Mtu amejenga tulipomzika babu yetu. Tufanye nini kupata mwili wa baba yetu tukauzike pengine?

Poleni sana. Msishindane naye huyo, anajua anachokifanya na anafanya kwa makusudi.
Cha msingi watafuteni wazee wa eneo hilo wawasaidieni ikiwemo serikali ya mitaa/kijiji
Kimaadili na kiutamaduni ana wajibu wa kuwaruhusu mkafukue na kuhamisha mabaki ya wapendwa wenu.
Hata serikali inapoamua kufanya shughuli za maendeleo kwenye maeneo yenye makaburi hutumia busara na wajibu wa kiutamaduni na kimaadili kwa kuhamisha kwanza makaburi ndipo inaendelea na projects zake.
asante kiongozi, hamna namna ni kuachana nae tu
 
Ni kweli mkuu, nashukuru sana
utapigiwa miruzi mingi sana ila kubwa ni tizama mbele maisha bado yapo na binadamu anahukumiwa kwanza na dhamira alafu ndio matendo,nyie kama dhamira yenu ni kumuenzi mzee wenu basi fanyeni dua na kumtakia msamaha uko aliko na kama mnataka kufanya matendo basi yale aliyokuwa anawakanya yaacheni kadri ya uwezo wenu na aliyokuwa anawakazania kuyafanya,fanyeni sana ila yasiwe yake yenye kumchukiza Mungu,mengine changamsha baraza!
 
Wewe ushawahi kununua kaburi lenye msalaba juu na ukalibomoa sababu halikuhusu wewe mnunuzi ukafurahia show?
Kwa hiyo hii mada ni kwa ajili ya waliowahi kununua makaburi yenye misalaba tu?
Halafu elewa kwamba Kaburi ni Kaburi msalaba hauongezi wala kupunguza kitu mbele ya sheria au maadili na utamaduni. Ina maana wasioweka misaraba ya kwao siyo makaburi?
 
Sasa wanajua kitofali na chungu kilipo au eneo la kaburi waliweka uzio kuzunguka alipozikiwa marehemu? Au watachimbachimba tu kila sehemu kuisaka mifupa ilipo?
wazee wangu wanajua hadi chumba ambapo kaburi lipo
 
utapigiwa miruzi mingi sana ila kubwa ni tizama mbele maisha bado yapo na binadamu anahukumiwa kwanza na dhamira alafu ndio matendo,nyie kama dhamira yenu ni kumuenzi mzee wenu basi fanyeni dua na kumtakia msamaha uko aliko na kama mnataka kufanya matendo basi yale aliyokuwa anawakanya yaacheni kadri ya uwezo wenu na aliyokuwa anawakazania kuyafanya,fanyeni sana ila yasiwe yake yenye kumchukiza Mungu,mengine changamsha baraza!
shukrani kiongozi, nimepokea ushauri
 
Sasa wanajua kitofali na chungu kilipo au eneo la kaburi waliweka uzio kuzunguka alipozikiwa marehemu? Au watachimbachimba tu kila sehemu kuisaka mifupa ilipo?
Kwa maelezo yake wanajua vyema maeneo waliyowapukzisha
 
wazee wangu wanajua hadi chumba ambapo kaburi lipo
Wao ndio walioijenga hio nyumba kwanini sasa wakati wanaijenga hawafanya utaratibu wa kuondoa hayo mabaki km ni hivyo? Maana basi itakuwa wamefanya kusudi ili wajenge kisha baadae ndio waje kufukua huoni km sio jambo zuri km walijua kabla kwanini hawakuondoa kabla? Mpaka leo hicho chumba kina chungu na kitofali?
 
Soma upya mada mkuu
 
Hii inaonyesha nyie ndiye wenye makosa. Kwa nini mlisubiri ajenge mpaka amalize ndiyo mnataka kufukua? Mtabomoa hiyo nyumba kabla ya kufukuwa au mtafanyaje?
infact eneo liliuzwa kinyemela tu, hata hivyo wazee wenye akili timamu walienda kumuoba kwa kutambua makosa alofanya ndugu yao ili wapate kufukua, ila ana haki ya kukataa au kukubali isipokuwa wao wanaona kama yule bwana ni kiburi sababu alishiriki kuzika mazishi
 
Hicho chumba nimeuliza km wanajua kwanini hawakutoa kabla hajajenga au mpaka leo kwenye hicho chumba kuna chungu na kitofali?
baada ya kuuzwa huyo muuzji alikuwa ana kaa kwake ambapo ni mbali na pale hivyo hata ujenzi wakti unaendlea hakuwepo na hakujali
 
