Mtu amejenga tulipomzika babu yetu. Tufanye nini kupata mwili wa baba yetu tukauzike pengine?

Witiri

Member
Joined
Dec 12, 2022
Posts
57
Reaction score
73
Habari za muda huu wakuu!

Kuna mtu amejenga nyumba yake mahali tulipomzika baba yetu mzazi na alikuwa anajua kuwa mahali pale amezikwa mtu na alishiriki wakati akiwa kijana kumzika mzee wetu.

Kilichotokea ni kwamba eneo alilozikwa mzee wetu lilikuwa mi eneo la babu na bibi ila kuna baba yetu mdogo alimuuzia huyo bwana aliyejenga.

Wazee waliobakia ambao ni baba zetu wadogo pia walienda kuongea na mhusika aliyejenga kumuomba walau wafukukue ili wapate mabaki kisha wahamishe pahala pengine ila yule mhusika amekataa.

Je, tufanye nini ili tuweze kupata mwili wa baba yetu tukauzike mahali ambapo tunaweza kwenda kuona kabuli lake?
 
Yaan alivunjavunja msalaba akajenga nyumba au sijaelewa au nyinyi ndio wale kaburi mnaweka kitofali na chungu kuonyesha hapa kuna kaburi baada ya mvua kupigapiga kitofali kikiisha panaonekana km pako kawaida tu kumbe chini kuna mifupa ya mtu?
 
hapo alipozika bado pako ktk umiliki wenu au ktk umiliki wake? Maana ukishaniuzia mkate hauwezi kunipangia niule mkavu au niutowezee,wakati mnapauza hamkufahamu kuwa pana kaburi la mpendwa wenu? Na je hamkujua kama pataendelezwa na mkatoa hayo mabaki mapema? Msimsumbue mtu na eneo lake na kuwapa hayo mabaki inabaki ni hisani yake,nakupa maneno makali lakini ndio ukweli unaotakiwa kuutambua,siku njema!
 
habari za muda huu wakuu! kuna mtu amejenga nyumaba yake mahali tulipomzika baba yetu mzazi na alikuwa anajua kuwa mahali pale amezikwa mtu na alishiriki wakati akiwa kijana kumzika mzee wetu, kilichotokea ni kwamba eneo alilozikwa mzee wetu lilikuwa mi eneo la babu na bibi ila kuna baba yetu mdogo alimuuzia huyo bwana aliyejenga. Wazee waliobakia ambao ni baba zetu wadogo pia walienda kuongea na mhusika aliyejenga kumuomba walau wafukukue ili wapate mabaki kisha wahamishe pahala pengine ila yule mhusika amekataa, je tufanye nini ili tuweze kupata mwili wa baba yetu tukauzike mahali ambapo tunaweza kwenda kuona kabuli lake?
Tembelea hapa. Mama Samia Legal Aid Campaign utapata msaada

🤣🤣🤣 hii dunia hii....kwahiyo anajua Pana Nini afu ameng'ang'ana? Aisee,huyo angeondoka mwenyewe bila kuaga🤒 si anajifanya kapinda
Muulize palikuwa na misalaba akaibomoa?
 
Website hii hapa

hapo alipozika bado pako ktk umiliki wenu au ktk umiliki wake? Maana ukishaniuzia mkate hauwezi kunipangia niule mkavu au niutowezee,wakati mnapauza hamkufahamu kuwa pana kaburi la mpendwa wenu? Na je hamkujua kama pataendelezwa na mkatoa hayo mabaki mapema? Msimsumbue mtu na eneo lake na kuwapa hayo mabaki inabaki ni hisani yake,nakupa maneno makali lakini ndio ukweli unaotakiwa kuutambua,siku njema!
Waliona pesa ndio ya muhimu zaidi kuliko hayo mabaki
 
Muulize palikuwa na misalaba akaibomoa?
Hapana,Sina haja ya kuuliza... maelezo yake yanajitosheleza mkuu.Kasema huyo aliyenunua na kujenga alikuwepo hata wa kuzika marehemu.Huoni kama hicho ni kiburi?
 
🤣🤣🤣 hii dunia hii....kwahiyo anajua Pana Nini afu ameng'ang'ana? Aisee,huyo angeondoka mwenyewe bila kuaga🤒 si anajifanya kapinda
🤣🤣🤣 ila tuwe wakweli je kosa lake ni lipi? Eneo kanunua na anafanya uendelezaji je amekosea? Wamekosea hao wameuza nguo kumbe ndani ya mfuko kuna pesa🤣🤣🤣
 
Alijua pia kuwa panakaburi....kafanya ubabe tu ....
 
Yaan alivunjavunja msalaba akajenga nyumba au sijaelewa au nyinyi ndio wale kaburi mnaweka kitofali na chungu kuonyesha hapa kuna kaburi baada ya mvua kupigapiga kitofali kikiisha panaonekana km pako kawaida tu kumbe chini kuna mifupa ya mtu?
Waliweka tu alama, unajua watu wa vijijini mazishi yao waliowengi haswa miaka ya 96 walikuwa wanafanya kama ulivyosema. ila huyo mnunuzi alishiriki kuzika pale kabla hajapanunua na alikuwa anaishi jirani tu
 
Tembelea hapa. Mama Samia Legal Aid Campaign utapata msaada

hatopata msaada wowote ambao unaweza kumuumiza huyo mtu kwakuwa wanakiri kuwa wamemuuzia na ujue vijijini uwa hakuna eneo maalum la kuzikia watu la umma ila kila koo utenga eneo kwa ajili ya shughuli hyo na wao wameweka pesa mbele wakamega eneo na kuuza sasa hapo wanasheria wanataka kuwapa tu pesa ya bure labda wawe wanasheria wa bure na hata wao watawapa makavu asubuhi tu🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom