Mtu gani alikuja katika maisha yako alikusaidia na kuondoka

Ok
 
Mwaka 2017 Nilienda kufanya usaili kwenye NGO moja ivi dodoma, kwenye usaili ule majibu mengi ya uzoefu nilidanganya, ila yule mwanamke aliekua ananihoji alinipenda.
Akanisaidia sana kupata ile kazi, na baada ya kuipata akaniambia najua ulikua unadanganya ila nilipenda ulivojiamini.
Tukawa wote kwa mwezi mzima akinifundisha kazi, na baada ya apo alikaa mwezi mmoja akaumwa sana na akafariki.
Ni kama alikua na mda mfupi kwa ajili yangu.
Na kwa kuniamini kwake, kumenipa uzoefu sana kwenye eneo ili.
Mungu amulaze mahali pema.
 


Ajaondoka, bado yupo, namwona kama malaika.
 
Mungu amlaze mahali pema peponi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…