Mtu kama Elon Musk anaweza kuamua nani awe Rais wa Marekani

Uchaguzi wa Marekani ni wa kipumbavu sana. Mtu anaweza shinda kura nying sana za wananchi ila akaja kuenguliwa na kikundi cha watu 538 wanaojiita electoral college. Ili uwe mshindi wa urais lazima upate kura 270 za hawa wajumbe wa electoral college hata kama kwenye kura za kawaida ulishinda. Hakuna demokrasia huko
 
Sio kweli
 
Atutengenezee mfumo wa kupiga kura kwa biometrics
 
Marekani rais hachaguliwi kwa kura acheni kudanganga watu
Tupe idadi ya kura alizopata hillary clinton na trump wakati ule
Marekani kuna kakikundi tu cha mabwenyenye 400 sijui miangapi wale hao ndio wanachagua rahisi awe nani na nani asiwe
Kura za wamarekani hazina msaada wowote zaidi ya kiini macho
Leta kura za mwaka 2016 hapa halafu utwambie kura za wamarekani zina msaada gani
Marekani hakuna kura kuna wale wajanja mia ndio wanawaamulia wamarekani zaidi ya 300M nani awe rahisi
Marekani ni madikteta kama madikteta wengine
 
Hata kwenye hiyo electoral college hupitishwi pitishwi kirahisi rahisi na kijanja janja tu.

Lazima ushinde kwa kura zinazotakiwa na hao wahusika.
Sasa wananchi wanapiga kura zanini ikiwa rahisi anapitishwa ama kuchaguliwa na electrol?
Demokrasia iko wapi?
 


Kwanza ujue, Elon Musk ndio living practical real genius aliepo kizazi hiki, so influence yake kisayansi, kiuchumi, kijamii na kisiasa iko juu sana duniani kote sio USA tu..!! Kumbuka aliwaambia UN atawapatia dollar bil 6 free ikiwa watamhakikishia hizo fedha zitamaliza njaa duniani kote, na UN wakatoa plan na Elon aliwapa hizo fedha free kabisa


So, kuhusu Elon Musk kuwa na influence kubwa katika nyanja karibu zote duniani ni sawa kabisa, lakini usisahau kuna Democratic party tycoon and lobbyist George Soros huyo ndio jambazi la kiasiasa na kiuchumi na bilionea for years..!!
 
Kwa mfumo wa marekani hawezi, labda wawe wengi lakin peke yake hatoweza, ni kutokana na mfumo na misingi ya kupata kiongozi ilivyo pande hizo
 
Electro vote ni kura jumuishi . Kila jimbo lina idadi kadhaa ya electro vote. Hizi ni za muhimu kwani zinasadia raisi asichahulie na upande mmoja tu anaokubalika. Mfano kwa tanzania mgombea anaweza chaguliwa na kanda moja na akawa raisi kisa tu hiyo kanda inawakazi wengi.
Kwa Marekani hiyo kanda moja yote inajumuishwa kuwa electro vote kadhaa. Hivyo lazima mgombea apate electro vote nyingine kutoka kanda nyingine ili kuwa na electro vote nyingi kuliko mgombea mwingine.

Ni moja kati ya democrasia bora kabisa. Lazima ukibalike kote.
 
Electoral College haifanyi kazi hivyo, wanaopiga kura za Electoral college ni raia wa kawaida kabisa ambao wengi ni wanachama wa vyama husika. Wakati wa uchaguzi wa rais kila chama huwa kinawasilisha wapiga kura wake wa Electoral college(electors) katika serikali za majimbo na mgombea anayeshinda kwa wingi wa kura katika hilo jimbo electors wa chama chake tu ndio wanapewa mamlaka ya kupiga kura ya Electoral college.
 
Huyu ndio wanamuogopa akisema namsapoti nani awe rais

 
Marekani ina vyama vya kisiasa zaidi ya 30 kama hujui ila viwili ndivyo maarufu zaidi kwa sababu viko katika kila kona ya nchi. Kaa ukijua hivyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…