Mtu anayetoa milion 10 kununua bajaji Ili apewe 20k Kwa siku ni kufanya biashara kichaa

Mtu anayetoa milion 10 kununua bajaji Ili apewe 20k Kwa siku ni kufanya biashara kichaa

Yaani Kuna watu akili kama zimepungua kichwani hivi unanunua bajaji milion 10 halafu unampa mtu mmoja awe anapiga deiwaka anakuletea 20k Kila siku na risk za kutosha hii ni akili Gani yaani hela za mashamba ya urithi nyumbani kwenu unatarajia hii biashara kichaa ikunufaishe aisee kweli washamba mnaotoka kijijini na pesa za urithi wa mashamba mtaendelea kukumbatia umasikini milele?
Nini maana yako yani twambie tujifunze kitu
 
Ndio mana nimetoa hoja kwa moderators kwamba hii mada ina lengo au imewekwa kwa lengo la kukejeli biashara hii kwamba wanaofanya biashara hii ni vichaa kama.mleta mada anavyowatukana humu, sasa ndo nawauliza moderators kuna ulazima gani wa kuendelea kua na mada hii hewani ikiendelea kuwakejeli na kuwadharau wanaofanya biashara hii au waliowekeza kwenye biashara hii,

Payge

Active
Hiyo sio biashara ni uchizi
 
Kuna watu mnaongea tu ili kujifurahisha, hamjafikiria kuwa hizo bajaji zinatoa ajira kiasi gani? Wanaouza vifaa vya bajaji wamuuzie nani? Wenye garage na mafundi wapate wapi kazi? Nasisi ambao ni usafiri wetu hatuna uwezo wa kununua magari mmetufikiria? Kwa mantiki hio msifikirie tu kwa upande wa anayenunua bajaji kwani hufaidisha watu wengi. Lakini pia mimi ni shahidi kuna watu zinawajengea hapa mjini. Halafu kwa wale wenye wasiwasi kuwa inaweza kuharibika kabla ya kurudisha hela niwaambie tu kuwa kila biashara ina changamoto zake, na mjue kuwa bajaji inaweza kukaaa miaka 5 bila kuguswa injini.
Hakuna hoja zaidi ya matusi ..kufedhehesha na kukejeli biashara za watu waliowekeza

Ndio mana sioni umuhim wa hii threas kuendelea kuwepo mana hata alieanzisha anawatukana kweli pengine wenye hii investment
 
Kilimo we kisikie tu. Tunatakiwa usiwe mtu wa kukata tamaa.

Nililima maharagwe nikiwa na lengo la la kuvuna gunia 20-25 @ nilitegemea ningeuza Kwa lakin 3. nilipigwa Moja ya chembe chaliii.
Hahahahah, noma sana
 
Haiwez kuja yote kama ilivyo. Labda uyo mnunuaji aendeshe mwenyewe. Ila kama anampa mtu asitegemee iyo 7M kwa mwaka, coz kuna kupigwa kiswahili, dereva kuna cku haleti hela. Inshort biashara yoyote ya usafirishaji kama ndo unaanza fanya mwenyewe ila sio kumpa mtu.
GREAT POINT
 
Hesabu we huoni hapo million 10 na 20k Kwa siku ni mbingu na ardhi halafu biashara yenyewe bajaji
Wewe ulitaka ununue bajaji 10m halafu deiwaka akuletee 5m kwa siku ili utajirike haraka? Acha dharau zako mzee. Biashara ya bajaji ndio inatuweka mjini.
 
Nawashukuru sana ndugu mmenifunza kitu.hakika jf ni chanzo cha maarifa ambayo walimu walionifundisha easingeweza peana madini na mimi kama haya
 
Tupe hesabu zako basi zinazosibitisha uchizi wake??
20,000x365days= 7,300,000 hiyo ni kwa mwaka mmoja.
Sasa na wewe code, 20,000/= per day, Unategemea 20 nzima uweke pembeni kwa mwaka mzima, hivi utaishije! Hutaki kula, hutaki kuvaa n.k! Hata mimi siwezi kufanya upumbavu huo
 
Yaani Kuna watu akili kama zimepungua kichwani hivi unanunua bajaji milion 10 halafu unampa mtu mmoja awe anapiga deiwaka anakuletea 20k Kila siku na risk za kutosha hii ni akili Gani yaani hela za mashamba ya urithi nyumbani kwenu unatarajia hii biashara kichaa ikunufaishe aisee kweli washamba mnaotoka kijijini na pesa za urithi wa mashamba mtaendelea kukumbatia umasikini milele?
Vipi anaenunua bus kama yutong 300m sijui halafu kwa siku analetewa laki 5 ?
 
Ni kweli kabisa ni biashara ya ukichaa na inakufanya ukosane na watu wote labda uendeshe wewe mwenyewe
 
We kaa hapo kwa shemeji,mwishoe aje akupige paipu nawewe, kuna mshkaji iyo milion kumi alienda kusini kununua korosho,alinunua kwa Kg 1300,kaja kuuza kg 4400, kanunua karibia awamu mbili, kapata faida chafu, sasaivi anasubiria ufuta,

We unasema milioni kumi utafanya biashara gani, kuna mshkaji ana meza pale mwenge mtaji kaanzia milioni tu,sasaivi yuko good kimtaji na maendeleo
Huna akili ,fala wewe
 
Tupe hesabu zako basi zinazosibitisha uchizi wake??
20,000x365days= 7,300,000 hiyo ni kwa mwaka mmoja.
Kwaiyo mkuu unawekeza M10 ili upate M7 kwa mwaka..hahaha....Halafu unasahau kitu..iyo M7 unayoipigia hesabu apo ki kama Bajaji itafanya kazi mwaka mzima bila ya kupumzika ata siku moja...kumbuka Kuna hesabu za service na garama zingine za uendeshaji kama Kodi za TRA,Insuarence saivi hadi zimamoto wanawataka mabajaji wawe na mitung ya kuzima moto kwa dharula..kiukweli mleta mada yuko sahihi sana..kuwekeza M10 kwa faid isiyo zid M6 kwa mwaka huo ni uvivu wa kufikilia..
Kuna biashara ambazo ukiingiza hiyo M10 kwa mwaka na ukawa unasimamia iyo biashara kikamilifu ndan ya mwaka unaweza ukatengeneza faida ata ya M15..
 
Back
Top Bottom