Mtume Muhammad: Jamii isipotoshwe; Jua huzama katika Chemchemu ya matope Meusi na Mazito

Mtume Muhammad: Jamii isipotoshwe; Jua huzama katika Chemchemu ya matope Meusi na Mazito

Status
Not open for further replies.

SANCTUS ANACLETUS

JF-Expert Member
Joined
Mar 5, 2016
Posts
3,338
Reaction score
4,676
Wanajukwaa:

Dunia yetu inaendelea kushika kasi katika suala la Sayansi na Tekinolojia.Kwa siku za hivi karibuni,wanasayansi wamegundua kuweza kutengeneza Moyo kwa kutumia stem cells,ikiwa ni hatua katika kuelekea kutengeneza moyo wa binadamu,hali ambayo itasaidia katika kukabiliana na matatizo ya Moyo yanayowakabili wanadamu,kwa kiasi kikubwa, yale ambayo uhusisha mwanadamu kupoteza maisha, kwa sababu tu Moyo wa mgonjwa husika hauna repair au hauwezi kubadilishwa.Miaka kama kumi hivi iliyopita,wanasayansi walikuwa wamefanikiwa kutengeneza Moyo wa panya kwa kutumia hizo stem cells.

Kumbe,kwa tafiti mbalimbali zinazoendelea kufanyika sehemu mbalimbali duniani,ama ardhini au angani,zote zinalenga katika kuboresha maisha ya mwanadamu na hata kuongeza siku za kuishi kwake.Historia inao watu wengi sana ambao wamejihusisha na Sayansi kwa nyakati tofuati tofauti.

Leo,ninataka tumuangalie Mtume Muhammad kwa namna alivyoweza kujihusisha na suala la Sayansi kwa kile kinachosemwa ni kwa msaada wa Mungu.Kurani neno la Mungu;maneno ambayo Mungu akiisha kuyaandika huko Mbinguni, alikuwa anampatia Malaika Gabriel na malaika Gabriel akampatia Mtume Muhammad katika Nyakati tofauti tofauti na Muhammad kuyaweka katika maandishi,lakini kwa namna ya pekee,kwa mara ya kwanza kabisa ikiwa ni katika Pango lililoko katika Mlima Hira, Jabal an-Nour,huko Makka,ambako inadaiwa Mtume Muhammad alipokea ufunuo huo, kwa matatizo sana kwa sababu ya kutojua kwake kusoma na kuandika,Malaika Gabrieli alijikuta anamkaba.

Kwa njia ya ufunuo wa Kurani,tunafunuliwa mambo mengi ya Kisayansi ambamo Muhammad anatujuza jinsi mambo yalivyo.Kwa leo, ninawaletea jambo moja tu.Nalo ni juu ya namna Jua linavyokuchwa na kadri Mungu atakavyotujalia tutayaangazia na mambo mengine.


Kurani kupitia Sura al-Kahf (18: 83-86), inaeleza kwamba Jua huchwea katika chemchemu ya matope meusi mazito(dark Muddy spring):

“83-Na wanakuuliza khabari za Dhul- Qarnaini. Waambie: Nitakusimulieni baadhi ya hadithi yake.84 -Sisi tulimtilia nguvu katika ardhi na tukampa njia za kila kitu.85 - Basi akaifuata njia. 86 - Hata alipo fika machwea-jua aliliona linatua katika chemchem yenye matope meusi. Na hapo akawakuta watu. Tukasema: Ewe Dhul-Qarnaini! Ama uwaadhibu au watwae kwa wema.”

Wakati Muhammad akiwa ametupasha ukweli huo ambao aliandikiwa na Mungu, Ukweli wa kisayansi umebainisha kwamba Jua ni kubwa zaidi na lenye joto kali kuliko dunia.Na ikitokea kwamba Dunia inakaribiana na Jua,basi dunia itayeyuka kutokana na joto kubwa la Jua.

Ukweli mwingine,ambao pia Sayansi imetupatia ni kwamba Jua halitembei bali sayari mbalimbali ndio hulizunguka,ikiwemo Sayari yetu ya Dunia. Historia inaonyesha kwamba mtu wa kwanza kugusagusa habari za kuwa Jua lilikuwa halizunguki alikuwa ni Aristarchus (310-230KK).

