Ndagullachrles
JF-Expert Member
- Jun 20, 2023
- 256
- 259
Mtu mmoja anayedaiwa kuwa na tatizo la afya ya akili ,adaiwa kuchoma moto kwa makusundi jengo la zamani la mahakama ya mwanzo mjini Moshi mkoani Kilimanjaro na ,kusababisha uharibifu mkubwa wa jengo pamoja na nyaraka mbali mbali zilzokuwa zimehifadhiwa ndani ya jengo hilo.
Kamanda wa Jeshi la zimamoto na Uokoaji mkoa wa Kilimanjaro Jeremia Mkomangi katika Taarifa yake kwa vyombo vya habari Leo Agost 24,2026 amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Amesema baada ya kikosi chake kupata taarifa za tukio hilo,Askari walifika eneo la tukio walikuta moto ukiendelea kuwaka na jitihada za kuuzima moto huo zilifanikiwa .
"Vyumba vinane vya mahakama ya mwanzo pamoja na nyaraka zake zote na jengo la ustawi wa jamii Moshi vimeungua na chanzo cha tukio hilo ni moto uliowashwa kwa makusudi na mtu anayesadikiwa kuwa na tatizo ya afya ya akili,"Amesema Mkomangi.
Pichani chini ni jengo la mahakama ya mwanzo mjini Moshi likiungua moto