Stephen King ,mtu maarufu kwa uandishi wa Vitabu duniani aliwahi kukataliwa Kazi zake Mara nyingi.
Aliwahi kwenda kwa wachapishaji (Publishers) wa Vitabu 30 wakikataa Kazi zake kwamba hazikuwa na ubora .
Hali hii ilimfanya aanze kukata tamaa na mafanikio.
Akiwa katika hali ya kukata tamaa aliambiwa neno kubwa na mke wake " *Mume wangu ,tusikate tamaa tuendelee kutafuta wachapishaji wengi ipo Siku tutafanikiwa tu* "
Kutokana na hilo neno la mke wake lililomtia nguvu na ujasiri aliendelea kutafuta hatimaye akapata.
Stephen King ameandika vitabu 58 na stori fupi zaidi ya 200 .
Stephen King ameshauza nakala za vitabu milioni 350 duniani mpaka sasa .
Tafiti zinaonesha kwamba Stephen King ni tajiri wa 5 katika waandishi wa vitabu duniani mwaka 2019 , akiwa na dolla million 400.
Hakika hakuna safari isiyo na changamoto katika maisha isipokuwa lazima uangalie aina ya mtu unayesafiri naye.
Mke wa Stephen King alimwambia mume wake hivi akafanikiwa
[emoji1377]
*Mume wangu ,tusikate tamaa tuendelee kutafuta wachapishaji wengi ipo siku tutafanikiwa tu*
Je, mke wako anakwambiaje unapokwama , mume wako anakwambiaje ukikwama ? Ndugu, jamaa na rafiki zako wanakwambiaje ukikwama?
Hakikisha unasafiri na mtu anayeona matatizo kwa jicho la mafanikio.
*You're the Sperm that won the race*
#Nanauka