Mtu anayetoa milion 10 kununua bajaji Ili apewe 20k Kwa siku ni kufanya biashara kichaa

Mtu anayetoa milion 10 kununua bajaji Ili apewe 20k Kwa siku ni kufanya biashara kichaa

Bajaji za mkataba service anafanya dereva , wewe Kila siku pesa Yako inaingia. Faida ipo kwakua mkataba Huwa ni miaka 2. Na bajaji haifi haraka ndomna Kuna bajaji used.

Bajaji ni uwekezaji Mzuri kwa pesa ya kula Kila siku hukwami ila kama plan ni kukukuza mtaji ngumu kutoboa. Pesa yake huja kidogo kidogo lakini zinalipa.
Mwanangu mimi nafanya hiyo kusema ukweli kutunza hela sio rahisi Yan kwa ajili ya kula afu spea utaomba pooh sio poa Yan ni hatari engine inadai Kila mara
 
Ni biashara ya kifala kweli, ila biashara nyingi faida yake ni ndogo pia cha msingi ni mzunguko wa fedha usiende mbali na wewe.
unaijua biashara ya hardware hii ni manyoko usipouza stock kubwa kwa mwezi mmoja tu
Waajiriwa wa serikali tukisikia habari hizi huwa tunajiuliza hao wafanyabiashara wanaotutukana kuhusu kuajiriwa kwetu, huwa wanaingiza faida kiasi gani kwa siku baada ya makato yote?
 
Mleta mada kapata mgao wa urithi sasa anatafuta wazo la biashara kinguvu.
Wazo lake kuu ilikuwa anunue bajaj ila kaja na njia ya kuiponda aone muitikio wa watu.
Ipo hivi, kama utanunua boda boda ama bajaj na ukakomaa nwenyewe faida inakuja kubwa sana na hela inarudi fresh tu.
Kumpa mtu bajaj au bodaboda akuletee hesabu basi jiandae kugawana 50/50 na dereva hata kama hela ya matengenezo madogo madogo ni juu yake.
Wastan wa hesabu ya bajaj ni 60,000 kwa siku. Ukiondoa changamoto ndogo ndogo za rushwa, n.k basi baki yako hapo ni 40,000. Kama ulimpa mtu basi tarajia katika hiyo 40,000 upewe 20,000 ili nae achukue 20,000 yake.
Mtoa mada tembea Mbeya na Songwe yote uzione hizo 10M zilivyojaa barabarani.
 
Tupe hesabu zako basi zinazosibitisha uchizi wake??
20,000x365days= 7,300,000 hiyo ni kwa mwaka mmoja.
Kijana una masihara unahisi hiyo bajaji ita operate siku zote za mwaka 365? Hakuna siku itayoenda marekebisho? Hakuna siku suka ataumwa au emergency yeyote? Bado kuparamiana huko road?

Unapokua na siku nyingi za kuoperate bajaji ili ikuletee faida ndipo na risks ya hasara pia inakua kubwa hivo?

Ni bora hata boda ya milion 3 ukiletewa 10k per day sio mbaya, itachukua muda mfupi kurudisha bei ya kununulia chombo plus costs zozote ulizoingiliwa kufanya chombo kiwe road(insurance, nenda kwa usalama kama zipo etc) kuliko kuwa ba bajaji worth 10000k
 
Mleta mada kapata mgao wa urithi sasa anatafuta wazo la biashara kinguvu.
Wazo lake kuu ilikuwa anunue bajaj ila kaja na njia ya kuiponda aone muitikio wa watu.
Ipo hivi, kama utanunua boda boda ama bajaj na ukakomaa nwenyewe faida inakuja kubwa sana na hela inarudi fresh tu.
Kumpa mtu bajaj au bodaboda akuletee hesabu basi jiandae kugawana 50/50 na dereva hata kama hela ya matengenezo madogo madogo ni juu yake.
Wastan wa hesabu ya bajaj ni 60,000 kwa siku. Ukiondoa changamoto ndogo ndogo za rushwa, n.k basi baki yako hapo ni 40,000. Kama ulimpa mtu basi tarajia katika hiyo 40,000 upewe 20,000 ili nae achukue 20,000 yake.
Mtoa mada tembea Mbeya na Songwe yote uzione hizo 10M zilivyojaa barabarani.
Hao ni machizi mtu mweusi hasa wa kijijini hajawahi kuwa na akili ya utajiri
 
Back
Top Bottom