Mtume Muhammad: Jamii isipotoshwe; Jua huzama katika Chemchemu ya matope Meusi na Mazito

Mtume Muhammad: Jamii isipotoshwe; Jua huzama katika Chemchemu ya matope Meusi na Mazito

Status
Not open for further replies.
Mimi nashindwa kumuamini Mohammad kwanza wakat anapokea revelations ushahidi hakuna alikuwa peke yake
2 hakufanya miujiza zaidi ya kupaa na farasi(hakuwa na shahidi aliemuona) tofauti na Yesu aliemfufua Lazaro watu wakishuhudia
Aliuliza tufani ziwani watu wakishuhudia
Akitembea juu ya maji watu wakishudia
Alinisha watu 5000 hii ni miujiza isio na shaka kwanin Mohammad alipokea maandiko pekee yake bila ushahidi tutakuamini vipi?
 
Unamkwepa kiranga ili mada yako ishambulie upande unaoutaka..hahahaaa
Mtu anakwambia hataki uongo.

Mpaka hapo niko naye. Na mini sitaki uongo.

Anaonesha uongo wa Quran. Mpaka hapo niko naye. Na mimi nauona uongo wa Quran.

Nikimwambia tuendelee kupinga uongo basi. Na huu wa Biblia nao ni uongo. Tuupinge. Au kama unaona si uongo nieleweshe labda mimi nakosea.

Mtu anakimbia mjadala. Hataki kujadili uongo wa Biblia.

Hapo naona huyu hapingi uongo.

Anapinga Quran tu.

Uongo wa Biblia mbona anaukumbatia na hataki kuujadili?
 
Hahahahaha jua haina pa kuzalia labda ulimaanisha black hole
Hata kama wamegundua kwamba Mungu hakuwahi kusema hivyo kwamba Jua linachwea katika matope meusi,ni suala la kukiri tu hadharani na kufuta hiyo aya na kisha maisha yanaendelea.Kwani kuna shida gani kufuta hiyo aya katika Kurani na kubakisha yale yaliyo ya kweli?
 
na kule Roma ilikuwa unafungiwa sakramenti au kufukuzwa kabisa kuwa muumini kama ungetamka kuwa "dunia inalizunguka jua" pia wanasayansi wa kanisa waliamini du

Likewise nia ni kama meza hivi ambapo unaweza kutembea hadi mwisho ambapo kuna "korongo" kubwaa!
Sasa hivi kanisa linapambana na utafiti na majaribio ya stem cell, maana siku akitengezwa binadamu kwenye maabara ndio utakuwa mwisho wa mafundisho ya "dhambi ya asili"

Sijawahi kuiamini hii misahafu na waandishi wake! Japo mimi ni mkatoliki kanisani huwa naenda kama " social activity" na sio kuitafuta mbingu.
 
Embu msipoteze muda na porojo ! The sun is almost entirely made of two Major gases
Hydrogen 75% &,helium15%
The huge amount of thickness of the gases leads to nuclear fusion which produces light/heat
The light give us life here on earth
 
Usifikirie nimekuja kufurahisha genge au kwamba nina kahoja kamoja nimekaolkota huko na kisha kukimbia nako hapa.Kwa taarifa yako unajadiliana na mtu anayemfahamu Muhammad, Kurani na Uislamu kwa kina.Kung'an'gania hoja moja ya Jua kuzama ni kuonyesha uweledi wangu katika mijadala.Siwezi kujadili hili na hapo hapo nikawa nimerukia suala jingine.Mpaka hoja hii ionekane kwamba imejadiliwa exhaustively ndio nitahamia hoja nyingine.
Nilitaka kuingia kwenye mjadala ila nikakutana na Swali la Joshua kusimamisha jua wakati jua lipo static na bado watu wanaami kuwa kweli alisimamisha nikaona bora niwaachie wafia dini.
 
