Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli
Elimu Kazi yake kûbwa ni kumkomboa Mtu ndiye Mwanamke na Mwanaume kifikra.
Haiwezeniki Mtu kafika chuo Kikuu, amesoma degree au katika chuo cha Kati akasoma stashahada akaibusti Akili Yake Akaelimika alafu Wakati wa kuchumbia au Kuoa au kuolewa akakubali Kutoa au kutolewa mahari.
Mtu aliyesoma au Mtu yeyote àmbaye akili yake Iko Huru na inachaji hawezi kushindwa kujua kuwa mahari ni biashara haramu ya kumnunua Mwanamke
Sisi Watibeli hata kusingekuwa na shule Kabisa, tusingeshindwa kujua kuwa Mahari ni biashara haramu àmbayo Watu hawapaswi kuifanya. Tunajua Jambo hili Kwa sababu ya haki, ukweli, maarifa na upendo.
Huwezi mnunua Mtu bhana tenà Mtu unayempenda Kwa Kile ambacho Mila na desturi potofu zilikiita Mahari ili kupumbaza Watu.
Wanawake hawawezi kuwa na Haki Sawa na Wanaume ilhali waô wananunuliwa kimafungu kama Mbuzi.
Sisi Watibeli hatufanya Vitu kuridhisha Watu hata kama Watu hao ni wazazi wetu, Watoto wetu, ndugu zetu, wake zetu ilhali Vitu hivyo tunajua NI dhulma, ukatili, udhalilishaji, na uovu.
Nafahamu Watu wengi wanajua kuwa Mahari ni biashara haramu lakini hawanabudi kufanya ili kuridhisha Wazazi na ndugu na Mila. Jambo hilo Kamwe Sisi Watibeli hatutafanya.
Watoto wàngu, Jambo lolote ambalo mnajua ni ovu na siô Haki Kamwe msilifanye Kwa lengo la kuniridhisha Mimi Baba Yenu au kumridhisha Mama Yenu.
Wazazi Bila aibu mnakaa mnajadili na kupanga bei ya Binti Yenu. Kisha kijana naye anakuja kutajiwa bei Kisha ati mnashushana bei mara Milioni nne. Mwanaume anasema Nina Milioni Mbili unusu, ooh mnamwambia tatu mwisho kama mnauza tukutuku.
Mimi kama Mtibeli siwezi kufanya wala kujadili uharamu wa namna hiyo.
Kama tunajadili kuhusu kununua Ng'ombe Sawa lakini kununua Mtu sijui Mwanamke alafu mnaleta unafiki kuwa hamuuzi ila NI Mahari sijui shukrani. Shukrani gàni inapangwa na Mpokeaji?
Kwamba ati uniletee Laki tisa kama Shukrani ya kumchukua Binti yàngu. Hivi Akili zenu zinafanya Kazi Sawasawa.
Huyo siô Mimi, hao siô Watibeli. Watibeli hawatoi Mahari wala Binti zetu hawatolewi Mahari. Kwa sababu Binti zetu ni Watu Huru, hawanunuliki.Hatuwezi kuwathaminisha ati huyu nipe kiasi kadhaa nikupatie awe Mkeo.
Mmekubaliana Huko njooni Kwetu Wazazi mjitambulishe, tuwaone na kuwajua, mtujue, tufurahi. Tuwabariki. Full stop!
Watibeli tunatambua adhabu Kwa Watoto wetu. Ikiwa Watoto watakiuka Baadhi ya Sheria mfano wamekutana juu Kwa juu Huko wakabebeshana Mimba pasipo kûja nyumbani kutambulishana ni ruhusa Kwa Wazazi kuwapa adhabu na hiyo adhabu lazima iwahusu watoto wôte wawili, yàani Kijana na Binti wôte lazima wawajibike na siô kumpa adhabu Mtu mmoja. Hiyo ndîo haki.
Kumpa adhabu kijana pekee ni dhulma, ukatili, uonevu na hii humfanya kijana awe katika mazîngira ya kuona anammiliki Binti Jambo ambalo siô kwèli. Hii hufanya unyanyasaji na ukatili baadaye utokee.
Wamepeana Mimba, wôte wamekosea, kama adhabu NI kutoa Pesa, Basi wôte watoe Pesa mmoja kama ni Laki tano Basi kîla Mtu atoe Laki Mbili unusu. Wakiamua kushirikiana siô kesi Acha washirikiane. Hizô Pesa zipelekwe Kwa familia ya upande Binti na familia ya kijana Nusu Kwa Nusu.
Watu walale Kwa starehe zào Kwa mapenzi Yao alafu ninyi mseme ati Binti Yenu ameharibiwa hivi mnaakili Sawasawa. Binti anayeharibiwa NI Yule àmbaye hajafikia Umri wa Ûtu uzima. Huyo kaharibiwa na Sheria lazima zichukue mkondo wake.
Mabinti msikubali kutolewa Mahari. Vijana msikubali Kutoa Mahari. Wazazi msiuze mabinti zenu.
Unakuta familia inamnyanyasa Binti Kisa ilimnunua Kwa Milioni Moja.
Binti Fanya Kazi. Kazi ndîo Ûtu wako. Kazi itakufanya uheshimike. Usikubali kutolewa mahari. Ikiwa alikutolea mahari, na unaona anatumia uanaume wake kukunyanyasa, mrudishie mahari Yake.
Usikubali Kupewa talaka Kabla hujarudisha Mahari ya Watu kama alikutolea mahari. Huo ni utapeli. Wewe ulinunuliwa tuu Rudisha mahari ya watu
Oooh! Nilimzalia Watoto hivyo sirudishi Pesa. Ndivyo Akili za Watumwa zilivyo. Mtu Huru au mwenye Akili zilizotimia Huwezi kuongea maneno ya ajabu na hovyo namna hiyo. Kwamba ulinunuliwa ili ukazae Sasa Kazi ushafanya hivyo hudaiwi.
Ndîo maana Wanaume Huona Watoto ni haki Yao Kwa sababu waliwanunua. Mtoto ni Baba na Mama. Kisayansi na Kiroho. Hata kihaki Ipo hivyo Ila kibiashara Mtoto ni Wa baba Kwa sababu alishamnunua Mwanamke. Kwa wale Wanaofanya hizô biashara haramu.
Hakufanya ubaya na Jambo ambalo tunaliona halipo Sawa kumridhisha yeyote.
Acha nipumzike sasa
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa Sasa Dar es salaam