Naanza na Chui; Ni mnyama anayependa kujitenga na muda mwingi anapenda kupumzika juu ya mti au chini ya vichaka vichaka vizito vizito/ambavyo havipitishi mwanga mpaka ndani. Kutembea kwake ni pale tu anapoenda kutafuta chakura/mawindo na hapendi usumbufu. Unapomuona Chui gafla na yeye hajakuona eye to eye contact we inamisha kichwa chako au angalia sehemu nyingine huku ukiendelea na safari yako. Pale mtakapogonganisha macho chakwanza akili mwake ni kujihami maana anajua umeenda pale kumuwinda yeye na anajua asipokuwa utamuwahi yeye. Chui ana asiri ya ufuatiliaji, akikuona na kama hujamuona anaweza kukufuatilia umbal wa hata 1km bila wewe kutambua kuwa nyuma yako anakufuatilia nia ni kujua huyu mtu ana nia mbaya nami au vip, akijiridhisha kuwa hawezi kupata madhara kutoka kwako anajiachia zake huyo.
Simba; Ni mnyama anayependa kutembea kimagrupu, ukimuona simba mmoja basi jua ndani ya mita 50 kuna simba mwingine au wengine. Mara nyingi hujigawanya pale wanapofanya mawindo maana wakiwa wanawinda hawapendi kukimbia umbari mrefu so wanajigawanya ili kupunguza usumbufu wa kupata windo lao hata kama windo litakimbilia upande flan basi hukuo kunakuwa na mwingine wa kumuinterupt huyo windo. Simba ana aibu sana mbele ya binadamu na ukikutana nae usioneshe uwoga wala kutetemeka wala usigeuke na kumpa kisogo simama mwangalie eye to eye contact mwishowe huyo atapotea zake. Nadhan nimekusaidia kidogo kwa nilichojifunza juu ya hawa wanyama.