Kituo chenye wapiga kura 125,239 (registered voters) msimamizi anatangaza wamepiga kura 437,980, hata wizi hauko hivyo.
Uchaguzi ambao karibu nusu ya wagombea ubunge nchi nzima aidha wamekamatwa, wanashikiliwa na polisi au kujeruhiwa kwa silaha, utashangiliaje matokeo haya.
Matokeo ya uchaguzi ambao karatasi za kura feki zimezagaa mitaani nchi nzima.
Uchaguzi ambao wakati wa kuhesabu kura polisi wanaingia vituoni wanawatoa mawakala wote wa vyama vingine anabaki wakala wa CCM na msimamizi wa kituo wakihesabu peke yao.
Uchaguzi ambao OCD anaingia kituo cha kupigia kura anakwapua ballot box na kuondoka nalo.
Hata mwana CCM mwenye akili timamu hawezi kushangilia matokeo ya uchaguzi kama huu unaokwenda kuligawa taifa.