Uchaguzi 2020 Mtu ambaye Wanadamu hawakutaka aishi, lakini leo hii Mtu huyu anakwenda kuwa Mgombea wa Urais. Jambo hili lina maana gani?

Kama ni hivyo ina maana yanayofanyika ni maigizo siyo...!?
Pamoja na hayo huyo mwenyekiti wa tume labda akatangazie matokeo nchi nyingine.
Kwa kifupi katiba ndio utakayowasumbua upinzani . Haiwekani viongozi wote wa tume wateukiwe na rais alafu eti hao hao wamtangaze mtu mwingine.
 

Kazi ipo hapo October 28
 
Kanza sasa kumuombea kura kwa ndugu na Jamaa zako wote, hakikisha wanapiga kura kwelikweli halafu huenda zitahesabiwa wazi. Yeye kasema safari hii hataachiwa Mungu, Bali repoti TU ndio itaenda huko!
Me namkubali sana Lissu ila Wewe jamaa unapenda sana kujifariji na bahati mbaya Chadema uchaguzi huu haitapata hata kura laki 5 achilia mbali kiti cha ubunge
 
Mnajipa matokeo mkishindwa muwanze kulialia vyombo vya nje viingilie.

Uzeeni sera. Lissu hawezi endesha nchi kwa hoja ya kupigwa risasi.


unashangaa kipi hapa..

Yanga FC kufungwa na MBAO FC au

Daby County kutoka draw na Man U.??

halafu sera haziuzwi.
 

Binadamu wate walio hai, wanafikiri na mawazo, lakini hua yanatofautiana, na sio lazima tuwe na fikra moja na maono ya namna moja, even TWINS can differ in thoughts.

Kuna mambo mengine tunamsingizia Mungu lakini ni mambo na mbinu za mwanadamu, Mungu ametupa akili tofauti na wanyama wengine.
walio pamga kumuuwa LISSU walikuwa binadamu wenye nia Mbaya, na sasa wanaojenga UMAARUFU wake ni wanadamu waliokaa na wakafirikia vizuri namna ya kuitumia nafasi/fursa hii na kuzitumia Huruma za watanzania ili kukiletea manufaa Chama chao na Lissu mwenyewe. So this is a Human plan, na wameitumia vizuri na kwa ufanisi. Tusijaribu kulifanya ni Tendo la Miujiza, Hapana sio Miujiza, bali ni Proper & Intelligent Planing iliyopikwa kwa miaka mitatu, na mipango ilikuwa ni mingi sana, hii ya leo ndiyo iliyofanikiwa. Hata ACT walitayarisha plan yao iwapo angeamua kujiunga nao.

Sio ukweli kuwa wengi hatukuamini kuwa LISSU atarudi, Jilo lilikuwa Wajibu wake kuwajuza watu, na uwezo au uamuzi wa kurudi au kuwa Mkimbizi.
 
Pamoja na hayo huyo mwenyekiti wa tume labda akatangazie matokeo nchi nyingine.
Kwa kifupi katiba ndio utakayowasumbua upinzani . Haiwekani viongozi wote wa tume wateukiwe na rais alafu eti hao hao wamtangaze mtu mwingine.

Kama akitangaza kuwa mwingine kashinda pale Mwl Nyerere hall, atangazwe Lissu hivi hao wengine, magu na washirika wake watamfanyaje mwenyekiti maana tunajua akishatangazwa mshindi ndio basi..!
Wataenda mahakani au watalala barabarani, au nini watafanya haswa... watamfunga, kumteka ama...!?!!
[emoji848]
 
TAL ana nia na maadui wanao julikana, hata na watoto wadogo! Usiturudishe kwenye asilimia mia zako za gizani wakati ukweli upo wazi! Kama alikua tayari kufa ili kutufumbulia yaliyo fichwa, tupate wapi tena mtu kama huyu wa kuuongoza taifa letu????? #sasabasi
 
Huyo ndo Yesu Kristu wa Kweli Sasa (Achana na Yule feki) kutoka jamhuri ya Push
Mafarisayo,Masadukayo hawakutaka Yesu Aishi... Wakamdhihaki ,wakampiga wakamuwamba mtini....Ila siku ya Tatu akafufuka,akapaa Juu Mbinguni

Usimfananishw Kristo na mambo ya ajabu ajabu.
 
Inawezekana muujiza kweli haupo hapo kwenye mipango ya miaka, lakini kutokufa kwa Lisu siyo man making! Huwezi kutengeneza hiyo, na hii mipango/fursa yenye umri wa miaka mitatu sasa, ina mkono wa Mungu!
 
