumu maana hata mwanamke kumuona ni ngumu ukimuona ni mzee asie na matamanio lakini dunia inawaona hawawapi wanawake haki zao, mtihani, mwanamke ni dhahabu kuu ya dunia, anatamaniwa kila kona, ndie kitu ghali kuliko vyote, mi hushngaa ninapowaona watu wakishangaa eti kaolewa kwa ngombe 60, au mwanamme kahonga gari 3, au kamjengea nyumba yeye hana, mwanamke ndie kitu chenye thamani duniani ndivyo Mungu alivyoumba msaidie kazi, mlinde hata kama watakuona una wivu mpeleleze kidogo na dini inakataza usimchunguze eeeeeeeh ndio mtihani ndugu zangu, si unajua mtihani huwa na maswali magumu na yenye kutega ssaaana, fanya tu, hakuna mwenye nafuu na mwanamke mwenyewe nae anatuona sisi mtihani basi maisha ya duniani ni mtihani mkubwa kwa wote, pesa sio solution kwa wanawake, uwezo sio solution, uchamungu at least kidogo una nguvu. lakini ndio dunia ndugu zangu tusi panic, tuombe Mungu sana na tumshukuru Mungu sana siku njema ya wanawake duniani na ijumaa njema na ili uishi mtangulize sana Mwenyezi Mungu, Mungu amlipe mema mengi alhj ali hassan mwinyi aliekuwa rais wa awamu ya Pili, aliwahi kuwajibu kua moja ya sababu ya yeye kuishi miaka mingi ni pamoja na kuoa wake wawili, mmoja unaweza kupata kichaa uki jali sana.
Kwa maisha yetu tumuombe Mungu atuongoze, inshaalah amina.