Mkuu wa mkoa wa Arusha, Paul Christian Makonda amekutana na kuzungumza na Kiongozi Mkuu wa Kanisa la Inuka Uangaze, Boniface Mwamposa ofisini kwake, jijini Arusha
View attachment 2962309
Mwamposa aliyeambatana na viongozi wengine wa Kanisa hilo wamempongeza Makonda kwa kuendelea kuaminika na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan na kumtaka kuendelea kuwatumikia wananchi kwa nguvu na jitihada zake zote
Aidha, Mwamposa sambamba na watumishi wenzake wa Mungu walimuombea baraka Mkuu wa mkoa huyo sambamba na kumuomba Mwenyezi Mungu aendelee kumpa utashi, afya njema na nguvu za kuwatumikia wananchi wa mkoa huo
View attachment 2962315
Makonda leo, Jumamosi Aprili 13.2024 anafanya kikao cha ndani na Wakuu wa taasisi, Wakurugenzi na wakuu wa idara mbalimbali pamoja na kusikiliza kero za wadau mbalimbali ikiwemo wa sekta ya maliasili na utalii.
Pia soma:
Makonda amtumia Mwamposa kupata umaarufu kwa kisingizio cha Salamu za Rais Samia , ni mbinu duni sana