Unamkwepa kiranga ili mada yako ishambulie upande unaoutaka..hahahaaa

Ni mtu ambaye hajasoma vizuri na kutaalumika vya kutosha katika masuala ya Mantiki ndiye anaweza kuona alichokifanya Kiranga ni suala la Kisomi.Mjadala ni juu ya Jua kuzama katika matope meusi, yeye Kiranga anakuja anazusha mjadala mpya ndani ya mjadala! Katika ulimwengu wa Logiki hilo ni kosa na linaitwa The Fallacy of Red Herring Arguments.Kwa hiyo, ni kwa kuelewa kuwa Kiranga kafanya kosa hilo la kimantiki,mimi sijataka kabisakufanya kosa kama hilo.

Mimi natambua makosa yanayofanywa na watu katika mijadala na mwisho wa siku wanashindwa hoja hivi hivi tu.Wakati ukituruhusu siku nyingine tutajadili suala la makosa ya kimantiki munayofanya waislamu munapokuwa mnajibu hoja za Muhammad na Uislamu.Mambo haya lazima muyafahamu vizuri vinginevyo mtaendelea kuonekana vichekesho katika kila Angle kuanzia kwenye unabii hadi namna munavyoutetea huo unabii.
 
Embu msipoteze muda na porojo ! The sun is almost entirely made of two Major gases
Hydrogen 75% &,helium15%
The huge amount of thickness of the gases leads to nuclear fusion which produces light/heat
The light give us life here on earth
Umeongea kitu kinachoweza kuwa verified na astronomical spectroscopy.

Astronomical spectroscopy - Wikipedia

Kuona kizazi cha leo bado kinaamini hiyo mivitabu ya dini iliyoandikwa katika zama za ujinga inayosema jua linazama kwenye tope ni jambo la fedheha kubwa.

Watu wa zamani naweza kuwasamehe hawakuwa na sayansi ya kujua mambo. Habari zilikuwa ngumu kupatikana. Hata kujua kusoma watu walikuwa hawajui. Vitabu vilikuwa anasa vinaandikwa kwa mkono.

Leo hii watu tunatembea na internet mkononi kwenye 4G networks halafu watu bado wanaamini hizi habari za Biblia na Quran bado?

Kwa kisa gani?
 
Embu msipoteze muda na porojo ! The sun is almost entirely made of two Major gases
Hydrogen 75% &,helium15%
The huge amount of thickness of the gases leads to nuclear fusion which produces light/heat
The light give us life here on earth

Mimi na wewe tunaweza kufahamu hivyo lakini ushahidi wetu ni upi juu ya hilo? Kwa mjibu wa Kurani,Mungu ndiye alimuona Alexander the Great (Dhul-Qarnaini) akiliona Jua likizama katika matope.Sasa mwenzangu mimi na wewe tuna ushahidi gani au ubavu gani wa kupingana na Mungu?
 
Mimi nilivyosoma Quran nikakutana na aya inasema kuna watu Mungu kawafanya mioyo yao iwe migumu wasimjue, akawaziba macho na masikio wasimjue, halafu Mungu huyo huyo atawahukumu watu hao hao kwa kutomjua Mungu, nikaona hiki kitabu ni cha kijinga sana.
Usiitukane kuran mkuu, waweza tupa mbadala wa kitabu unachoona chafaa kwa sisi kukiamini pasipo kuitukana kuran. We tupe tu book zako hizohizo za sayansi unazoziamini tupatie ili zitupindishie imani zetu kutoka kwenye kuran tuwe kama wewe!
 
na kule Roma ilikuwa unafungiwa sakramenti au kufukuzwa kabisa kuwa muumini kama ungetamka kuwa "dunia inalizunguka jua" pia wanasayansi wa kanisa waliamini dunia ni kama meza hivi ambapo unaweza kutembea hadi mwisho ambapo kuna "korongo" kubwaa!
Sasa hivi kanisa linapambana na utafiti na majaribio ya stem cell, maana siku akitengezwa binadamu kwenye maabara ndio utakuwa mwisho wa mafundisho ya "dhambi ya asili"

Sijawahi kuiamini hii misahafu na waandishi wake! Japo mimi ni mkatoliki kanisani huwa naenda kama " social activity" na sio kuitafuta mbingu.
Vatican imesubiri miaka 350 kukubali kwamba ilikosea na kumuomba radhi Galileo.

