Uchaguzi 2020 Mtu timamu hawezi kushangilia matokeo haya

Uchaguzi 2020 Mtu timamu hawezi kushangilia matokeo haya

Quinine

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
22,227
Reaction score
49,628
Kituo chenye wapiga kura 125,239 (registered voters) msimamizi anatangaza wamepiga kura 437,980, hata wizi hauko hivyo.

Uchaguzi ambao karibu nusu ya wagombea ubunge nchi nzima aidha wametekwa, wanashikiliwa na polisi au kujeruhiwa kwa silaha, utashangiliaje matokeo haya.

Matokeo ya uchaguzi ambao karatasi za kura feki zimezagaa mitaani nchi nzima.

Uchaguzi ambao wakati wa kuhesabu kura polisi wanaingia vituoni wanawatoa mawakala wote wa vyama vingine anabaki wakala wa CCM na msimamizi wa kituo wakihesabu peke yao.

Uchaguzi ambao OCD anaingia kituo cha kupigia kura anakwapua ballot box na kuondoka nalo.

Uchaguzi ambao matokeo yanaonyesha wagombea wote wa ubunge toka CCM wameshinda, matokeo ambayo yanakwenda kuunda bunge la chama kimoja.

Hata mwana CCM mwenye akili timamu hawezi kushangilia matokeo ya uchaguzi huu yanayokwenda kuligawa taifa.
 
Baadaye Ndiyo Tutaelewa Kuwa Tanzania Ni Moja

Uchaguzi Siyo Dhambi, Vyama Vingi Vipo Kwa Mujibu Wa Sheria Ya 1992. Unashangaa Mbona Hawa Wanapokuwa Wanataka Wabaki Wenyewe Kwa Kura Fake Mamlaka Zinatazama
 
Mleta mada si Rais wenu wa mtandaoni aliwambia kuwa atawaingiza barabarani, una lialia nini sasa?

Labda tu nikuulize baada ya Kamanda mkuu kutangazwa kuwa kashindwa mpaka Sasa hivi Makamanda wake mmeshaingia barabara ngapi?
 
Hakika ukiona mtu anasimama na kijivuna juu ya matokeo haya yafaa ajichunguzee, maana kinachofuata hapa ni kilio tu na wakutusemea akuna maana 89% ya hao viongozi watakuwa hawajachaguliwa na wananchi hii ni hatari sana aisee!
 
Hizi kura "Za Nyongeza" sio kote zimeshtukiwa. Na hata Kawe tuseme hicho alichokiona Mdee ni kituo kimoja, what about others?

Karatasi zilizobambwa ni "Genuine" kabisa, ndo kusema kua Tume walichapisha na karatasi za ziada wakawapa CCM.

Tumeingia gharama kubwa kuandaa haya maigizo. Ni heri tukawa hatuna Uchaguzi hizi hela zikaenda kwenye kazi zingine.
 
Mleta mada si Rais wenu wa mtandaoni aliwambia kuwa atawaingiza barabarani, una lialia Nini Sasa

Labda tu nikuulize baada ya Kamanda mkuu kutangazwa kuwa kashindwa mpaka Sasa hivi Makamanda wake mmeshaingia barabara ngapi?
Usiombee hilo na wala usitamani litokee jambo kama hilo hata wewe hutokaa kwa amani.
 
Back
Top Bottom