Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa

Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa

Morning_star

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2018
Posts
6,042
Reaction score
17,320
Nimejaribu kuwaza watu wanaochepuka na wake au waume za watu wanajitambua kweli? Hivi wanajua chemistry iliyojengeka kati ya mtu na mwenza wake? Hata kama wenyewe kwa wenyewe watagombana waache lakini usimvue nguo mke au mme wa mtu. Labda mwenyewe ajifunge kwa maneno yake na kujihakikishia kuwa yuko single, vinginevyo hili neno linakuhusu:

Mithali 6:32-33
[32]Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa;
Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake.
[33]Atapata jeraha na kuvunjiwa heshima;
 
Basi hilo neno la Mungu hapo juu linakuhusu ndo maana likaandikwa kuwaweka kwenye mstari!

Tatizo wanawake wa kileo wanawaza ngono muda wote yaani mambo yamebadilika ,zamani wanaume ndiyo walikuwa wanawaza ngono sana ila sasa imegeuka ,ukiingia mitandao hadi vitoto vya 2000 vimegeuka makungwi....Wanasambaza sumu na hupelekea wanawake wahisi kuna kitu wanakosa na kwenda kujaribu nje.
 
Kwahiyo zinaa ni ruhusa as long as sio mke wa mtu?
 
Na kafanya maamuzi yake binafsi na kidude chake kaamua ampe nan , then wewe ufure kama cobra🙄
Hicho kidude unachokisema si mali yake. Ukishakubali kuingia kwenye mahusiano ya ndoa uke/uume sio mali yako tena!

1 Wakorintho 7:4
[4]Mke hana amri juu ya mwili wake, bali mumewe; vivyo hivyo mume hana amri juu ya mwili wake, bali mkewe.
 
Back
Top Bottom