Aristarchus alikuwa ni mwana-Astronomia wa Kigriki.
Yeye aliamini dunia ilikuwa katikati ya Mfumo wa Jua(Solar system) na sayari zingine (ikijumuishwa na nyota ambazo zilikuwa zimefungwa katika nafasi fulani) ndio zilizokuwa zikilizunguka Jua.

Hata hivyo, baadaye mwanasayansi,Aristarchus, alikuja kugundua kuwa sio dunia iliyokuwa katikati ya Mfumo wa Jua, bali ni Jua na hivi kwamba ni Dunia na sayari zingine ndizo zilikuwa zikilizunguka Jua.Ugunduzi wa namna hii ulipatikana miaka mingi sana (takribani karne tatu hivi) kabla hata ya Yesu Kristu kuzaliwa na karne tisa kabla ya Muhammad kuzaliwa.

Mwanasayansi mwingine pia aliyekuja na mtizamo tofuati na wa Muhammad (kwa kadri ya ufunuo kutoka kwa Mungu) ni Jean Buridan (1300-1359/61). Huyu) anafahamika kama Mwanafalsafa Mashuhuri sana katika Ufaransa.Buridan alikuwa Mwalimu katika Kitivo cha Sanaa cha Chuo Kikuu cha Paris kwa kupindi chote cha maisha yake ya kitaaluma akimakinika hasa hasa katika masuala ya Logiki (Logic) na kazi za mwanafalsafa Aristotle.

Ni Bridan aliyeanzisha wazo juu ya kiitwacho Copernican Revolution katika Ulaya.Hili ni fundisho lililoleta mwangaza kutoka kuamini kwamba dunia ilikuwa imesimama sehemu moja katika ulimwengu na kwamba Jua ndio lilikuwa linaizunguka dunia (Geocentrism) hadi kueleweka kwamba kumbe Jua ndilo limesimama wakati dunia na sayari zingine zikilizunguka (Heliocentrism).

Kumbe, sasa kwa uchache,kwa mawazo ya hao wanasayansi wawili,tunapata picha kwamba Muenendo wa Jua kuchomoza na kutua sio jambo lililoanza wakati wa Muhammad.Na kama suala la Sayansi ya Mfumo wa Jua lilianza mapema kabla ya Yesu na Muhammad kuzaliwa, yeye Muhammad alipopewa ufunuo na Mungu, hakuweza kujiuliza iwapo ufunuo huo wa Mungu inakuwaje unapingana na ukweli wa mambo?Katika kutafakari ufunuo huu wa Mungu kwa Muhammad, nimejikuta nina maswali yafuatayo,ambayo naomba yatuongoze katika kujadili suala hili.Ni muhimu kujadili kwa sababu pengine Dunia inatufundisha vitu ambavyo havipo.Hivi kweli Mungu anaweza kumueleza Muhammad mambo ya uongo?Maswali mengine ambayo bila shaka hata wewe unaweza kujiuliza ni haya:

1. Hiyo Chemchemi ya matope mazito na meusi iko hapa duniani?Na kama haipo hapa duniani iko angani? Na kama iko angani iko sehemu gani?


2. Huyo Dhul-Qarnaini alikuwa ni kiumbe wa namna gani huyo aliyepewa uwezo wa kuona Jua linavyotumbukia katika matope?


3. Pamoja na kwamba wakati wakati wa Muhammad, labda Sayansi ya kwamba Jua halizunguki, isipokuwa dunia ndio hulizunguka Jua, ilikuwa haijafika katika maeneo ya ardhi ya Arabia, bado hata vizazi vya zamani sana havikupata kuwa na uelewa kama huo wa Muhammad kuwa Jua lilikuwa linatua matope meusi! Je,ilikuwaje katika Vizazi vyote hivyo hapo katikati(ikiwemo na Yesu mwenyewe ambaye Muhammad anamuelezea kama aliyekuwa na uwezo wa kufinyanga wanasesere na kuwapulizia uhai na wakawa ndege kamili), kabla ya Muhammad, akakosekana mtu mwenye uelewa wa kuliona Jua likizama katika matope meusi tofauti? Hivi wewe kwa sayansi hii ya Muhamma juu ya Jua kuchwea katika matope meusi haikupelekei kujiuliza yafuatayo:

· Je, Muhammad kusema mambo ambayo hakuwa nayo uthibitisho ilikuwa ni kutafuta tu kuonekana kwamba Mungu amempa ufunuo wa kipekee juu ya ulimwengu?