Kwa hiyo hii mada ni kwa ajili ya waliowahi kununua makaburi yenye misalaba tu?
Halafu elewa kwamba Kaburi ni Kaburi msalaba hauongezi wala kupunguza kitu mbele ya sheria au maadili na utamaduni. Ina maana wasioweka misaraba ya kwao siyo makaburi?
Msalaba ni alama kaburini maana yake hapa kuna kaburi usipitishe katapila lako pitisha kanisa likushukie
 
Wao ndio walioijenga hio nyumba kwanini sasa wakati wanaijenga hawafanya utaratibu wa kuondoa hayo mabaki km ni hivyo? Maana basi itakuwa wamefanya kusudi ili wajenge kisha baadae ndio waje kufukua huoni km sio jambo zuri km walijua kabla kwanini hawakuondoa kabla? Mpaka leo hicho chumba kina chungu na kitofali?
hiyo nyumba ni imeisha na watu wanaishi mbona yan maana yake kuna sakafu yenye tairizi
 
baada ya kuuzwa huyo muuzji alikuwa ana kaa kwake ambapo ni mbali na pale hivyo hata ujenzi wakti unaendlea hakuwepo na hakujali
Hakuwepo na hakujali wahusika wakuu waliowaambia hayo walichukua hatua gani au hawakuchukua hatua yoyote na wao ndio waliojenga kwanini ujenzi ukiwa unaendelea wasitoe mabaki watake kwenda kutoa leo huoni hilo ni jambo la kushangaza?
 
hiyo nyumba ni imeisha na watu wanaishi mbona yan maana yake kuna sakafu yenye tairizi
Ndio nimekuuliza kwanini mwanzo pale wakati ujenzi unaendelea hao ndugu wanaosema kuna kaburi kwanini pale pale mwanzo kabla nyumba haijafika kwenye lenta hawakwenda kueleza kwamba wanataka wayachukue mabaki ya mpendwa wao kwanza au ndio walikua wanatumbua pesa kwanza? Zimeisha ndio wanakumbuka kumbe pale kulikua na mabaki yetu si ndio?
 
infact eneo liliuzwa kinyemela tu, hata hivyo wazee wenye akili timamu walienda kumuoba kwa kutambua makosa alofanya ndugu yao ili wapate kufukua, ila ana haki ya kukataa au kukubali isipokuwa wao wanaona kama yule bwana ni kiburi sababu alishiriki kuzika mazishi
kuzika au kutozika hakumuondolei haki yake na anaweza kukana pia kuwa hakuwepo je una ushahidi? Suala ni kuwa amejenga kwake full stop! Wewe haujawahi kwenda kuomba msaada kwa ndugu au jamaa mwenye unafuu wa maisha na akakunyima na ukampa tafsiri kuwa ni mchoyo au ana kiburi? Kumuona ana kiburi au vinginevyo ni mizania mliyoiamua ila kaeni mtafakari mtajua kuwa hakukosea kuwanyima na kama eneo bado la umma mngeenda kulidai mapema ila wote kama ukoo mmekubali ni kwake sasa mnataka kumsumbua na eneo lake? Zingatia ushauri niliokupa ndugu,fanya yenye kuweza kuleta mkate mezani mengine yaweke ktk mfumo wa maombi na matendo mema kwa mzazi wako!
 
ni umiliki wake, sababu aliuziwa na baba mdogo amabe alifanya tu kwa tamaa zake. hata mimi nimeona kuna ugumu ndio maana nikaomba mawazo mbadala
WITIRI, hata hayo mawazo mbadala yana UGUMU wa kiwango kilekile au zaidi
 
infact eneo liliuzwa kinyemela tu, hata hivyo wazee wenye akili timamu walienda kumuoba kwa kutambua makosa alofanya ndugu yao ili wapate kufukua, ila ana haki ya kukataa au kukubali isipokuwa wao wanaona kama yule bwana ni kiburi sababu alishiriki kuzika mazishi
''Kuuzwa kinyemela'' ina maana gani hapa? Je, aliyeuza hakuwa na haki ya kuuza? Kama alikuwa na haki ya kuuza huwezi kusema kuwa aliuza kinyemela. Anyways, suala lako lina mashiko zaidi kwenye mambo ya ''ubinadamu, mila na desturi'' kuliko sheria. Yaani ni kuwa huyo aliyeuza nahuyo aliyenunua wameonyesha hawana utu na hawazingatii mila na desturi ila kisheria hawana makosa yoyote. Kuna swali moja ambalo hujalijibu: Akiwakubalia kufukuwa huo mwili, hiyo nyumba aliyojenga mtabomoa kabla ya kufukuwa? Na mkibomoa, baada ya kufukuwa, mtaijenga?
 
Back
Top Bottom