Mtu aliacha Shule Darasa la 2 anataka kuwa Mbunge? Tutafakari vigezo vya kugombea Ubunge

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2021
Posts
1,183
Reaction score
2,100
Juzi aliyekuwa Naibu Rais wa Kenya, Rigathi Gachagua, alinukuliwa akisema: “Mtu aliacha shule darasa la pili anataka kuwa mbunge? Mtu asiyejua hata neno moja la Kiingereza awe mwakilishi wa wananchi?”

Hii kauli imeibua mjadala mpana kuhusu sifa za msingi zinazopaswa kumfanya mtu astahili kuwa kiongozi wa umma. Ingawa kauli hiyo imeibuliwa katika siasa za Kenya, ujumbe wake unaakisi hali halisi ya siasa katika nchi nyingi za Afrika, ikiwemo Tanzania.

Kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania, mtu anayetaka kugombea ubunge anatakiwa tu awe anajua kusoma na kuandika Kiswahili na awe na akili timamu. Hakuna sharti la elimu ya juu, taaluma maalum, au uelewa wa sheria, uchumi, au masuala ya kimataifa, licha ya kwamba wabunge hawa ndio hujadili, kurekebisha, au kupitisha mikataba na sheria zinazogusa maslahi makubwa ya nchi.

Hali hii imejidhihirisha bungeni mara kadhaa ambapo baadhi ya wabunge hujikuta wakisifia bila kuuliza maswali ya msingi au kupitisha mikataba ya kimataifa ambayo hawaielewi vyema. Kuna ushahidi wa baadhi ya wabunge kuunga mkono kila hoja ya serikali bila kujali athari zake kwa wananchi wao, si kwa sababu wanaamini hoja hiyo ni sahihi, bali kwa sababu ya kukosa uwezo wa kufahamu kwa undani yaliyomo.

Matokeo ya hali hii ni kwamba Bunge linapoteza nafasi yake kama chombo cha kusimamia serikali na kuwa sehemu ya kupitisha maamuzi bila hoja za kina. Mbunge ambaye hana uelewa wa msingi wa sheria, uchumi au utawala bora, hawezi kuwawakilisha ipasavyo wananchi wake katika zama hizi za dunia ya mabadiliko ya haraka.

Kauli ya Gachagua ituamshe na tujiulize maswali magumu, tunawezaje kuhakikisha Bunge linajaa watu wenye weledi, uelewa na uwezo wa kujadili mustakabali wa taifa kwa kina?

Hawa wabunge wa Yessssssssssss kila kitu na kugonga meza hawatufai na sio afya kwa Taifa

Ni huzuni kukubali kuwa hatuna bunge tuna wafuata mkumbo, wasifiaji ambao hawajali maslahi ya Wananchi

Tuamke!!! Taifa lenye uwajibikaji na maendeleo halihitaji Wabunge vilaza!!!
 
Wapo kadhaa niliosoma nao elimu za chini nawafahamu uwezo wao darasani ilikuwa huwapati kwenye 50 bora kunako mitihani ya shule. Sijui walipitapita wapi wakajiunga na siasa na leo hii ni wabunge. Michango yao bungeni haijulikani wanachangia nini na mara nyingi hawana hoja maridhawa. Majimbo yao yako hoi kimaendeleo. Mkiwa na mbunge zero brain ni aibu kwa wananchi wa jimbo hilo kwani huwakilisha wananchi wa jimbo hilo na huonekana wote wana akili kama za mbunge wao
 
Hawatakuelewa kina Msukuma,mtu aanzishe hiyo mada Bungeni,watanywea kuliko maelezo na kutia Huruma!
 
Wapo kadhaa niliosoma nao elimu za chini nawafahamu uwezo wao darasani ilikuwa huwapati kwenye 50 bora kunako mitihani ya shule. Sijui walipitapita wapi wakajiunga na siasa na leo hii ni wabunge. Michango yao bungeni haijulikani wanachangia nini na mara nyingi hawana hoja maridhawa. Majimbo yao yako hoi kimaendeleo. Mkiwa na mbunge zero brain ni aibu kwa wananchi wa jimbo hilo kwani huwakilisha wananchi wa jimbo hilo na huonekana wote wana akili kama za mbunge wao
Tuamke Sasa tupige chini hawa akina timbavandtu!
 
