Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
Kwema Wakuu!
Unajua hawa Vijana wa sasa hivi ni kama wamewehuka fulani hivi.
Unakuta mtu analalamika Mshahara wake ni mdogo, unajaribu kumsikiliza, unamuuliza unalipwa bei ngani, anakuambia labda laki tatu au laki mbili. Unamuuliza Elimu yako vipi, anakuambia Darasa la Saba au aliachia njiani au aliishia kidato cha nne.
Sawa, unamuuliza, unataka kulipwa kiasi gani. Anakuambia angalau laki saba huko au ikipungua kidogo laki tano. Unabaki kusema iiiiiihsh! Unaweza kumzabua.
Kusoma hakutaka, mshahara mdogo hataki, kajiajiri basi pia hataki. Hivi huko ni kulogwa au nI kitu gani! Hutaki Kulipwa Mshahara mdogo na unajijua haujasoma nenda;
Hukusoma sawa, hutaki Mshahara mdogo sawasawa, kajiajri basi, hutaki kujiajiri, sio sawa, mpuuzi nini?
Vijana Maisha ni yako. Kazi yoyote Ile halali ukiifanya Kwa kuipenda itakuheshimisha.
Nataka kukuambia, kuna wakulima wanapesa kuliko Madaktari na Wanasheria waliosoma. Kuna Wachekeshaji na ma-dancer wanamaisha mazuri kuliko wasomi.
Kazi ni kazi. Utalipwa Mshahara kulingana na thamani yako. Maisha mazuri yatatokana na vipaombele vyako.
Acha nipumzike sasa
Sabato njema.
Robert Heriel,
Taikon wa Fasihi,
Kwa sasa Dar es Salaam.

- Kalime vibarua.
- Kuwa Dalali chapuchapu.
- Kuwa machinga.
- Kuwa mpiga debe, Sarange, piga Pesa.
- Kuwa Mganga WA kienyeji, piga Pesa.
- Kuwa Aposto uuze maji ya upako upige Pesa.
- Kuwa Bodaboda, upige Pesa.
- Kuwa muokota makopo, piga Pesa.
- Kuwa Mwanamuziki, piga Pesa.
- Kuwa mwana Tiktok, mwanamtandao, piga Pesa.
- Kuwa muosha wadadakucha, piga Pesa.
- Kuwa mpiganaji WA masumbwi, piga Pesa.
- Kuwa Mama au Baba ntilie, piga Pesa.
- Kuwa promoter au manager wa wasanii, piga Pesa.
- Kuwa MC wa sherehe, misiba na matukio Mbalimbali, piga Pesa.
- Kuwa feminist au mtetezi wa Wanawake, piga Pesa.
- Kuwa mchora Tattoo, piga Pesa.
- Kuwa Game Trainer, piga Pesa.
- Jifunze kuogelea, kuwa muogeleaji kisha kuwa Mwalimu wa kuogelea, Piga Pesa.
- Jifunze ngumi, Martial arts, kuwa Mwalimu wa Ngumi, piga Pesa.
- Kuwa Dancers, piga Pesa.
- Kuwa mchekeshaji na muongea vioja na vituko, piga Pesa.
- Kuwa Makeup Artist, piga Pesa.
- Kuwa mpambaji wa sherehe na matukio, piga Pesa.
- Jifunze ususi, Suka Watu, piga Pesa.
- Jifunze Ukungwi, piga Pesa.
- Kuwa mwanamazingaombwe, piga Pesa.
- Kuwa chawa, mpambe, Mkandikaji Watu, mpaka Watu mafuta
- Kwa mgongo wa chupa, piga Pesa.
- Kuwa mshonaji nguo, piga Pesa.
- Kuwa models, mwanamitindo, piga Pesa.
- Kuwa Mtunzi wa simulizi, muongoza filamu, mtayarishaji, piga Pesa.
- Kuwa mpiga picha, jifunze kupiga picha hata Kwa simu yako, piga Pesa.
- Kuwa Mwalimu wa wanyama kama Mbwa, farasi, Mwewe, Afu piga Pesa.
- Kuwa kinyozi wa kujitegemea, au nyozi la taifa, piga Pesa.