Mungu siku zote huwa anaandaa watu wa kukuvusha mahala fulani ufike upande wa pili. Iko hivyo yan kubali kataa halaf hawa watu Mungu anaowaletaga huwa hawama mambo mengi.
USHUHUDA
Mwaka 2020 June baada ya kuamua kuacha kaz kutokana na sababu fulani plus majungu ofisni nilipitia msoto mmoja mtakatifu.Hapo nina family. Migogoro ya kifamilia niliijulia hapo baada ya kipato kuyumba. Na sikua nalipwa pesa ya maana,ni shilingi 800k tu uzuri kulikua na vi deal vya hapa na pale ambapo iliniwezesha kujenga nyumba within 3 years tu so mpaka naacha kazi familia haikua kwenye nyumba za kupanga.
Basi siku hiyo tumetoka kugombana sana na yf asubuh akiwa anaenda kazini nikajawa mawazo makali sana. Ile ameondoka home nimebak alone watoto wko shule , GHAFLA simu inaita.
Kuchek ni manzi mmoja hivi tulisoma class 1 o level.
Yeye : mambo?
Mimi: poa niaje xxxx
Yeye: fresh, mbona kama hauko fresh shida nini, kazi zinaendaje?
Mimi: aah hamna tatizo, mambo ya hapa na pale tu ila kwasasa siko kazin miez 6 nilipoteza kazi!.
Yeye: daah sasa mbona hatuwasiliani umekaa kimya hivyo? Basi haina tabu, pole nitakuchek baadae.
Mimi: poa poa, siku njema!
Baada ya kukata simu sikuwaza chochote. Nikaendelea na kuawaza na kuwazua kujitafuta!.
Kesho yake asubuh ananipigia simu mshkaji mmoja hivi, ofcz tunafahamiana japo hatukua na ukaribu, ila wana ukaribu na huyo manzi aliyenipigia simu jana yake!. Hakua na mambo mengi alipopiga simu
Jamaa: oyaa niaje wewee,habar ya miaka??? Sasa nimepigiwa na (akamtaja jina) amenieleza situation yako, fanya kunitumia CV yako halaf kesho utapigiwa simu, ufike makubusho saa 4 asubuh!!
Kwel bwana nikapigiwa simu kesho nikatakiwa kufika makumbusho pale ofis flan, hakukua na mambo mwngi ile naingia , habar zangu na CV ilishanitangulia so kufika pale ilikua ni kujadili tu maelekezo ya kazi, na kusaini contract mshahara kwa mwezi 2.5million, haina interview wala nini!!!!.
Posho nikiwa nje ya Dar 80k per day nalipiwa hotel chakula na usafir...haina kupanda basi, ni kula flight tuu. Kuna time nachukua posho kubwa kuliko mshahara.
MAMBO HAYA NYIE ACHENI TUU!!!
Baada ya kufanya kazi miezi 6 kwa hiyari yangu nikaamua kuacha kazi bila kusukumwa, why?
Kipindi najitafuta tafuta nilikua nishapata wazo la nini nifanye so ile pesa nilikusanya ndani ya miezi 6 (ilikia kama miliion 26 hiv) nika settle madeni yaliyoniandama baada ya kukaa kipindi kirefu bila kazi, nikaboresha nyumba yangu kimtindo na nyingine nikanunua gari kwa ajili ya shughuli ambayo nilipata idea kuifanya.
Nikaanza ujasiriamali nikiwa siingizi hata shilling 0 kwa kwa mwezi na nimeacha kazi ya 2.5M kwa mwezi (sounding crazy) ila tayar ule msoto wa kwamza ulishanifunza kitu kuhusu ajira na msoto so kwakifupi woga wa maisha ulinitoka kabisaaa.
Baada ya mwaka now ,idea yangu ina generate almost 1.8M kwa mwezi and am still struggling...nikaanza kupita tena kwenye msoto mwingine ila huu ni wa kujitakia kwa hiyari maana kwenye biashara hiz mambo hazikwepeki..
BAADA YA HAPA KUNA TUKIO LINGINE LA MTU MWIMGINE TENA KUJITOKEZA KU SUPPORT IDEA YANGU MPAKA SASA TUKO PAMOJA.