Kununua Bajaj kwa ajili ya biashara sio mbaya kama mmiliki ataamuwa kuendesha mwenyewe, ikitokea mmiliki ameamuwa kuendesha mwenyewe ndani ya miezi sita mpaka saba pesa ya bajaj imesharudi na kuanza kuingiza faida, chombo chochote cha moto kikiwa kipya unatakiwa ukomae mwenyewe kabla hakijaanza kuomba spea, pengine kwa kumsahihisha mtoa mada bajaj ya millioni kumi kama utaisimamia na kuiendesha mwenyewe kuna faida ya kurudisha pesa ndani ya huo muda niliousema hapo juu, maana kama utakuwa unafanyia kazi katika majiji kwa siku kwa wastani lazima ilale elfu 50,000-60,000 Ths, na katika miji midogo kwa siku 40,000-50,000 tsh haikosekani na hizi hesabu zitatokea kama utaiendesha mwenyewe na sio kumpa mtu mwingine aendeshe.