Asante kwa ufafanuzi yakinifu binadada, Nimeelewa sana hasa hapo kwenye kuvuna na kupanda we are all guilty of that at some points in life.
Kwanza kabisa ifahamike kokosea/kukengeuka ndani ya mahusiano inaweza kutokea kwa mtu yeyote yule iwe ni KE au ME, na ninavyoamini mimi na hata wahenga wanasema katika mahusiano/ndoa kila mmoja ni mlinzi wa mwenzake kwa mantiki ya kwamba linapotokea tatizo lolote ambalo chanzo ni mmoja wenu basi wewe ambaye umeona ni tatizo ndio unabeba jukumu la kuhakikisha kuwa tatizo hilo halikui na linaondoka mara moja kwa namna yoyote ile inavyowezekana. Ndio maana huwa tunapokabidhiwa kutoka kwa wazazi tunaambiwa kabisa mbali na kuwa mke/mume lakini huyu pia ni mwanao hivyo mlee.
Changamoto inakuja kwenye kuishi mitazamo/busara tulizoonesha kuzipokea kutoka kwa wazee kama nilivyoelezea hapo juu, je ni wangapi tuna ule moyo/juhudi za` ku deal na wenza wetu pale wanaponesha mabadiliko yasiofaa pasipo kukata tamaa haraka hili kumrudisha kwenye mstari mnyoofu?.. unamuona mwanaume mlevi, sio muaminifu, asiyejari familia na mgomvi umefanya nini hili kumfanya aachane na tabia hizo za ajabu? umekaa nae chini kwa njia ya mazungumzo imeshindikana sasa je, umejaribu kuwashirikisha mashee/wachungaji? wanafamilia au ndugu na jamaa? je umefanya hayo yote na kwa muda gani kama kweli una nia ya kumsaidia mwenza haondokane na tabia mbovu isiyokupendeza? Hii sio kwa mwanamke tu hata kwa mwanume pia(japo kwa mwanaume akipitia hizi njia zote ataonekana ni dhaifu mno).
Ni ukweli ulio wazi tulio wengi hasa kwa kiizazi cha sasa hatuweki efforts kubwa kiasi hicho kwa ajili ya kunusuru mahusiano pale mambo yanapokuwa sio mazuri na hasa ukizangati wewe huna kosa lolote liliofanya mwenzako kafanye madudu. Na hatuoni sababu ya kutumia efforts zote hizo sababu mahusiano tunayachukulia kirahisi rahisi sana na hivyo kutoa mwanya wa tatizo kuwa kubwa zaidi na kadri linavyozidi kuwa kubwa linaleta emotional separation, na kukishatokea tu mtengano wa kihisia chuki/mimba ya uchung lazima iwepo na uchungu/chuki ni mzigo unaokaa kifuani kwa muda mrefu mpaka pale utakapata mahala sahihi pakuutelea, na mahala sahihi penyewe ndio kama hapo yule mbwana anapoingia matatizoni na wewe ndio mtu uliyenaye karibu basi utamuoinesha visanga vya kila namna hili kumfanya ajutie yale yote aliyokuwa anayafanya na kukupa mateso uliyojitahidi kuyavumilia.
Kikubwa ninachokiona mimi kama mwanamke/mwanaume anaona mwenzake ameshapotea kiasi kwamba kwenye ubinadamu hayumo tena, kuliko kuanza kumsubiria huku unamuombea sala mbaya aingie matatizoni hili uyatumie matatizo yake kupata relief ni mara mia ukamuacha mara moja kabla hata hizo sala zako mbaya hazijajibiwa, zaidi ya hapo basi mvumilie na umfariji wakati wa matatizo. Maana hata kama ukishatimiza unachokusudia(kulipiza), baada ya matatizo kuisha kuna uwezekano mkubwa sana akarudi kwenye ile hali yake ya mwanzo ambayo ilikukosesha raha na amani na tena safari hii anaweza kuwa pasua kichwa zaidi sababu hata yeye atakuwa na uchungu uliotokana na namna ulivyokuwa una misbehave wakati yuko kwenye crisis.
Halafu hili suala la kuchepuka...... kuchepuka..... kuchepuka..... kuchepuka...!mbona mnapenda kuligusia sana? vipi mnatuonea wivu nini? the mother nature favors us a lot in this(kidding).