Mtu anayetoa milion 10 kununua bajaji Ili apewe 20k Kwa siku ni kufanya biashara kichaa

Mtu anayetoa milion 10 kununua bajaji Ili apewe 20k Kwa siku ni kufanya biashara kichaa

TAHADHARI !

MLETA MADA APUUZWE

Mleta mada unaijua vizuri biashara ya Bajaji au unasimuliwa?,Je umewahi kumiliki,kuendesha ya mtu au kwenu mmewahi miliki bajaji?

Bajaji Kwa siku inalaza si chini ya elfu 40 na hii ukiwa unaendesha mwenyewe siyo kumpa mtu!

Dereva (Deiwaka) anapata faida kubwa zaidi ya mmiliki!
Sasa kaka hapo chukulia mtu anakaz au biashara nyingine maana yake wengi wanaonunu bajaji hawawez kuifanya ajira kamili yaan waendeshe wenyewe sababu wana kazi au biashara ambayo ndio ilileta hiyo 10m ya kununulia hiyo bajaji

Hawawez kufanya bajaj kama ajira anataka kufanya kama source of incime ya pilo

Sasa tatizo ndio linaanzia hapo
 
Kununua Bajaj kwa ajili ya biashara sio mbaya kama mmiliki ataamuwa kuendesha mwenyewe, ikitokea mmiliki ameamuwa kuendesha mwenyewe ndani ya miezi sita mpaka saba pesa ya bajaj imesharudi na kuanza kuingiza faida, chombo chochote cha moto kikiwa kipya unatakiwa ukomae mwenyewe kabla hakijaanza kuomba spea, pengine kwa kumsahihisha mtoa mada bajaj ya millioni kumi kama utaisimamia na kuiendesha mwenyewe kuna faida ya kurudisha pesa ndani ya huo muda niliousema hapo juu, maana kama utakuwa unafanyia kazi katika majiji kwa siku kwa wastani lazima ilale elfu 50,000-60,000 Ths, na katika miji midogo kwa siku 40,000-50,000 tsh haikosekani na hizi hesabu zitatokea kama utaiendesha mwenyewe na sio kumpa mtu mwingine aendeshe.
Kwa hiyo tuki summarize kutoka kwenye maelezo yako ni kuwa uwekezaji wa biashara ya usafiri wa bajaji haifai kwa wenye kazi au biashara zingine. ni lazima mwekezaji aifanye ajira kamili amejiajiri na sio kuifanya njia ya kipato cha pili
 
Mzee hii tunaita kitunzia fedha, biashara ni imani kama imani zingine
 
10 milion ni mtaji tosha sana kama utaamua kufanya biashara ya vifaa vya pikipiki au bajaj, Hakikisha unaisimamia mwenyewe au kama una kijana basi hakikisha una mmonitor kila siku.

Vitu vya kuzingatia, Tafuta sehemu nzuri ambayo ni karibu na kijiwe cha boda au njia ambayo inatumika mara kwa mara, tafuta fundi mzuri na mwaminifu.

Hakikisha sehemu unayofungua duka kusiwe na utitiri wa washindani wako, na hakikisha bidhaa unazochukua zile ambazo zinatumika kila siku. Kwa mfamo oil,lina,taa,bearing,plug n.k.

Kuna baadhi ya vifaa vya pikipiki faida ni top mfano plug na bearing, plug na bearing unaweza kununua kwa 10k ambapo zinakaa pc 10 na ukauza kwa bei ya 2k per pc ambayo faida unapata 10k ukimaliza.

Pikipiki nyingi za sasa especially Tvs zina changamoto sana ya plug so kama utakaa sehemu nzuri unaweza uza hata box mbili za plug ambazo zitakuingizia 20k as faida hapo nje ya faida ya vifaa vingine.

Kama unataka kuingia kwenye hii biashara nicheck Pm tupeane mawazo mbadala.

Note: Biashara ya duka kuna vifaa kwaajili ya kupendezesha duka na vifaa ambavyo vinatembea kwa mauzo, hakikisha unajaza vifaa vinavyouzika badala ya kupendezesha duka.
 
10m peleka utt au kanunue bond, kwa utt unapata 1.2m Kila mwaka na kwenye bond unapata 1.5m Kila mwaka kwa miaka 20 na baada ya miaka 20 pesa Yako unarudishiwa 10m kamili kama ilivyo.Hapo ni akili ku mkichwa tu risky ndogo faida kidogo,ila ni kwa uhakika kwa miaka 20 unakula 1.5 m Kila mwaka au unakula 1.2m Kila mwaka kwa utt mpaka hapo utakapouza hizo utt zako zote.Iko hivi kuliko kununua Bajaj moja kwa moja,Bora ukanunue bond za 10m then tumia iyo Bond kuchukua mkopo wa Bajaj then faida ya bond utarudisha kwa mkopo wa Bajaj na hesabu ya Bajaj itakulisha.
Siajelewa hapa ebu nieleweshe vizuri backbencher
 
