Mtu gani alikuja katika maisha yako alikusaidia na kuondoka

Mtu gani alikuja katika maisha yako alikusaidia na kuondoka

Mimi niliwahi kusaidiwa na Mzungu mmoja hivi,ilikuwa hivi nilikuwa naenda kuangalia kiwanja changu kigamboni na kipindi hicho nilikuwa kwenye ajira katika Moja za hotel hapa Dar,nikafika pale tunapokata ticket huyo Mzungu alinisalimia akaniambia dada naomba unisaidie nilipie tickets nivuke hapa halafu alikuwa na mabegi kibao ila alikuwa amechoka halafu si unajua wazungu Huwa na harufu zao mbaya zile Mimi nikamuhurumia nikamsadia na nikamlipia baada ya kumuhoji yaliyomkuta nikamlipia na bajaji akaniambia nimpe namba yangu ya simu hiyo ilikuwa 2009 nikampa ,Sasa katika story za hapa na pale aliniuliza unafanya kazi wapi nikamwambia hotelini na nikamtajia hoteli tukaachana hapo,baada ya mda mrefu Sana alikuja hotelini kwetu akiwa na mkewe na dada yake wakaja Kula breakfast na ilikuwa weekend tunaita brunch basi aliwaambia Kila kitu Kwa hiyo kama aliwaambia ni huyu,Nashukuru Mungu mpaka Sasa maisha ninayoishi Mimi na familia yangu ni kwasababu yake aliniunganisha na dada yake huyo ambaye anaishi Hong Kong na amenifundisha biashara huyo dada na yeye muonganishaji sijamuona mpaka Leo,Dada yake alikuwa anatafuta mtu mwaminifu atakaye mwamini wapige kazi pamoja mpaka Leo nipo napiga kazi na dada yake nimekanyaga ardhi ambazo sikutegemea kufika katika maisha yangu ila Mungu mkubwa Sana.
Ok
 
Mwaka 2017 Nilienda kufanya usaili kwenye NGO moja ivi dodoma, kwenye usaili ule majibu mengi ya uzoefu nilidanganya, ila yule mwanamke aliekua ananihoji alinipenda.
Akanisaidia sana kupata ile kazi, na baada ya kuipata akaniambia najua ulikua unadanganya ila nilipenda ulivojiamini.
Tukawa wote kwa mwezi mzima akinifundisha kazi, na baada ya apo alikaa mwezi mmoja akaumwa sana na akafariki.
Ni kama alikua na mda mfupi kwa ajili yangu.
Na kwa kuniamini kwake, kumenipa uzoefu sana kwenye eneo ili.
Mungu amulaze mahali pema.
 
Hello.

Wana chitcharts ni nani alikuja katika maisha yako ukiwa na uhitaji mkubwa wa jambo alikusaidia kwa asilimia kubwa na Akaenda Hakurudi tena au haukuwahi kuendelea kuwasiliana nae.

Kuna rafiki yangu alinikopesha million 1 nilipotoka kumaliza chuo aisee yule Dada ni wakishua nimesoma nae alinisaidia nikaanza biashara ya viatu mtumba.

Nikawa nikipata faida namrudishia hela kidogokidogo mwanzo kabisa nilipompa laki moja akaniambia usinilipe nimekusamehe,kiukweli sijui yuko wapi maana baada ya kuolewa Tuliamua kupoteza au kuacha kuwasiliana

Ajaondoka, bado yupo, namwona kama malaika.
 
Mwaka 2017 Nilienda kufanya usaili kwenye NGO moja ivi dodoma, kwenye usaili ule majibu mengi ya uzoefu nilidanganya, ila yule mwanamke aliekua ananihoji alinipenda.
Akanisaidia sana kupata ile kazi, na baada ya kuipata akaniambia najua ulikua unadanganya ila nilipenda ulivojiamini.
Tukawa wote kwa mwezi mzima akinifundisha kazi, na baada ya apo alikaa mwezi mmoja akaumwa sana na akafariki.
Ni kama alikua na mda mfupi kwa ajili yangu.
Na kwa kuniamini kwake, kumenipa uzoefu sana kwenye eneo ili.
Mungu amulaze mahali pema.
Mungu amlaze mahali pema peponi!
 
Back
Top Bottom