Mtume Muhammad: Jamii isipotoshwe; Jua huzama katika Chemchemu ya matope Meusi na Mazito

Mtume Muhammad: Jamii isipotoshwe; Jua huzama katika Chemchemu ya matope Meusi na Mazito

Status
Not open for further replies.
Picha ya kwanza na ya tano nikiwa namsimulia mtu jinsI nilivyoliona jua linazama nikamiambia nimeliona jua linazama kwenye maji nitakua namaanisha linazama kwenye maji kweli au ndivyo nilivyoona kwa muono wangu? VipI kuhusu picha ya pili Jua si naliona linazama ardhini? Na picha ya tatu utamuelezeaje mtu kwamba unaliona jua linazama vipi? Nikisema nyuma ya mlima nitakosea? Picha ya nne nikisema jua limezama kwenye mawingu meusi je?

Nadhani hata huyo anaesimuliwa katika Qur an anasema aliliona jua linazama katika matope meusi kwa muono kama huo hapo juu.View attachment 814741View attachment 814742View attachment 814743View attachment 814744View attachment 814745
Mkuu mjadala uhaumaliza mapema tu.......hizi picha zimemaliza ubishi wote,wenye akili washakuelewa japo huyu muanzisha mada ataendelea kujifanya haelewi.Umesaidia sana kuleta hz picha mkuu.
 
Muhammad alikuwa mwanaume na mwanaume hawezi kuogopa aibu.Watoke wanazuoni wa kiislamu leo mbele, waiambie dunia kwamba hilo lilikuwa ni tangopori na dunia itawaelewa tu na maisha yatasonga mbele.Waifute hiyo aya katika Kurani ili kuepusha Vizazi vijavyo kuendelea kukuta vitu vya aibu namna hiyo, kwa sababu madhara yake ni makubwa.Watoto wa jamii ya Kiislamu wanadumazwa kisayansi kwa sababu wata-tend kuiamini Kurani kuliko Sayansi.
Mkuu.. It's too bad u've ur own conclusion on the matter!! Laiti lengo lako lingekuwa ni kuelewa.. Ni kitu kidoogo saana hicho.. Ungeelewa!! But lengo lako 'ni kukejeli.. Basi utafanikiwa ktk Hilo!! Huyo mtume Mohammad صلى الله عليه وسلم uliye mdhihaki NA kukejeli alipata kusema..' hakika kila amali/jambo italipwa/itafanikiwa kulingana na niya/dhumuni '... Nakuapia huto elewa kamwe hadi utakapo kuwa na niya thabit ya kueleweshwa!!!
 
Unaelewa kwamba aya kuwa na utata tu ni ushahidi Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo?

Unaelewa kwamba habari za Mungu kuhitaji kuelezewa kwa kitabu, kwa tafsiri ya lugha fulani tu, kunaonesha huyo Mungu hayupo?

Kama yupo, kwa nini atoe kitabu chake kwa lugha fulani?

Kwa nini asiweke habari za kuwepo kwake kwenye DNA wote tujue pamoja?

UMESHASOMA MAJIBU YA MASWALI YAKO ULIYOLETA ???
 
Ndugu usipotoshe Qur'an Kwa kuitafsiri wewe utakavyo!!!

(18:86) until when he reached the very limits where the sun sets,63 he saw it setting in dark turbid waters;64 and nearby he met a people. We said: "O Dhu al-Qarnayn, you have the power to punish or to treat them with kindness."65
63. “The setting place of the sun” does not mean the place of the setting of the sun. According to Ibn Kathir, it means that he marched to the west conquering one country after the other till he reached the last boundary of the land, beyond which there was ocean.
Mabubu.. Viziwi.. Vipofu... Nao kamwe hawatorejea..!! Lengo lke ni kutafuta contradiction.. Na c kuelewa
 
Hata kama wamegundua kwamba Mungu hakuwahi kusema hivyo kwamba Jua linachwea katika matope meusi,ni suala la kukiri tu hadharani na kufuta hiyo aya na kisha maisha yanaendelea.Kwani kuna shida gani kufuta hiyo aya katika Kurani na kubakisha yale yaliyo ya kweli?
Umejua ni matope ya wapi..matope meusi..
 
Unamkumbuka yule mwanafasafa wa kirumi aliyeuwawa na kanisa katoliki kwa kusema dunia ni duara na siyo flat?
Kurudi kwenye swali lako ni kwamba Quran haisomwi kama riwaya za kufikirika bali ipo kwa mafumbo ambayo huhitaji kusherehewa na kutafsiriwa kwa kutumia vitabu vingine na wanazuoni wasomi.
Vitu kama hivi mkuu ni beyond your tiny capabilities kuelewa..
Mfano " tumemuumba Adam kwa udongo.." kwa tiny brain yako utadhani Allah alikuwa na washirika.
Just let it go hii sio riwaya ya Eric Shigongo
Amejua ni matope ya kidimbwi cha mvua!!!!!
 
UMESHASOMA MAJIBU YA MASWALI YAKO ULIYOLETA ???
Majibu yote yanajibu maswali.

Maana yake habari za Mungu zina utata.

Majibu yanazaa utata zaidi badala ya kumaliza utata.

