MTAZAMO
Platinum Member
- Feb 8, 2011
- 20,203
- 35,840
Wakuu,
Kwenye mapito ya maisha unaweza kupitia mambo mengi ukifikiri imetokea tu kumbe Mungu anakuandaa na nyakati ngumu. Muogope mtu ambaye aliandaliwa na Mungu kuvuka nyakati ngumu.
Tunajua makomandoo wa Jeshi lolote huandaliwa kukabiliana na nyakati ngumu. Lakini hawa huweza kuvumilia kwa kiwango kile kile walichofundishwa. Lakini mtu aliyeandaliwa na Mungu kwa nyakati ngumu uvumilivu wake huwa unalindwa divinely na Mungu mwenyewe sio usugu wake binafsi.
Nina uhakika ukikaa na Tundu Lissu na kufatilia kuanzia kuzaliwa kwake, mapito yake ya shule hadi harakati zake kote alikopitia hata yeye binafsi hajui alivukavuka vipi.
Harakati zake kule migodini hakujua anajiandaa na nini, risasi zile kumi na sita mwilini hajui ameponaje! Lakini kitu kilichozaliwa ndani yake baada ya hapo ni Mungu pekee ndio anaweza kubadili hatma sio mtu au kikundi cha watu.
Leo nimetafakari sana kiwango chake cha kuhimili magumu haya, nikasikia sauti ndogo ndani yangu ikisema "si yeye ni YEYE" ( asemavyo Pascal Mayalla ). Sisi tuendelee kumuombea lakini mtu yeyote anayeamini hata kidogo uwepo wa YEYE aepuke dhuluma juu ya huyu mtu maana anashindana na YEYE bila kujua!