· Je, vizazi ya Kiarabu na dunia kwa ujumla baada ya kugundua kwa tafiti za kisayansi, ambazo zimethibitisha kuwa Jua huzungukwa na sayari mbalimbali, ikiwemo Sayari yetu ya dunia, vimuoneje, Muhammad na Uislamu kwa ujumla?


· Je,wanadamu wa vizazi vyote vinavyofahamu kuwa Jua halijawahi kuzama katika matope ama meusi,bluu au meupe, visimuamini Muhammad katika mambo mengine aliyoyasema au vimuchukulie kama mtu aliyekuwa anajaribu kupiga ramli ya jinsi mambo yalivyo?

Lakini swali la mwisho kabisa ambalo nitaomba ujiulize ni hili:Je,Ni kwa nini hadi leo baada ya kugundulika kuwa Jua halizami na wala halizunguki,ni kwa nini hadi sasa aya hiyo iko imesalia katika Kurani?Je,ni nani anasema uongo kati ya Mungu na wanasayansi juu ya suala la Jua?

Karibu kwa mjadala ili tupate kujua ukweli kwa faida ya maendeleo ya Dunia yetu.
 
Battle za kiiman/dini zilishaanza kupotea ila siku zikianza yan mpk unajiuliza wamefunguliwa toka wapi kwa mbali naona zkrud, hamna atakayetaka kua nyuma kila yule ataleta Mungu Wa imani yake nakumuelezea
 
Battle za kiiman/dini zilishaanza kupotea ila siku zikianza yan mpk unajiuliza wamefunguliwa toka wapi kwa mbali naona zkrud, hamna atakayetaka kua nyuma kila yule ataleta Mungu Wa imani yake nakumuelezea

Vita iko wapi hapo? Hatujadili dini Bali ukweli Wa Sayansi ya Jua.Lazima kutenganisha Dini na sayansi katika suala hilo.Jua liko kwa faida yetu wanadamu na si kwa faida ya Mungu.Kwa hiyo,tukijifunga kutojadili mambo yanayotuhusu, tunaokuwa tunaumia ni sisi na wala sio Mungu.
 
lengo lako si mashndano ila kuna watakaotumia uzi huu kimashndano, yan ile tu mtu asionekane yupo nyuma....

Watu wa namna hiyo tutawaelimisha tu kwamba wasivuruge mjadala huu.
Hatuwezi kuacha kujadili suala muhimu kama hilo la Jua kuchwea katika matope meusi katika Sayari yetu.

Ni muhimu tufahamu ukweli huo maana kama ni kweli Jua linachwea katika matope na tena katika nchi yoyote hapa duniani, kuna siku tunaweza kuja kudhurika kutokana na Joto jingi ambalo Jua linalo.

Ni muhimu tufahamu hiyo Chemchemu ya matope meusi iko nchi gani katika Dunia hii na nini hasa kinaifanya hiyo sehemu inakuwa ya matope meusi?

Ni muhimu tufahamu ni kwa nini wanasayansi wametupotosha kwa muda mrefu namna hiyo kwamba Jua halizunguki?
 
'Ingekua ruhusa yangu mijadala ya kidini ingeishia makanisani na misikitini tuu.
Ndio maana sio ruhusa yako!...hii tabia ya kuogopa kufungua akili kwa minajiri ya kupata maarifa mapya ni upuuzi.

Sijaona mjadala wa kidini. Nalitamani maustadhi na mapadri kila mmoja kwa nafsi yake na elimu ya dini aliyoipata kuja kukanusha hiki mleta uzi alichokisema.

Kama kuna uongo urekebishwe, kama ni kweli basi tujieleimishe kwa minajiri ya ukuzi wetu wa maarifa!
 
