Ukikutana na Simba au Chui ghafla porini, Kama ni Mkristo usali sala ya Baba Yetu...Kama ni Muislam piga kelele ya Allah hu Akbar na Kama ni mpagani chagua nyimbo yoyote ya Diamond au Joto hasira muimbie Simba au Chui labda atakuonea huruma. Kila la kheri huko porini.Wakuu huenda nikaenda kuisha mazingira ya porini na nimekua nikisikia kuhusu wanyama wa kali ni hatari je hatua zipi nichukue kukabiliana na majanga tofouti tofauti nikiwa huko?
Ukikutana na Simba au Chui ghafla porini, Kama ni Mkristo usali sala ya Baba Yetu...Kama ni Muislam piga kelele ya Allah hu Akbar na Kama ni mpagani chagua nyimbo yoyote ya Diamond au Joto hasira muimbie Simba au Chui labda atakuonea huruma. Kila la kheri huko porini.
Mkuu inategemea unaenda pori gani, kwenye miombo kuna mpaka koboko! Kifupi hakuna formula ya kukutana na wanyama wakali porini cha msingi ni kuwa makini tu! Nshagongana nao sana tu, hasa koboko, nyati, simba na tembo kutokana na kazi yangu. Hawana formula wale, omba mungu baada ya muda utawaona wa kawaida sana tu.
Ukikutana na simba ghafla we jitahidi usiogope hata kama anakuja we inama shika magoti muangalie tu haki tena akifika karibu yako hujakimbia anageuza speed kujificha. Ila ukweli inahitaji ujasiri hakina myama muoga kama simba. Simba siku zote hakamati kitu kwa mbele hukamata kwa nyuma, inamaana mpaka ukimbie umpe mgongo ndio anakuwa mjanja. Face to face muoga. Jaribu hata kuangalia video zao utakibaliana na mimi.