Mengine ni madeni bro, Kuna siku nipo ofisini sasa Kuna mwamba aliacha simu yake chaji hapo hapo akawa ametoka mara ikaanza kuita na aliweka mlio mkubwa unakera mpaka hata inaharibu attention ya kazi... Ikaita mara ya kwanza, ya pili, ya tatu... Ya nne nkasema acha nipokee nimwambie bwana mwenye simu hayupo amcheki badae... Aisee najuta kupokea hiyo simu.. jamaa alinitukana akasema nimepangwa na mwenye simu nimzuge.. akaniambia basi nilipe Mimi hilo deni maana nina shobo na masiara na deni la watu... Akasema KADI ya bank jamaa ameiacha na mshahara ametoa wote simbanking kabla jamaa hawajachukua Chao.. alifoka mshikaji katukana sana... Saiv simu hata ikiita mara mia.. siwezi kuigusa kama ni kelele Bora kazi nifanyie kwenye vimbweta vya watoto