Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Wanabodi
Japo kwa kawaida usiku ni wakati wa kulala na kupumzika, ila kwa watu ma jobless wakiwemo kada yangu ya watu wa "mishe mishe", moja ya usiku ngumu sana, huwa ni usiku wa Jumapili kuamkia Jumatatu ambayo umeipitisha weekend kwa mazabe mazabe, halafu blue Monday inakuja!, usingizi huwa unakata mapema sana, by saa 9:00 usiku, usingizi umekata, hivyo huna jingine lolote la kufanya zaidi ya kushuka JF, ndipo unakutana na taarifa za Corona, usingizi unakata kabisa unakuwa full awake!, hivyo kushuka na makala hii "Kwa Maslahi ya Taifa".
Hii ni thread ya swali tu linalohusu uzalendo na kutanguliza mbele maslahi ya taifa, nikiuliza, hivi mtu kama huyu ni binadamu mwenzetu au shetani? Anaombeaje ugonjwa wa Corona ufike nchini kwetu Tanzania ili kuikomoa serikali? Mtu kama huyu ni mzima kweli au ni mwendawazimu? Kuiombea nchi yako majanga, sio ni zaidi ya uendawazimu? Huu sio ushetani huu?!
Hivi kweli kuna Watanzania wenzetu wenye akili zao timamu kabisa, kwa vile wao sio CCM hivyo wana chuki ya ajabu na serikali ya Magufuli mpaka kufikia hatua ya kuiombea nchi yetu majanga kwa kuomba janga la ugonjwa wa Corona litue nchini mwetu ili kuikomoa serikali kwa kuona jinsi itakavyo kabiliana nalo?!
Corona ikija, atakayeteseka ni serikali au ni mwana CCM pekee?!
Swali hili ni kufuatia nilikuwa nafuatilia thread fulani humu JF, nikakutana na mchango wa ajabu sana wa mwana jf fulani
Huu sio zaidi ya uendawazimu? huu sio ni ushetani kabisa huu?
Pamoja na vitendo vya kiendawazimu na vya kishetani wapinzani wanavyotendewa na serikali yetu, kweli tumefikia kiwango cha Watanzania wenzetu kukosa utu na kugeuka wanyama kwa kuombea majanga yalikumbe taifa letu eti kwa sababu tuu kuna wendawazimu fulani serikalini wanafanya vitendo vya kiendawazimu na kishetani kwa wapinzani, hivyo sasa kuombea ushetani huu utokee kwa serikali yetu kuadhibiwa na janga la ugonjwa wa Corona? Hivi hii Corona ikiingia, atakayeathirika ni serikali ya CCM au ni Watanzania wote akiwemo mwendawazimu huyu?
Nasisitiza ule wito wangu wa siku zote kwenye hizi makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa", kwenye issues za kitaifa yakiwemo majanga mbalimbali, Watanzania tusimame pamoja kwa uzalendo, umoja, upendo na mshikamano na serikali yetu kwa kutanguliza mbele maslahi ya taifa, regardless political affiliations zetu, sisi Watanzania lets pray and stand as one against Corona.
Mungu tuepushie mbali hili janga la ugonjwa wa Corona.
Mungu Ibariki Tanzania.
Nawatakia Jumatatu Njema
Paskali
Updates.
JF has impact, ukisikia taarifa ya serikali kuhusu mitandao ya kijamii, ujue ni jf.
Rejea
Angalizo kwa Wana JF: Tuwaepuke "Prophets Of The Doom", kauli zao huumba!
Uzalendo wa ajabu wa watanzania, unafurahije wakati nchi yako imepata majanga. Hawa ni ma nunda, ma sadist or what?
Rejea za Mandiko ya The Same Author Kuhusu Janga la Corona

Duh...!. Kweli is this what you wish for your beloved country Mama Tanzania?.Korona ije kwanza ili serikali isipoteze rasimali kupambana na Chadema bora izo nguvu wazitumie kupambana na korona kukosa majanga ya kitaifa kunaifanya nchi kubweteka na viongozi kufanya mambo ya kipumbavu ugonjwa huu uje tuone investment yake.
Huu sio zaidi ya uendawazimu? huu sio ni ushetani kabisa huu?
Pamoja na vitendo vya kiendawazimu na vya kishetani wapinzani wanavyotendewa na serikali yetu, kweli tumefikia kiwango cha Watanzania wenzetu kukosa utu na kugeuka wanyama kwa kuombea majanga yalikumbe taifa letu eti kwa sababu tuu kuna wendawazimu fulani serikalini wanafanya vitendo vya kiendawazimu na kishetani kwa wapinzani, hivyo sasa kuombea ushetani huu utokee kwa serikali yetu kuadhibiwa na janga la ugonjwa wa Corona? Hivi hii Corona ikiingia, atakayeathirika ni serikali ya CCM au ni Watanzania wote akiwemo mwendawazimu huyu?
