Mtu anayeweza kutoa ushauri mzuri kwa Watanzania kuhusu mtindo wa maisha (lifestlye) ni Rais Mstaafu Mzee Ali Mwinyi

Mtu anayeweza kutoa ushauri mzuri kwa Watanzania kuhusu mtindo wa maisha (lifestlye) ni Rais Mstaafu Mzee Ali Mwinyi

Mungu amemjalia maisha marefu mzee wetu huyu, mpaka sasa anaikaribia miaka 100.

Pamoja na kuwa tunasema ni kwa neema na kudra za mwenyezi Mungu lakini nina uhakika kuna mambo huwa anaepuka kuyafanya ama huyafanya kwa kiasi mpaka kuufikia umri huu.

Basi ni muda umefika mzee wetu aulizwe ili atupe mwangaza wa namna yeye anaishi. Atutajie kinagaubaga vitu anavyopendelea kuvifanya, chakula anachopendelea kula, na atuambie ni mambo gani hapendelei kuyafanya.

Badala ya kutegemea mambo ya vitabuni ambayo wakati mwingi huwa hayaendani na uhalisia ni vema tukachota maarifa kutoka kwenye kisima kinachotembea.

Wafuasi wa Prof. Janabi mpo?
Kwa nini awe Mwinyi wakati Tanzania huko vijijini ndani ndani kuna wazee wenye miaka zaidi ya mia tena wanaishi maisha ya kawaida kuliko Mzee Mwinyi ambaye ni mtu tajiri mwenye uwezo na anahudumiwa na serikali, maana yake ni kwamba kama asingekuwa na huo uwezo angekuwaje, tuanze na hao walioko vijijini kwanza.
 
Pamoja na kwamba umeandika kwa kufokafoka, ila umesema sahihi sana. Bora nife wakati nina uwezo wa kwenda chooni mwenyewe kuliko uzee wa utoto. Ni fedheha kama unaona kinachoendelea halafu huwezi kujisaidia mwenyewe.
Ni mateso kwa kweli,kujipa tabu tu na kuwapa tabu wanaokutunza
 
Hivi nyinyi mnafikiri kuishi miaka 100 ndio kufanikiwa? yaani binadamu tuna upeo Mdogo sana wa kujidanganya..
hivi mtu Kama Ali Hassan Mwinyi kwa umri huo alionao ana raha gani? chooni hawezi kwenda mwenyewe,nguo anavishwa,Ni maisha ya tabu tu ya kusumbua watu kukulea
mtu timamu na mwenye kujitambua angependa kufa akiwa bado na nguvu kuliko kuishi maisha ya fedheha na udhalili kisa tu umri mrefu!
Tabu gani hii kutawazwa na uliowazaa na matusi juu,huna nguvu ya kufanya mambo yako Ni kuamliwa tu na kufokewa
Sasa kwann mnahangaika na mahubiri ya janabi?? Kama unataka kuishi maisha mafupi kunywa sumu ufe leo.
 
Sasa kwann mnahangaika na mahubiri ya janabi?? Kama unataka kuishi maisha mafupi kunywa sumu ufe leo.
hizo vurugu Sasa! ntakufa pale siku yangu itakapofika na naomba nisifike katika hatua ambayo ntakuwa Ni kero na mateso kwa walionizunguka !
 
Back
Top Bottom