Mimi huwa najiuliza Taifa letu lilianza kupoteza mwelekeo lini?
Maana kama sasa hivi hatuna bunge kabisa!
 
Tuamke Sasa tupige chini hawa akina timbavandtu!
hata tukiwapiga chini kwenye kura za maoni kama juu wanamtaka ataibuka mshindi kupeperusha bendera ya chama kwenye general election, huko nako huibuka kidedea na kutinga bungeni huku akili ni zero brain
 
Juzi aliyekuwa Naibu Rais wa Kenya, Rigathi Gachagua, alinukuliwa akisema: “Mtu aliacha shule darasa la pili anataka kuwa mbunge? Mtu asiyejua hata neno moja la Kiingereza awe mwakilishi wa wananchi?”

Hii kauli imeibua mjadala mpana kuhusu sifa za msingi zinazopaswa kumfanya mtu astahili kuwa kiongozi wa umma. Ingawa kauli hiyo imeibuliwa katika siasa za Kenya, ujumbe wake unaakisi hali halisi ya siasa katika nchi nyingi za Afrika, ikiwemo Tanzania.

Kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania, mtu anayetaka kugombea ubunge anatakiwa tu awe anajua kusoma na kuandika Kiswahili na awe na akili timamu. Hakuna sharti la elimu ya juu, taaluma maalum, au uelewa wa sheria, uchumi, au masuala ya kimataifa, licha ya kwamba wabunge hawa ndio hujadili, kurekebisha, au kupitisha mikataba na sheria zinazogusa maslahi makubwa ya nchi.

Hali hii imejidhihirisha bungeni mara kadhaa ambapo baadhi ya wabunge hujikuta wakisifia bila kuuliza maswali ya msingi au kupitisha mikataba ya kimataifa ambayo hawaielewi vyema. Kuna ushahidi wa baadhi ya wabunge kuunga mkono kila hoja ya serikali bila kujali athari zake kwa wananchi wao, si kwa sababu wanaamini hoja hiyo ni sahihi, bali kwa sababu ya kukosa uwezo wa kufahamu kwa undani yaliyomo.

Matokeo ya hali hii ni kwamba Bunge linapoteza nafasi yake kama chombo cha kusimamia serikali na kuwa sehemu ya kupitisha maamuzi bila hoja za kina. Mbunge ambaye hana uelewa wa msingi wa sheria, uchumi au utawala bora, hawezi kuwawakilisha ipasavyo wananchi wake katika zama hizi za dunia ya mabadiliko ya haraka.

Kauli ya Gachagua ituamshe na tujiulize maswali magumu, tunawezaje kuhakikisha Bunge linajaa watu wenye weledi, uelewa na uwezo wa kujadili mustakabali wa taifa kwa kina?

Hawa wabunge wa Yessssssssssss kila kitu na kugonga meza hawatufai na sio afya kwa Taifa

Ni huzuni kukubali kuwa hatuna bunge tuna wafuata mkumbo, wasifiaji ambao hawajali maslahi ya Wananchi

Tuamke!!! Taifa lenye uwajibikaji na maendeleo halihitaji Wabunge vilaza!!!
Pamoja na darasa lake la pili CCM ikimtaka hata ufanyeje atakuwa mbunge wako tu, na ukichonga mdomo sana utapotezwa.
 
Huwezi kua na wakina msukuma Bungeni alafu hiyo nchi iko serious hii Mihimili Bunge na Mahakama zikiwa strong hata serikali itawajibika ipasavyo Spika wa Bunge hatakiwi kua Mbunge wa chama chochote cha siasa wala kuteuliwa na Bunge
 
Back
Top Bottom