Mtu wako wa karibu anakwambia nini katika hatua kama hii?

"mgawanyo wa majukumu" hii line unaipenda sana ila jinsi unayoitafsiri huwa napatwa na bumbuwazi.
Kwani mimi naitafsiri vipi na wewe unaitafsiri vipi? Hebu naomba nifafanulie.
 
kwanini na wewe usichukue uamuzi sahihi mapema pale unapoona unanyanyasika sababu ya hela zake na badala yake unakaa unavumulia manyanyaso weweeee, halafu siku akiingia matatizoni ndio unaona ni wakati wako wa ku retaliate unavyojua wewe?
Uamuzi upi sasa hebu nisaidie? Siwezi kuchukua uamuzi wowote kwa sababu kwa wakati huo anakuwa hana matatizo hivyo anakuwa hahitaji msaada wangu ila namsubiri siku akipata matatizo na kuhitaji msaada wangu ndipo nitamuomba aende kwa huo mchepuko wake ukampe msaada

Kwani alipokuwa anachepuka hakujua kwamba ipo siku na yeye atapata matatizo na kuhitaji msaada wangu? Yaani wanaume bwana mnatakaga sisi ndo tuwaze kwamba kwenye maisha kuna kupanda na kushuka ila ninyi hamtaki kuwaza kwamba kwenye maisha kuna kupanda na kushuka see you emphasize on actions which you, yourselves can not implement. Why?
 
Hakuna mwanamke anayefurukuta mbele ya mwanaume mwenye sifa hizo ulizozielezea labda awe karogwa ila sasa ndo ujiulize ni wanaume wangapi wenye sifa hizo ulizozielezea? Ukishapata jibu ndo utajua kwanini wanawake wengi wa sasa wapo hivi walivyo

Mimi nadhani vitu vingine msitulaumu sana wanawake ila mjichunguze kauli na tabia zenu hasa wanaume wa siku hizi yaani siku hizi hakuna mapenzi tena ni tamaa na utapeli tu kwa kwenda mbele na haya mambo walianzisha wanaume sasa kwanini na wanawake waendelee kukubali kuwa victims wa haya maovu kila siku?
 
Tangu mwanzo nilikwambia kuwa usipende sana kujihesabia haki na kuwaona wanaume kuwa ndio chanzo cha matatizo. Unaposema wanaume wa siku hizi unatakiwa kukumbuka pia Kuna wanawake wa siku hizi, sijui kama unajua hilo?
Mwanaume anapokutana na mwanamke wa siku hizi, hatakubali heshima yake kama mwanaume ipotee lazima atatafuta namna ya kumuadabisha huyo mwanamke ili kurudisha heshima yake.
Na mwanamke akikutana na mwanaume wa siku hizi kama mwenyewe unavyowaita basi lazima atateseka hata kama tabia yake ni nzuri.
Lakini pia wanaume bado na wanawake wanaoa jitambua wapo wengi tu ndio maana wakati wengine wakilalamika kuna wengine huku mitaani wazeeka pamoja sasa na ndoa zao.
Narudia tena,mwanaume atambue majukumu yake, na mwanamke pia akubali kuongozeka asiwe mshindani hapo watafika mbali.
 
Sawa nimekuelewa!
 
Inategemea na wewe huwa unanicomfort vipi mda nikiwa na shida
Kama dry na mi ntakosa pozi
Kama mwema napata moyo
 
Hapana siombi hata kubadilika na the way nilivyo na ninavoishi najiona nina amani siwez kua mwengine kwa kweli na unavoniona hivi ni mama yangu mtupu
Kweli, heko zake mama...Kimsingi amezaa mtu kweli kweli. Najiskia raha napoona hekima zako kupitia comment unazotoa humu. Wapo watakaojifunza kupitia wewe naiman.
 
et "mpo" ... nyie wanawake wa jamiiforum ambao kila muda tunawasoma humu na mentality zenu za ovyoo sijui mambo yakienda mrama ndani ya familia mume ndio chanzo!! kuwa na aibu hata kama tunatumia fake ids
Mkuu umewahi kumsoma mara ngapi huyu bibie Madame S ??? Believe me humu kuna wanawake wako njema sana sana sana!
 
Mkuu ni kweli hayo yapo ila si kwa wote. Tuepuke ku-generalize vitu kwa kweli. Wapo wanawake very smart in here ndugu yangu
 
Sasa hata kwa sisi wanawake tukipata wanaume waaminifu na wapole tunaanzaje kuwa wajeuri na wakorofi?
Mmh, kama kuna wanaume wanalizwa basi ni aina ya Ben Pol. Mwanamke wa kibongo akipata mtu mpole kama Ben anaanza vituko vya abuja yani. Mara ajiskilizie mara kiburi kiburi ilimradi tu kero. Mwishowe huwa wanasaliti penzi maana ukiwa mpole mwenye mapenz mwanamke wa kiswahili anakuona kama Zoba tu au zezeta. Wengi hawanaga tabia ya ku appreciate upendo.

Utashangaa lime kucheat tu linaenda kugongwa na mchizi mbabe babe asiejali ila hapo ndio ataganda kama saruji ya mlima Klimanjaro. Kisha kilio kinaanza yani mwanaume hana care kabisa, sijui blah blah.
 
Hivi watu mnaishije kwenye hizo ndoa?? Sioni sababu ya kuoa aseee kama ndio mambo yapogo hivo, sijaona mahali wala kusoma mahali watu wanafurahia ndooaa sanaaaa ni mitifuano tuu

Hapana aisee, ngoja kwanza, nisije nikadandia train kwa mbele
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…