Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
Kwema Wakuu!
Kuna habari zinazoendelea hapa nchini hasa kanda ya ziwa na huko kanda ya magharibi ya nchi yetu kuhusu Watu waliokufa kuonekana tena , kurudi na juzi kuna mmoja amepiga simu ati kuwatakia ndugu zake mwaka mpya mwema.
Ni jamii ya kijinga inayoamini kuwa mtu akifa tena akazikwa anaweza kufufuka na kurudi tena.
Jamii zilizogizani, familia zenye mambo ya kishirikina na Uchawi, familia zenye elimu duni ndio zinazoweza kuamini na kutokewa na matukio kama hayo ya uongo.
Habari hizo ukizifuatilia kwa umakini utagundua ya kuwa zinafanana kwa namna hii;
1. Marehemu alipata ajali mbaya na uso wake haukuwa rahisi kuutambua,
Kuharibika kwa mwili na uso kwa marehemu wengi hupelekea Watu kuzika mtu asiye sahihi. Na hiyo kupelekea mtu sahihi ambaye hajafa akirudi waseme Amefufuka jambo ambalo sio kwéli.
Ukichukua DNA ya marehemu aliyefariki ambaye bila shaka yupo kaburini kwani alizikwa haziwezi kufanana na ndugu wa marehemu.
Kuhusu zile stori za mtu kufa alafu wakazika kisha kaburi likichimbwa wakakuta Mgomba ni stori za Watu wajinga ambao upeo wao upo chini kabisa katika kufikiri mambo.
Mtu yeyote anayeamini habari hizo lazima awe na sifa zifuatazo;
1. Ametoka familia Maskini sana.
2. Ametoka familia inayoamini ushirikina na uchawi ambao kimsingi hauwezi kufanya kitu kama hicho.
3. Ametoka familia isiyo na elimu na yeye mwenyewe hana elimu.
4. Ametoka familia isiyomjua Mungu isipokuwa miungu na mizimu.
Nawatakia Sabato Njema
Robert Heriel
Taikon WA Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam