Mtu kama Albert Msando, kwanini anateuliwa kuongoza watu Wilayani?

OH wakati huu si alikuwa CHADEMA inawezekana baada ya kutoka huko ameadilika
 
Hata background checks hawafanyi?

Mtu kama Msando anapasije background check huyu?
Mkuu hii nchi ni zoa zoa tu,sijui wanaofanya vetting ni watu gani? yaani kiufupi hatujawahi kuwa serious kwenye mambo ya msingi,nadhani uchama unachangia sana kwenye hili tatizo
 

1. Wewe jibu hayo maswali

2. Sehemu mojawapo muhimu katika ajira ni maadili na uadilifu.

Maadili ndiyo hujenga profile ya mtu

Maadili ndio hujenga vigezo vya mtu

Maadili ndio hutofautisha baina ya contenders

Maadili ni sehemu ya sifa za job requirements

Ili upate ajira hususani Kwenye ofisi za umma reference to the background ni muhimu sana

Kama huyajuwi hayo ni ujinga au kutojuwa management na integrity havitofautishwi.
 
Kuna jambo moja labda hujalielewa...

Kila mmoja humu anajua na kuelewa kuwa kila binadamu bila kujali umri, hadhi, cheo au status yake ktk jamii;

βˆšβ€’ Huenda haja kubwa na ndogo

βˆšβ€’ Hufanya ngono halali na zisizo halali

βˆšβ€’ Wengine hata hufanya hata zile ngono kinyume na maumbile...

βˆšβ€’ Lakini kwa kufanyikia sirini huko, hatuwezi kuwa mahakimu kwa mambo yake huyo mtu ayafanyayo sirini yasiyomuathiri mtu mwingine moja kwa moja ambayo ni haki yake mtendaji na ivyo anajuana na Mungu wake aonaye sirini..

βˆšβ€’ Tena sasa mara nyingi kama sio zote, wafanyao huu uchafu ni watu ambao kwa nje unawaona kama watu maana sana na wana hadhi fulani hivi kwa sababu ya nafasi zao kisiasa, kiuchumi, utajiri, fedha nk nk lakini kumbe ni uchafu mtupu...

POINTI NI HII:

Kwamba, haya mambo ya kwenda choo, ngono nk sharti yafanyikie sirini na wala hakuna atakayekuwa na ugomvi na awaye yeyote. Ila ukitoa mambo yako ya sirini hadharani mfano eti unavua na kunya haja kubwa hadharani barabarani au unafanya ngono hadharani, hapo ni haki ya jamii ikung'ong'e na kukuhukumu sawia...!

Moja ya hukumu ni kutoaminiwa kisha kupewa nafasi yoyote ya uongozi ktk jamii maana hutaifundisha jamii hiyo lolote la manufaa zaidi kuwa wakikuona tu watakuwa wanaona uchafu wako toka kwenye nyayo zako hadi utosini. Kama utaongoza watu wenye mtazamo hasi kwako, usitegemee utapata ushirikiano wa dhati kwao unless utumie udikteta..!!

Sasa wewe unapoingiza ishu ya watu "kama wangefungiwa kamera za siri" ili kurekodi yafanyikayo sirini na kila mtu, sijui unakuwa umewaza nini tu..

SHIDA IKO WAPI KATIKA HILI LA ALBERT MSANDO?

Iko hapa...

Kwamba, binadamu aliye timamu na kamili anakamilishwa na uwezo wake wa kutenganisha mambo ya kufanyia sirini na yale ya kuweka wazi kwa manufaa ya wengine...

Hili alilofanya Albert Msando ni la sirini. Amekosa maadili na hastahili kuwa sehemu ya mtu wa mfano wa kuigwa ktk jamii. Linai - spoil jamii na watoto wetu...

Inawezekana alishagundua makosa yake na kutubu na kusamehewa....

Lakini labda kidogo watu tunakuwa hatujui jambo moja muhimu sana la kimaisha na kiroho....

Kuwa, kusamehewa ni hatua moja na wala hiyo haina ugumu wowote kuitenda kwa yeyote aombaye msamaha wa dhati ya moyo...

Lakini madhara (cost effects) ya baadhi ya makosa ya kimaadili kama hili la Msando hukaa muda mrefu sana hadi kufutika. Na kwa kifupi mtu wa namna hii hawezi kuaminiwa tena na jamii na kwa lugha rahisi haishauriwi akapewa nafasi ya uongozi wa kijamii...

Na actually hii ndiyo gharama (cost) moja mbaya sana ya dhambi, kwamba, unasamehewa lakini kumbukumbu (matokeo ya dhambi hiyo) kufutika huwa ni ngumu sana na utaishi na matokeo hayo muda mrefu sana...

Albert Msando kwa tendo hili la kingono ya hadharani, alipaswa kuja kuwa kiongozi wa jamii ktk ngazi yoyote miaka 100 ijayo (kama atakuwapo) baada ya kizazi hiki kilichoona uchafu wake kutoweka na kuja kizazi kingine kipya kabisa kisichomjua....

Kwa sasa tendo lake hili litamwandama popote atakapokuwa na atakalokuwa anafanya....
 

Mkuu umeandika kwa ukali sana. Tatizo Nini. Nakumbuka alishaomba radhi. Ungeweza tu kuunderline maadili. Lakini umekuwa very Personal. Tuambie Kuna Nini Kati yako na wewe. Ukiachana na hayo mengine, nahisi atakuwa Mkuu wa Wilaya mzuri.

NB. Watanzania Sisi wanafiki sana.
 
Hivi Samia anaweza kweli kuiangalia hiyo clip halafu aone ni poa tu?
 
Ana gari zipi za kifahari mkuu? Mtu mwenye uwezo wa kumiliki gari za kifahari angefungua grocery au angekua anakimbizana na mabiashara makubwa 😒😒😒😒😒
Msando hana biashara kubwa??

Labda nikuulize hilo tu
 
I couldn’t have put it any better!!!!

πŸ’―%.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…