UHURU JR
JF-Expert Member
- Jul 24, 2014
- 16,543
- 7,880
Tatizo la watu wamejipa hisia kinyume na uhalisia,yani humu mitandaoni jinsi mtu anavyoelezea maisha ya Tz ni kana kwamba hapakaliki kiasi kwamba imefikia mtu kuwa hana cha kupoteza ameshakata tamaa kabisa na ndiyo maana haoni cha kupoteza hata ikija vita,ugaidi au mlipuko wotewote tu wa maradhi. Ila sasa mtu huyo huyo aliyekataa tamaa kiasi hicho ndiye ambae hata kwenda kwenye maandamano anaogopa virungu vya polisi,sasa hapo utajiuliza huyu mtu aliyekata tamaa ya maisha kiasi haogopi hata vita anaanzaje kuogopa virungu vya polisi wakati maisha anayopitia ni mabaya zaidi ya vita,ugaidi na hata Corona?Mkuu P, huyo jamaa ameeleweka, wewe ndiyo hujamuelewa. Iko hivi, huyu jamaa kaangalia alternatives zote za nini kifanyike kupunguza kero ambayo inaendelea kumkumba. Aidha wafe wao au yeye au sote. Hiki ni kiwango cha juu sana cha hasira inayoambatana na kukata tamaa ya maisha.
This is more than serious, na kimsingi hayuko sahihi na wewe hauko sahihi pia!
Jibu ni kwamba huyu mtu amejipa hisia ambazo hazitoki kwenye uhalisia na ndiyo maana anaishia kupiga kelele mitandaoni tu maana ana vingi vya kupoteza kwenye maisha halisi. Mtu aliyekataa tamaa ya maisha kwa kufanyiwa uonevu anawezaje kutulizwa kwa mkwara tu wa polisi?