Yesu mwenyewe amesema kuwa ametumwa kwa watu wa Israeli tu (Matayo 15:24) "Akajibu, Akasema, Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli.
" Pia Matayo 1:21 "Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana, yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao."
Yesu pia amesema kuwa hakuja kubadilisha ila kukamilisha (Matayo 5:17-18) "Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza. Kwa maana, amin, nawaambia, Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka, hata yote yatimie."
SWALI:
Lakini katika Marko 16:15 Yesu amesema, "Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe."
MAJIBU:
Hilo linapingana na kile kilichotajwa hapo juu katika matayo 15:24 na Matayo 1:21.
Pili, Marko 16:9-20 zimeondoshwa katika Biblia nyingi.
The New American Standard Bible imekiweka kipande hiki katika mabano na ikaweka maelezo yafuatayo:
"Baadhi ya miswada ya kale mno inaondosha kuanzia aya 9 hadi 20."
Biblia ya The New World Translation of the Holy Scriptures inayotumiwa na Mashahidi wa Yehova inakubali kuwa miswada maalumu ya kale inaongeza maelezo marefu au mafupi baada ya Marko 16:8 lakini baadhi ya miswada hiyo inaondosha aya hizo.
Na Biblia ya The Revised Standard version inachapisha chini ya ukurasa rejeo lifuatalo: "Baadhi ya mamlaka za kale zaidi inakileta hicho kitabu cha Marko na kukifunga mwishoni mwa aya ya 8..."
Hili linamaanisha kuwa ufufuo si kweli, kama ulivyoelezwa katika Marko 16:9.
SWALI:
Lakini Yesu amesema katika Matayo 28:19: "Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la
Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu."
MAJIBU
"Mataifa yote" lazima ifafanuliwe kuwa ni yale makabila kumi na mbili ya Israeli, vinginevyo itapingana na Matayo 15:25 na Matayo 1:21.
Katika Biblia ya The New American Standard Bible na ya The New World Translation of the Holy Scriptures, kifungu hicho hakitafsiriwi kuwa, ni "all nations – mataifa yote" lakini kinatafsiriwa "all the nations, - yale mataifa yote," inayomaanisha yale mataifa (makabila) kumi na mbili ya Israeli.
Hata sisi WaKisto Tunafahamu fika pasi na Shaka kwamba Yesu Kristo alikuja kwa ajili ya Waisraeli. Ni kawaida kunukuu Vifungu MBALIMBALI ILI kuthibitisha Hilo
[emoji116] [emoji116]
Yohana 1:11-12
[11]Alikuja kwake, wala walio wake hawakumpokea. [12]BALI WOTE waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, NDIO WALE WALIAMINIO JINA LAKE;
[emoji115] [emoji115]
Zingatia hapo juu anasema "wale waliaminio Jina Lake" tu.
Angali akitaka WaIsraeli kumpokea. Yesu KRISTO alikua na The Biggest Plan ahead ya kueneza Injili Ulimwenguni Kote.
[emoji116][emoji116]
Mathayo 10:18
nanyi mtachukuliwa mbele ya maliwali na WAFALME kwa ajili YANGU, kuwa ushuhuda KWAO NA KWA MATAIFA.
[emoji115] [emoji115]
Huu ujumbe unathibitisha unabii wa Roho mtakatifu kupitia Simeoni kua Yesu ndiye Nuru ya Mataifa yote duniani.
Simeon anena hapa chini[emoji116] [emoji116]
Luka 2:32
Nuru ya kuwa mwangaza wa Mataifa, Na kuwa utukufu wa watu wako Israeli.
Nabii Isaya naye alimtabiria Yesu vivyohivyo..
[emoji116] [emoji116]
Isaya 42:1
[1]Tazama mtumishi wangu nimtegemezaye; mteule wangu, ambaye nafsi yangu imependezwa naye; nimetia ROHO YANGU JUU YAKE; naye atawatolea mataifa hukumu.
Yesu anaTOA unabii kuhusu Injili.
[emoji116] [emoji116]
Mathayo 24:14
Tena HABARI NJEMA YA UFALME ITAHUBIRIWA katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa MATAIFA YOTE; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja.
Marko 13:10
Na SHARTI Injili ihubiriwe kwanza katika mataifa yote.
Yohana 12:46
Mimi nimekuja ili niwe nuru ya ulimwengu, ili kila mtu aniaminiye mimi asikae gizani.
Yohana 3:18
Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini JINA LA MWANA PEKEE WA MUNGU.
Mathayo 21:9
Na makutano waliotangulia, na wale waliofuata, wakapaza sauti, wakisema, Hosana, Mwana wa Daudi; ndiye mbarikiwa, yeye ajaye KWA JINA LA BWANA; Hosana juu mbinguni.
Mathayo 28:18-20
[18]Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani.
[19]Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;
[20]na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.
Bear in mind anapozungumzia Mataifa hazungumzii kua atakomboa na Mashetani ili yamrudie Mungu. Kristo amekuja Kukomboa wanadamu tu, aliewaumba kwa mfano wake na kuwapulizia na Pumzi akafanyika ScapeGoat kwaajili yao.
Yesu Kristo ni Adui Mkuu wa Mashetani na Baba wa Uongo na muuaji yote. Na Jina lake halitakwi na mashetani. Kwakua ni Jina Kuu Sana na Takatifu sana.