Hata sisi WaKisto Tunafahamu fika pasi na Shaka kwamba Yesu Kristo alikuja kwa ajili ya Waisraeli. Ni kawaida kunukuu Vifungu MBALIMBALI ILI kuthibitisha Hilo
[emoji116] [emoji116]
Yohana 1:11-12
[11]Alikuja kwake, wala walio wake hawakumpokea. [12]BALI WOTE waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, NDIO WALE WALIAMINIO JINA LAKE;
[emoji115] [emoji115]
Zingatia hapo juu anasema "wale waliaminio Jina Lake" tu.
Angali akitaka WaIsraeli kumpokea. Yesu KRISTO alikua na The Biggest Plan ahead ya kueneza Injili Ulimwenguni Kote.
[emoji116][emoji116]
Mathayo 10:18
nanyi mtachukuliwa mbele ya maliwali na WAFALME kwa ajili YANGU, kuwa ushuhuda KWAO NA KWA MATAIFA.
[emoji115] [emoji115]
Huu ujumbe unathibitisha unabii wa Roho mtakatifu kupitia Simeoni kua Yesu ndiye Nuru ya Mataifa yote duniani.
Simeon anena hapa chini[emoji116] [emoji116]
Luka 2:32
Nuru ya kuwa mwangaza wa Mataifa, Na kuwa utukufu wa watu wako Israeli.
Nabii Isaya naye alimtabiria Yesu vivyohivyo..
[emoji116] [emoji116]
Isaya 42:1
[1]Tazama mtumishi wangu nimtegemezaye; mteule wangu, ambaye nafsi yangu imependezwa naye; nimetia ROHO YANGU JUU YAKE; naye atawatolea mataifa hukumu.
Yesu anaTOA unabii kuhusu Injili.
[emoji116] [emoji116]
Mathayo 24:14
Tena HABARI NJEMA YA UFALME ITAHUBIRIWA katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa MATAIFA YOTE; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja.
Marko 13:10
Na SHARTI Injili ihubiriwe kwanza katika mataifa yote.
Yohana 12:46
Mimi nimekuja ili niwe nuru ya ulimwengu, ili kila mtu aniaminiye mimi asikae gizani.
Yohana 3:18
Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini JINA LA MWANA PEKEE WA MUNGU.
Mathayo 21:9
Na makutano waliotangulia, na wale waliofuata, wakapaza sauti, wakisema, Hosana, Mwana wa Daudi; ndiye mbarikiwa, yeye ajaye KWA JINA LA BWANA; Hosana juu mbinguni.
Mathayo 28:18-20
[18]Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani.
[19]Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;
[20]na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.
Bear in mind anapozungumzia Mataifa hazungumzii kua atakomboa na Mashetani ili yamrudie Mungu. Kristo amekuja Kukomboa wanadamu tu, aliewaumba kwa mfano wake na kuwapulizia na Pumzi akafanyika ScapeGoat kwaajili yao.
Yesu Kristo ni Adui Mkuu wa Mashetani na Baba wa Uongo na muuaji yote. Na Jina lake halitakwi na mashetani. Kwakua ni Jina Kuu Sana na Takatifu sana.