Hana uthubutu huo kwanza
 
Pamoja na hayo huyo mwenyekiti wa tume labda akatangazie matokeo nchi nyingine.
Kwa kifupi katiba ndio utakayowasumbua upinzani . Haiwekani viongozi wote wa tume wateukiwe na rais alafu eti hao hao wamtangaze mtu mwingine.
Hebu tuwe tu wa kweli.
Kwani Mwenyekiti wa Tume akimtangaza Mshindi wa Urais toka Chama cha Upinzani haina shida yoyote kwake mana tayari amiri Jeshi Mkuu atakua ni wa chama kilichotangazwa.

Tatizo ni kupata kura za kutosha. Kwa katiba yetu Chama kinachopata kura Nyingi ndicho kinachotangazwa.
Ndio maana kama ni wizi basi unafanyika kabla ya kura kuhesabiwa na kuwekwa hadharani.
Mtu akishashinda kwa kura My Friend sio mwenzako na akitangazwa hakuna mtu tena wa kumsulubu Mwenyekiti wa Tume.
Kule Zanzibar inakua hivyo hivyo ila tatizo ni Serikali ya Muungano ambayo inakua ndiyo iliyoshika Dola lote la Muungano.

Akitangazwa Mshindi basi ujue ndio mamlaka mpya.
Suala linalosumbua ni ule urafiki wa wazee walioshika madaraka kwenye tume na wale walioteuliwa kuwa na hofu na nafasi zao akija mtu mwingine lakini Katiba haina tatizo kumtangaza Mshindi wa Chama kingine Bali watendaji waliolewa madaraka wanakua na hofu ya kukosa madaraka akija kiongozi mwingine.

Suala sio tu katiba lakini ni viongozi wabinafsi wanaokula viapo vya uongo huku wakiwa wameshika Misahafu ya dini na Katiba.
Ilipaswa viapo hivyo vitolewe na viongozi wa Kidini au kimila ili anayekiuka ajikute akisomewa dua mbaya au alibadiri na kuwa vichaa.

Kwa Tanzania bado upinzani haujaweza kuchukua nchi kwa kura mana kura zao ni Chache sana labda mwaka huu ambao pia unaonekana bado kuna mikoa kama Dodoma Geita,Shimiyu, Manyara, Tabora, Rukwa, Songea, Pwani n.k ambayo ushindi kwa CCM kwenye Ubunge unaonekana wazi kuwa utakua ni 100%. Lakini siku ikitokea wananchi wameamua kuwapa wapinzani Kura basi ni rahisi sana kwa Mwenyekiti wa Tume kuwatangaza mana kuanzia wabunge ,madiwani na urais watakua wamepata kura za Kutosha.

Wahamasisheni watu wapige kura mshinde kwa wingi wa kura ndio mtatangazwa lakini kwa sasa ni woga tu ndio unatangazwa na CCM bado kwa ujumla tangu 1995 wamekua wakishinda kwa zaidi ya 50%+
 
Maisha ya Mwanadamu yako mikononi mwa Mungu
 
Halafu kuna watu wanasema hakuna Mungu! Risasi moja ya SMG inaua tembo lakini 16 hazikuua mtu lazima ni Mungu.

Na kama Mungu akipenda hata jiwe la changarawe linakuondosha kama David alivyomdondosha goliati. Acheni Mungu aitwe Mungu!
Zinaweza kutua hata 20 Bullets mwilini na usife... ila Trust me, it only takes One Bullet to kill a person. Sema sasa inategemea hiyo risasi imelenga wapi.
Binafsi sipendi bullets hata kidogo.
 
Ukimsikiliza Tundu Lissu anaongea zaidi kwa huzuni kuliko hasira sio kama anavyofanya mpinzani wake meko.

Tundu Lissu anaendelea KUSEMA Watanzania wamepoteza maisha yao na kazi zao:kutokana na rais ambaye hasemeleki hataki kukosolewa, analaumu wengine, anakataa ushirikiano na mpenda chuki.
 
Wauaji wake wanaona aibu kubwa sn na damu ya jamaa inawatesa vibaya sn
 
Maisha ya Mwanadamu yako mikononi mwa Mungu
Je hawa watu wanaouawawa kila siku duniani kote vipi, Je kwa hiyo Mungu amependa wao wafe?
Mungu ametupa Akili tujitafutie Maarifa na yote tunayofanya au kuamua hayo ni mwanadamu mwenyewe.
Mengine mengi Mungu katuachia tuamue wenyewe.
Mungu angeamua yote ya wanadamu basi duniani kusingekuwa na Masumbufu, Sababu rahisi tu angetuweka kwenye "Mstari mnyoofu". Lakini hafanyi hivo sababu amatupatia Akili tuamue mambo wenyewe. Likiwa baya poa, likiwa jema poa. Katuachia wenyewe. Ndo maana mambo Mazuri na Mabaya yote yapo duniani!
 
Woyoooooo.. Tundu Lissu all the way.

#NiYeye #NiZamuYaTunduLissuJamani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…