Mungu alishindwa kufanya habari zake zieleweke bila utata?

Kwa nini kashusha habari zake kwenye kitabu cha lugha ya Kiarabu wa wakati fulani wakati aliweza kuziweka hizo habari katika DNA ya kila mtu azijue hata kama hajawahi kujua lolote kuhusu Waarabu wala mtume?

Mungu alishindwa kufanya hivyo na kutuondolea utata kuhusu hizi habari?

Kama hakushindwa? Kwa nini hakufanya hivyo?
 
Hapana.

1.Hujathibitisha kwamba Mungu yupo, hutakiwi kusema Mungu anaumba hivi au vile kama hujathibitisha Mungu yupo.

2. Mungu gani hana logical consistency? Unaelewa kwamba bila logical consistency unakosa msingi wowote wa kusema Mungu yupo? Unaelewa ukikataa logical consistency umekubali unaposema Mungu yupo umaanishe hayupo na unaposema hayupo umaanishe yupo na chochote unachosema kiweze kutafsiriwa vyovyote? Unaelewa kwamba ukikataa logical consistency huna cha kujadili hapa, kwa sababu mjadala unataka logical consistency?
Sioni busara ya asie amin Mungu kujadili mambo ya Mungu!!!!
 
Sioni busara ya asie amin Mungu kujadili mambo ya Mungu!!!!
Ikiwa dawa ya UKMWI haipo.

Na kuna waganga wa uongo wanauza unga wanasema unatibu UKIMWI.

Na watu wanaamini.

Na kuna mtu anayejua kwamba hiyo si dawa ya UKIMWI.

Utasema huoni busara ya mtu anayesema hii si dawa ya UKIMWI kusema hivyo?
 
Hakikuzungumzwa katika Quran hiko unachomaanisha, hiyo ni mojawapo ya historia ya mmoja wa Manabii aliyetajwa ndani ya Quran. Hiyo aya ndiyo inaelezea kuhusu Juja wa majuja.

Mwanadamu kuna muda majira ya kuzama unaliona kama linaingia ziwani kama ziwa lipo upande wa unaozamia jua. Huo ni udhaifu wa macho yetu ulivyo, na huo ndiyo uliyosemwa hapo maana ilitajwa jinsi wanadamu walivyokuwa wakiona. Ndiyo kilichomaanishwa hapo hizo sayansi zipo ndani ya Quran, ila si huo uzushi wako

Hebu ukijaribu kukosoa fuatilia, itakuepusha usionekane poyoyo na pia kutunza heshima yako.

Munasema Mungu alikuwa anamusimulia Muhammad juu ya jinsi Alexander the Great alivyoliona Jua kadri ya upeo wake.Hii aya katika sura hiyo hiyo, inamaanisha nini? Ni nani hapo analiona Jua linapochomoza likiinamia kulia?

"18:17 - Na unaliona jua linapo chomoza linainamia kuliani mwao kutoka hapo pangoni; na linapo kuchwa linawakwepa kushotoni, na wao wamo katika uwazi wa pango. Hizo ni katika ishara za Mwenyezi Mungu. Ambaye Mwenyezi Mungu anamwongoa basi huyo ni mwenye kuongoka. Na anaye muacha kupotea basi hutampatia mlinzi wala mwongozi."
 
Maswali yote yanahusu Mungu na logical consistency.

Utamshambuliaje Mungu wa Quran kwa sababu hana logical consistency (kitu ambacho hata mimi nakiona0 halafu hapo hapo nikikwambia hata Mungu wa Biblia naye hana logical consistency hivyo Quran na Biblia vyote vina ujinga ule ule wa Mungu asiye na logical consistency ukakimbia swali kuhusu logical consistency hiyo hiyo ya kumhusu Mungu?

Hapa unaonekana unapenda kumshambulia Mungu wa Quran kwa sababu hana logical consistency, lakini, ukiulizwa habari hizo hizo za logical consistency kuhusu Mungu wa Biblia, unakimbia kujibu maswali.
Hahahaaa....
 
Mmi na-maintain hoja kwamba hoja iliyoko mezani ni juu ya Jua kuzama katika matope.Hoja za Mungu hayupo, nitazikabili siku nyingine.Hizi hoja kabla ya wewe kuzikopi somewhere, kuna watu wengi wenye akili waliwahi kujiuliza hata ya unavyojiuliza wewe lakini walipatiwa majibu.Mimi nitakujibu, tena na kwa kuongezea na maswali mengine ambayo wewe hata huyajui na wala hujawahi kuyauliza katika kuhoji Metafikizikia ya Mungu.
Unamkwepa kiranga ili mada yako ishambulie upande unaoutaka..hahahaaa
 
Habari za kisha nikaona farasi mweupe kama saruji,akija mawinguni,na mgogoni amekaa mwana wa Adam,akiwa na upanga,
Ukizitafsiri kwa sasa,haingii akilini farasi kupaa angani,na haileti maana,mwana wa adamu kupambana na upanga zama hizi za makombora ya cruiser.
Lugha iliyotumika ni kwa ajili ya wakati huko,na bahati mbaya mungu hajaleta new version
Kweli.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom