Mtu amejenga tulipomzika babu yetu. Tufanye nini kupata mwili wa baba yetu tukauzike pengine?

Mtu amejenga tulipomzika babu yetu. Tufanye nini kupata mwili wa baba yetu tukauzike pengine?

Hicho chumba nimeuliza km wanajua kwanini hawakutoa kabla hajajenga au mpaka leo kwenye hicho chumba kuna chungu na kitofali?
Wakati yote yanayokea, wao walikuwa wadogo.
Sasa hivi wamekuwa ndiyo wameona kuna namna wanatakiwa kuchukua hatua.
Kwakuwa jamaa ameshajenga juu ya hayo makaburi hakuna namna tena, waachane na hilo swala waendelee na maisha yao.
 
''Kuuzwa kinyemela'' ina maana gani hapa? Je, aliyeuza hakuwa na haki ya kuuza? Kama alikuwa na haki ya kuuza huwezi kusema kuwa aliuza kinyemela. Anyways, suala lako lina mashiko zaidi kwenye mambo ya ''ubinadamu, mila na desturi'' kuliko sheria. Yaani ni kuwa huyo aliyeuza nahuyo aliyenunua wameonyesha hawana utu na hawazingatii mila na desturi ila kisheria hawana makosa yoyote. Kuna swali moja ambalo hujalijibu: Akiwakubalia kufukuwa huo mwili, hiyo nyumba aliyojenga mtabomoa kabla ya kufukuwa? Na mkibomoa, baada ya kufukuwa, mtaijenga?
umenena vyema sana,wakibomoa na wakijenga ile pesa yote waliyouza eneo italingana ma yakujengea,watakuwa wanamsumbua marehemu🤣🤣🤣
 
Wakati yote yanayokea, wao walikuwa wadogo.
Sasa hivi wamekuwa ndiyo wameona kuna namna wanatakiwa kuchukua hatua.
Kwakuwa jamaa ameshajenga juu ya hayo makaburi hakuna namna tena, waachane na hilo swala waendelee na maisha yao.
Waliofanya uzembe ni hao ndugu waliowaambia pale kuna kaburi na wakati panajengwa wao walikuwepo hawakwenda kuondoa mabaki walikua wanasubiria nini ajenge amalize ndio waende kumwambia chumba hiki kina kaburi tunataka kufukua?
 
nyie ni wachokonozi wapenda chookochoko gharama za kurejesha nyumba kwenye hali yake mtaifidia na je kama mtabashiri kila sehemu na kuharibu jengo mkakosa mwili mtafidia.... mkae chini mjipange maana unaeza kuta alishafukua na kwenda kuutupa kwingine....(mnachotaka mkute hakipo)
binafsi nilishawahi kununua eneo usukumani lilikuwa na mkwaju na limti kama ishara ya kaburi....aliyeniuzia akasema mti huu sjakuuzia ntakuja kuchooma mkaa(hapo mimi i mgeni hajaniambia mambo ya kaburi wala nini) kuja kuwaonyesha washikaji site wananiambia hapa ni ishara ya kaburi....nikawa na hamu jamaa aje akate mti wake niukate na hilo lenye ishara ya kaburi....miaka ikapita nakuta watu wamefanya ishara za kishirikina kwenye mkwaju...siku moja isiyo najina nikaukata na kuungoa.... sasa hivi eneo lina yard....akija mtu kama wewe useme kuna ndugu yetu huku ndani utaeleweka...uliyemuuzia hukuandika eneo lina kaburi uliuza eneo kama eneo...
 
Back
Top Bottom