Mtu amejenga tulipomzika babu yetu. Tufanye nini kupata mwili wa baba yetu tukauzike pengine?

Hapana,Sina haja ya kuuliza... maelezo yake yanajitosheleza mkuu.Kasema huyo aliyenunua na kujenga alikuwepo hata wa kuzika marehemu.Huoni kama hicho ni kiburi?
ngoja tuwekane sawa,ndio alikuwepo wakati wa mazishi ya mzee wao je walimuuzia ili yeye asubirie azikwe hapo,azike ndugu zake au yeye mwenyewe ndio mwenye uamuzi na eneo lake? Hicho sio kiburi ni uamuzi kwa eneo lake
 
Waliweka tu alama, unajua watu wa vijijini mazishi yao waliowengi haswa miaka ya 96 walikuwa wanafanya kama ulivyosema. ila huyo mnunuzi alishiriki kuzika pale kabla hajapanunua na alikuwa anaishi jirani tu
Ndio hio najua sio vijijini tu hata huku mjini wapo wanaozika hivyo inapelekea watu wasijue km chini kuna mabaki wanapokuja kuzika wakichimba ndio wanakuta mifupa hio chungu kitofali mboni naijua sana hio
 
ngoja tuwekane sawa,ndio alikuwepo wakati wa mazishi ya mzee wao je walimuuzia ili yeye asubirie azikwe hapo,azike ndugu zake au yeye mwenyewe ndio mwenye uamuzi na eneo lake? Hicho sio kiburi ni uamuzi kwa eneo lake
Kununua tu eneo lenye kaburi hicho ni kiburi mkuu
 
ni umiliki wake, sababu aliuziwa na baba mdogo amabe alifanya tu kwa tamaa zake. hata mimi nimeona kuna ugumu ndio maana nikaomba mawazo mbadala
 
Alijua pia kuwa panakaburi....kafanya ubabe tu ....
ubabe kwani kavamia eneo lisilo lake? Zingatia ktk andiko la mwenye mada kaandika kuwa WALIMUOMBA,kuomba kuna mawili kupewa au kunyimwa,wawe wavumilivu
 
Ilitakiwa kabla ya kumuuzia mngeanza kuhamisha makaburi. Mlipomuuzia mlimuuzia eneo na kila kitu kilichomo, including makaburi na huenda yeye kwa imani yake alilinunua hilo eneo baada ya kuvutiwa na uwepo wa makaburi na aina ya watu waliozikwa humo.
Endeleeni kumbembeleza, vinginevyo ana haki ya kuyakunda makaburi yake kwa kujenga nyumba juu yake ili msije mkayachimbua.
 
ubabe kwani kavamia eneo lisilo lake? Zingatia ktk andiko la mwenye mada kaandika kuwa WALIMUOMBA,kuomba kuna mawili kupewa au kunyimwa,wawe wavumilivu
wazee wangu wengine walienda kuzungumza nae ili wachimbe maana wanasema kaburi lipo kwenye chumba kimoja wapo cha ile nyumba yan wanajua kabisa, ila amewakatalia na wao sasa wanataka kwenda mahakamani ili wapate kibali cha kufukua.
 
Nje ya mada

Takwimu zinaonyesha kwamba hapa duniani mpaka leo wameishi watu bilioni 100. Kati ya hao, bilioni 92 walishakufa na wamezikwa kila mahali.

Kifupi ni kwamba, karibu kila sehemu ukichimba chini utakuta mifupa kwahiyo hamna shida kujenga sehemu iliyokua kaburi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…