Kununua Bajaj kwa ajili ya biashara sio mbaya kama mmiliki ataamuwa kuendesha mwenyewe, ikitokea mmiliki ameamuwa kuendesha mwenyewe ndani ya miezi sita mpaka saba pesa ya bajaj imesharudi na kuanza kuingiza faida, chombo chochote cha moto kikiwa kipya unatakiwa ukomae mwenyewe kabla hakijaanza kuomba spea, pengine kwa kumsahihisha mtoa mada bajaj ya millioni kumi kama utaisimamia na kuiendesha mwenyewe kuna faida ya kurudisha pesa ndani ya huo muda niliousema hapo juu, maana kama utakuwa unafanyia kazi katika majiji kwa siku kwa wastani lazima ilale elfu 50,000-60,000 Ths, na katika miji midogo kwa siku 40,000-50,000 tsh haikosekani na hizi hesabu zitatokea kama utaiendesha mwenyewe na sio kumpa mtu mwingine aendeshe.
Ngoja nihamie kwenye bajaj sasa
 
Kuna watu mnaongea tu ili kujifurahisha, hamjafikiria kuwa hizo bajaji zinatoa ajira kiasi gani? Wanaouza vifaa vya bajaji wamuuzie nani? Wenye garage na mafundi wapate wapi kazi? Nasisi ambao ni usafiri wetu hatuna uwezo wa kununua magari mmetufikiria? Kwa mantiki hio msifikirie tu kwa upande wa anayenunua bajaji kwani hufaidisha watu wengi. Lakini pia mimi ni shahidi kuna watu zinawajengea hapa mjini. Halafu kwa wale wenye wasiwasi kuwa inaweza kuharibika kabla ya kurudisha hela niwaambie tu kuwa kila biashara ina changamoto zake, na mjue kuwa bajaji inaweza kukaaa miaka 5 bila kuguswa injini.
 
Mzee baba upo sahihi
 
Hii ni biashara ambayo inafanyika wewe ukiwa kwenye shughuli zako nyingine, imagine umenunua mbili that's 40,000/- per day yaani umeachana na kusumbuliwa hela za mchicha na vitunguu nyumbani hausumbuliwi whilst kila anaendelea na shughuli zake nyingine.
Kwahiyo ukiwanazo mbili ni 1,200,000/- kwa mwezi ilhali kila mtu akiendelea na shughuli zake nyingine kama kawaida.
Nyumba ni uwekezaji permanent lakini kama umejenga nyumba ya biashara ambayo utapata kodi ya 1,200,000/- itakuwa imekugarimu uwekezaji wa kiasi gani kuanzia ununuzi wa kiwanja mpaka ujenzi?
Angalizo:Kama una mtaji wa kujengea nyumba ya biashara jenga nyumba lakini kama una mtaji mdogo unaotosha kununua bajaji basi ni bora ununue bajaji.
Yaani uwekeze 20M Ili upate elfu 40 Kwa siku akili Gani hii
 
Tupe hesabu zako basi zinazosibitisha uchizi wake??
20,000x365days= 7,300,000 hiyo ni kwa mwaka mmoja.
Haiwez kuja yote kama ilivyo. Labda uyo mnunuaji aendeshe mwenyewe. Ila kama anampa mtu asitegemee iyo 7M kwa mwaka, coz kuna kupigwa kiswahili, dereva kuna cku haleti hela. Inshort biashara yoyote ya usafirishaji kama ndo unaanza fanya mwenyewe ila sio kumpa mtu.
 
Kwa maoni yangu kumpa mnyoa kiduku(virasta) bajaji ya milion 10 kwa rejesho la 20k per day ni uongo nazani wamiliki wa bajaji wangewaiga MO FINANCE na WATU rejesho per day 25k hadi 30k inategemea na kianzio na bado kuna kianzio ndio kitaamua rejesho lako vijana wanazigombania mno

Hii biashara ina pesa kama utaamua kuingia mwenyewe barabarani pesa utaiona haswaa. Mimi pia natarajia kuingia kwenye hii biashara maana nimeshamaliza process zote na bank ya CRDB bado kukabiziwa chombo changu

Bank wana mikataba mizuri na rejesho nafuu mimi nikipata chombo natakiwa nirejeshe 17k per day na dereva ni mimi mwenyewe kwa sasa nimechukua likizo ya miezi miwili kazini nataka nijaribu upande wa bajaji na pia ninampango wa kuomba miezi miwili tena bila malipo nazani kwa miezi 4 nitapata picha halisi kati ya biashara ya bajaji na kazi ninayofanya kipi ni bora

Tusikatishane tamaa kwa kusema biashara ya bajaji hailipi changamoto zipo kwa kila biashara sema wengi tunapenda umwinyi umenunua bajaji unamkabizi kiduku (virasta) bila kujua changamoto ya biashara kwa undani hapo shida ipo
Mm niko upande wako PIGA KAZI MWENYEWE.
ALL the best
 
Wanakuwa wamepiga mahesabu haya
View attachment 3173288

Kwa siku 500 wanakuwa wamerudisha hela yao. Siku 500 ni sawa na mwaka mmoja na miezi mitano hivi.

Kwa hiyo baada ya kipindi hicho kupita ndio anaanza kuhesabu faida.
Hiyo bajaji haina service wala wala repair and maintenance cost?
 
Ujue

Wewe ni fala sana wewe upo kupondea Ebu toa proposal za biashara kasuku wewe sio kukandia tu kuta Ata biashara ya nyanya huna
We shoga kama umeumia Mimi kusema ukweli piga kimya siitaji machoko hapa unaleta hasira zako za umasikini kwangu
 
Back
Top Bottom