Nasisitiza ule wito wangu wa siku zote kwenye hizi makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa", kwenye issues za kitaifa yakiwemo majanga mbalimbali, Watanzania tusimame pamoja kwa uzalendo, umoja, upendo na mshikamano na serikali yetu kwa kutanguliza mbele maslahi ya taifa, regardless political affiliations zetu, sisi Watanzania lets pray and stand as one against Corona.
Mungu tuepushie mbali hili janga la ugonjwa wa Corona.
Mungu Ibariki Tanzania.
Nawatakia Jumatatu Njema
Paskali
Updates.
JF has impact, ukisikia taarifa ya serikali kuhusu mitandao ya kijamii, ujue ni jf.
Rejea
Angalizo kwa Wana JF: Tuwaepuke "Prophets Of The Doom", kauli zao huumba!
Uzalendo wa ajabu wa watanzania, unafurahije wakati nchi yako imepata majanga. Hawa ni ma nunda, ma sadist or what?
Rejea za Mandiko ya The Same Author Kuhusu Janga la Corona
- Mtu kama huyu ni binadamu au shetani? Anaombeaje Corona ifike Tanzania. Kuiombea nchi yako majanga, sio zaidi ya uendawazimu? Huu sio ushetani? - JamiiForums
- Corona: Japo ni janga, pia ni fursa. Tanzania bado hakuna maambukizi, tupunguze panic, tuongeze Elimu. WB kumwaga mihela, tuchangamkie fursa - JamiiForums
- Corona inatufundisha Tanzania tuna tatizo kuchanganya siasa na professionalism. Hongera Prof. Janabi kwa elimu uliyotoa, so far you are the best! - JamiiForums
- RC Makonda, Dar ni jiji la wote, vyama vyote. Mbowe sio mwanasiasa uchwara aliyefilisika, Zitto sio mshirikina. Tunakupenda, heshimu wote uheshimiwe - JamiiForums
- Je, ni kweli kuna Waziri anaugua Corona inafanywa Siri? Tunaficha nini? Hala hala kisa cha mficha maradhi! Truth & Transparency the only way out! - JamiiForums
- Star TV: Msemaji Mkuu wa Serekali, Dr. Hassan Abbas, azungumzia wajibu wa vyombo vya habari kuripoti janga la Corona - JamiiForums
- Ama kweli nabii hakubaliki nyumbani!. Je Magufuli ni nabii? Tanzania wanambeza, Afrika wanamlilia! Tanzania yapigiwa mfano Magufuli awe Rais wa Afrika - JamiiForums
- Vita Janga la Corona: Msemaji Mkuu wa Serikali, Dr. Hassan Abbas, Naibu Waziri wa Afya, Dr. Faustine Ndungulile, kesho watakuwa live JLNH-Star TV - JamiiForums
- Star TV: Msemaji Mkuu wa Serikali, Dr. Hassan Abbas na Naibu Wazuri wa Afya Dr. Faustine Ndungulile, Wanazungumzia Corona - JamiiForums
- Mungu ni Omnipresent. Kufuatia Local Transmission ya Corona. Je, Sasa Tushinikize Watu Wasalie Majumbani Mwao, ila Sadaka Ndio Itumwe Kwa M-Pesa? - JamiiForums
- Nabii Malisa: Mungu ameniambia Corona ni April tu, May hakuna Corona na hakuna atakayekufa!. - JamiiForums
- Kwa Kasi Sasa, Jee Tuendelee Ushujaa wa Ka-Corona, Tusitishane, Tuchape Kazi Tukiteketea, Au Sasa Tubadili Msimamo Tusitisishe Mikusanyiko Tuokoke? - JamiiForums
- TBC - Mjadala wa Role of The Media kwenye mapambano ya Corona, Je, Media Inatimiza Wajibu Wake Ipasavyo? - JamiiForums
- Live on Star TV: Corona Kushika Kasi Ndio Habari Kubwa Tanzania, Jee Media ya Tanzania, Inatimiza Wajibu Wake Ipasavyo? - JamiiForums
- Corona: Tusinyoosheane vidole. Kama unaweza kusaidia, please do. Usisubiri uombwe - jitokeze saidia, vinginevyo nyamaza! - JamiiForums