Mtu kama huyu ni binadamu au shetani? Anaombeaje Corona ifike Tanzania. Kuiombea nchi yako majanga, sio zaidi ya uendawazimu? Huu sio ushetani?

Huyo mwendawazimu angepita na kiberiti wakati wa utawala huu ingekuwa poa sana,yaani Kuna watu ikitokea nikawakuta kwenye mtaro wamejificha? Lazima niwale kwanza tigo
 
Mtu kama huyu ni binadamu au shetani? Anaombeaje Corona ifike Tanzania. Kuiombea nchi yako majanga, sio zaidi ya uendawazimu? Huu sio ushetani?
Fikiria binadamu moja anamiminiwa risasi Zaidi ya thelathini. Fikiria makumi kwa mamia ya miili ya binadamu inaokotwa kwenye viroba kando ya bahari. Fikiria viongozi waliochaguliwa na wananchi wanatembezwa uchi wa mnyama Segerea. Fikiria...ah, machozi yananitoka!
Mungu tuepushie mbali hili janga la ugonjwa wa Corona. Mungu Ibariki Tanzania.
Mungu tuepushe na vitendo vyote viovu wanavyopitia raia wa nchi hii mikononi mwa watawala awamu hii. Mungu wape mioyo ya unyenyekevu, huruma na upendo viongozi tuliowapa ridhaa na dhamana ya kutuongoza.
Nakutakia Jumatatu NjemaPaskali
Nakutakia usiku mwema Pascal Mayalla
 
Mods kwanini mnafuta comment za wengine huku bila sababu, tena ambayo haijamtukana mtu, kuna mtu alisema mpo corrupt jana nikawatetea,kumbe kweli mpo corrupt, mnaka upendeleo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Iran mbona wamekufa sana tatizo ni nini au hawajapatiwa mafunzo ya dini?

Sent using Jamii Forums mobile app
Ukiona mtu kafa ujuwe siku yake imefiika haijaliehi kafa kwanini.

Waislam tunaamini kifo ni haki yetu nna kifo si kuonewa kwa sababu mwisho (akhera) ni bora kuliko hapa (mwanzo).

Na elewa kuwa si kila anaepata corona anakufa, wengi zaidi wanasalimika kuliko wanaokufa. Isipokuwa elewa kuwa kuuguza na kuzuwia wengi wasiuguwe ni gharama kuliko kuzika.

Hakuna Muislam anaeogopa kifo. Kumbuka hilo.
 
Hivi Aki wish corona ije
Inaweza kuja Tuwekeze ngumu kwenye juhudi za kuelimisha Jamii namna ya kujikinga na kutoa taarifa mapema ili tuweze kucontain. Na heri aliyesema Hivyo kuliko aliyekaa kimya na hujui kadhamiria kufanya nini.....
 
Nadhani huwa unatoka lindo kutoa ripot kwa wasiojulikana.

Wewe kila siku usiku wa manane ndiyo usingizi hukuisha.?

Mashaka ni mengi,ila tunashuru kwa mada zako za uzalendo kwa Tanzania.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Najua P Mayalla una lengo la kuwa expose wengi zaidi. Hujaacha kile ulichomfanyia Kabendera.

Lengo lako ni comments kama hizo zitiririke hapa upeleke file huko.

Una roho mbaya sana, ila watu tu hawakujui.
Amfichue mjinga huyo,hajui hata wafuasi wa Chadema kama yeye watakuemo kwenye janga hilo?

macson
 
Kwa akili yako we tanzania unaona shetani ni yule pekee anaeombea Corona iingie nchini Bali huoni mashetani wanaomwaga na kuteka watu.wanaotesa watu,waminyaji was demokrasia, waombaji waombewe ili waishi zaidi wazidi kuumiza wengine?
Labda wewe paskali una interest nao
Hao ndo wabaya kuliko gonjwa la corona, NI mafirauni na mapaka shume, mapanya buku
 
Sawa kabisa unavyosema Paskali. Nakuunga mkono 100%. Kama ingekuwa gonjwa likiingia nchini litawaandama watumishi wa serikali tu au wana CCM peke yao, hapo ndipo mpinzani angekuwa sahihi kuomba gonjwa lije. Kiukweli ni kwamba ugonjwa ukija labda baba yake mpinzani, au mtoto wake, au bibi yake ndiye atakayekuwa wa kwanza kuupata. Vivyo hivyo nililaumu jana kauli ya Lissu kushinikiza wafadhili waiwekee vikwazo Tanzania. Watakaoumia ni Watanzania wa hali ya chini (wakiwemo ndugu zake Lissu mwenyewe). Nilitoa mfano wa vikwazo vilivyowekewa Zimbabwe kwa takriban miaka 20 kwa visingizio vya kumwadhibu Mugabe. Mzimbabwe wa kawaida ndiye aliyekuwa akiumia wakati Mugabe anapeta tu. Mtu anayeiombea mabaya Tanzania, ananitakia mabaya mimi mtu wa kawaida, na siwezi kumthamini kabisa. Huo ni upinzani uchwara. Hapo juu Paskali ameitwa mbumbumbu na majina mengine kem kem. Ukweli ni kwamba anayemuita hivyo ndiye mbumbumbu mkubwa ambaye amezidiwa hoja na kwa kukosa cha kusema anaishia kutoa matusi tu. Toa hoja itakayonifanya nielewe kwamba ipo sababu ya kuniombea mimi Mtanzania wa kawaida nidhurike kwa magonjwa au nchi yangu kuwekewa vikwazo. Ukifaulu kufanya hivyo ndipo nitakapoacha kukuita wewe mbumbumbu. Heko kwako Paskali. Endelea kutoa elimu ya manufaa kwa Mtanzania wa kawaida. Usifishwe moyo na wapinzani uchwara wanaotutakia mabaya sisi Watanzania wa kawaida.
 
Mbona Al Kaaba imefungwa! Kweli virus wanafanya Al Kaaba ifungwe?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…