'Ingekua ruhusa yangu mijadala ya kidini ingeishia makanisani na misikitini tuu.

Hapa tunajadili ukweli wa Kisayansi juu ya Jua na ambao unaihusu jamii ya wanadamu.Au wewe Jua halikuhusu na halina faida kwako? Unapendekeza tukafanye mjadala kama huu huko msikitini au kanisani,kwani Mungu Jua linamsaidia nini?
 
Ndio maana sio ruhusa yako!...hii tabia ya kuogopa kufungua akili kwa minajiri ya kupata maarifa mapya ni upuuzi.

Sijaona mjadala wa kidini. Nalitamani maustadhi na mapadri kila mmoja kwa nafsi yake na elimu ya dini aliyoipata kuja kukanusha hiki mleta uzi alichokisema.

Kama kuna uongo urekebishwe, kama ni kweli basi tujieleimishe kwa minajiri ya ukuzi wetu wa maarifa!

Sawa sawa mkuu.Kuna mambo mengi sana tumeelezwa isivyo.Hili la Jua ni cha mtoto.Kuna masuala nitayaleta kadri ya muda utakavyoturuhusu ambayo tukiyaacha yaendelee kuaminiwa na kufundishwa namna yanavyofundishwa,tutakaokuwa tunapata hasara ni sisi wanadamu na sio Muhammad au Yesu Kristu.
 
Yani hapa ni kukamata BAPA la KONYAGI na kulikata taratibu huku nikiangalia mpambano Nani zaidi kati Yao huku nikibaki katika kile ninachokiamini,maana sitaki kuchimba sana hata mambo nisije jikuta milembe bure kwa kuchanganyikiwa...
 
Kwa kusema "sawa" unamaanisha nini,mkuu? Kwamba Mungu ni Muongo au wanasayansi ndio waongo juu ya Suala la Jua kuchwea katika matope meusi au kwamba Jua halizunguki?
hata uzi sijausoma wote mkuu nimeishia njiani gari ilipata hitilafu kidogo
 
na kule Roma ilikuwa unafungiwa sakramenti au kufukuzwa kabisa kuwa muumini kama ungetamka kuwa "dunia inalizunguka jua" pia wanasayansi wa kanisa waliamini dunia ni kama meza hivi ambapo unaweza kutembea hadi mwisho ambapo kuna "korongo" kubwaa!
Sasa hivi kanisa linapambana na utafiti na majaribio ya stem cell, maana siku akitengezwa binadamu kwenye maabara ndio utakuwa mwisho wa mafundisho ya "dhambi ya asili"

Sijawahi kuiamini hii misahafu na waandishi wake! Japo mimi ni mkatoliki kanisani huwa naenda kama " social activity" na sio kuitafuta mbingu.
 
Tatizo kubwa ni AIBU, waumini wanaona aibu kukiri ukweli kwamba wamedanganywa!

Hata kama wamegundua kwamba Mungu hakuwahi kusema hivyo kwamba Jua linachwea katika matope meusi,ni suala la kukiri tu hadharani na kufuta hiyo aya na kisha maisha yanaendelea.Kwani kuna shida gani kufuta hiyo aya katika Kurani na kubakisha yale yaliyo ya kweli?
 
na kule Roma ilikuwa unafungiwa sakramenti au kufukuzwa kabisa kuwa muumini kama ungetamka kuwa "dunia inalizunguka jua" pia wanasayansi wa kanisa waliamini dunia ni kama meza hivi ambapo unaweza kutembea hadi mwisho ambapo kuna "korongo" kubwaa!
Sasa hivi kanisa linapambana na utafiti na majaribio ya stem cell, maana siku akitengezwa binadamu kwenye maabara ndio utakuwa mwisho wa mafundisho ya "dhambi ya asili"

Sijawahi kuiamini hii misahafu na waandishi wake! Japo mimi ni mkatoliki kanisani huwa naenda kama " social activity" na sio kuitafuta mbingu.
Mkuu huo muda unaopoteza kwenda kanisani bora uende bar.
Unajipotezea muda tu kama huna Imani
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom