Mtu anayetoa milion 10 kununua bajaji Ili apewe 20k Kwa siku ni kufanya biashara kichaa

Mtu anayetoa milion 10 kununua bajaji Ili apewe 20k Kwa siku ni kufanya biashara kichaa

Nimefanya hii biashara kusema ukweli ni changamoto ndio maana watu wa nanunua bajaji wa nawapa vijana mkataba wa miezi miezi 24,26 hadi 28 ambayo apromixately watarudisha milion 14 kwa hio miezi kwahyo mwenye chombo atakuwa na faida ya milion 4 Baada ya miaka miwili na hela yake inarudi
Yaani Kuna watu hawana kama zimepungua kichwani hivi unanunua bajaji milion 10 halafu unampa mtu mmoja awe anapiga deiwaka anakuletea 20k Kila siku na risk za kutosha hii ni akili Gani yaani hela za mashamba ya urithi nyumbani kwenu unatarajia hii biashara kichaa ikunufaishe aisee kweli washamba mnaotoka kijijini na pesa za urithi wa mashamba mtaendelea kukumbatia umasikini milele?
 
10m peleka utt au kanunue bond, kwa utt unapata 1.2m Kila mwaka na kwenye bond unapata 1.5m Kila mwaka kwa miaka 20 na baada ya miaka 20 pesa Yako unarudishiwa 10m kamili kama ilivyo.Hapo ni akili ku mkichwa tu risky ndogo faida kidogo,ila ni kwa uhakika kwa miaka 20 unakula 1.5 m Kila mwaka au unakula 1.2m Kila mwaka kwa utt mpaka hapo utakapouza hizo utt zako zote.Iko hivi kuliko kununua Bajaj moja kwa moja,Bora ukanunue bond za 10m then tumia iyo Bond kuchukua mkopo wa Bajaj then faida ya bond utarudisha kwa mkopo wa Bajaj na hesabu ya Bajaj itakulisha.
 
Kuna jamaa yangu aliuza kiwanja kanunua bodaboda mpya mbili kazikodisha zimletee hesabu! Ndani ya miezi mitatu ziko hoi taabani kazipaki!
Ooooh,always nunua kitu kinachopanda thamani sio kinachoshuka,hasa wafanya kazi kwakua huna chakupoteza zaidi ya kuwekeza,ila kuna wazee wa bet hua huwaambii kitu kuna miji TZ ina bajaji kuliko public transport
 
Ukitaka kusaidia mtu wa aina hii, mpe wazo mbadala. Hii m10 ipo hapo ndani afanye nini?

Ni kwamba, Hiyo M10 unakuta mtu anayo anajua ataitapanya kwa haraka anaamua anunue bajaji itapanyike kidogo kidogo, hakuna jipya.

Halafu Biashara nyingi tu ukizichunguza huwa ni kuleta mzunguko tu hakuna faida kubwa.
 
TAHADHARI !


MLETA MADA APUUZWE



Mleta mada unaijua vizuri biashara ya Bajaji au unasimuliwa?,Je umewahi kumiliki,kuendesha ya mtu au kwenu mmewahi miliki bajaji?

Bajaji Kwa siku inalaza si chini ya elfu 40 na hii ukiwa unaendesha mwenyewe siyo kumpa mtu!

Dereva (Deiwaka) anapata faida kubwa zaidi ya mmiliki!
 
Back
Top Bottom