The New York Times waliandika hii habari hapa chini.

Halafu mtu anayefuata habari za hili kanisa eti naye anaisema Quran kwa sababu Quran ina uongo.

After 350 Years, Vatican Says Galileo Was Right: It Moves After 350 Years, Vatican Says Galileo Was Right: It Moves
 
Kama aya za kitabu cha Mungu zinahitaji msuli kuzielewa basi huyo Mungu kashindwa kazi na katungwa na watu tu, hayupo.

Aangekuwepo, aya zake zisingehitaji kueleweka kw amsuli.

As a matter of fact, Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na ujuzi wote haandikwi kwenye kitabu.

Kwa sababu ana access ya moja kwa moja kwenye ubongo wa kila mtu, kwa nini aandikwe kwenye kitabu?

Ukiona Mungu huyo kandikwa kwenye kitabu, ujue ni watu tu wameandika hizo habari.

Kwa nini Mungu asiweke kila kitu wazi kwa kila mtu kwenye ubongo wa kila mtu bila kuhitaji kitabu, sijui tafsiri kutoka lugha fulani na utata mwiiingi?

Mungu huyo hayupo, aliyeandikwa katungwa na watu tu.
Naona unajaribu kumfanya Mungu afikiri kama ewe mavumbi unavyofikiria!!
 
Usiitukane kuran mkuu, waweza tupa mbadala wa kitabu unachoona chafaa kwa sisi kukiamini pasipo kuitukana kuran. We tupe tu book zako hizohizo za sayansi unazoziamini tupatie ili zitupindishie imani zetu kutoka kwenye kuran tuwe kama wewe!
Kwa nini unanikataza kukikosoa kitabu kama kina uongo?

For starters, anza na Feynman's Lectures on Physics. Cha Richard Feynman. Series ya Lectures ina vitabu vitatu. Pitia vitatu vyote. Fanya na mazoezi yake.

Halafu nenda kwa Roger Penrose. Soma " The Road To Reality: A Complete Guide To The Laws of The Universe".

Hicho unaweza kusoma polepole huku ukipozea na "A Brief History of Time: From The Big Bang To Black Holes" cha Stephen Hawkings.

Halafu uje tujadili hapa.

Not that havina makosa, but the worldview is quite above the bullshit in the Quran and Bible. Plus it does nit clain to be beyond reproach. You can get a Nobel in Physics for improving this outlook.

Unlike the Bible or Quran.

Soma halafu tujadili.
 
Naona unajaribu kumfanya Mungu afikiri kama ewe mavumbi unavyofikiria!!
Kabla ya kusema Mungu hivi au vile.

Unaweza kuthibitisha yupo kwa namna yenye kutojipinga kimantiki?

Usiweke stories nyingi kumhusu Mungu ambaye hata kuthibitisha kwamba yupo huwezi.
 
Vatican imesubiri miaka 350 kukubali kwamba ilikosea na kumuomba radhi Galileo.

The New York Times waliandika hii habari hapa chini.

Halafu mtu anayefuata habaribza hili kanisa eti naye anaisema Quran kwa sababu Quran ina uongo.

After 350 Years, Vatican Says Galileo Was Right: It Moves After 350 Years, Vatican Says Galileo Was Right: It Moves

Hiyo sio hoja tena! Washauri sasa na Waislamu wafanye ammendments katika Kurani kuondoa hiyo aya?

Kiranga, mbona unajadili kwa kufanya makosa ya kimantiki? Hili unalofanya hujui kama ni Fallacy of False Assumptions? Huwezi kusema kama Muhammad alisema uongo basi iwe defense yake iwe ni kwamba nayo Vatikan ilimu-condemn Galileo! Hebu jaribu kuwa makini na mijadala ya kisomi mkuu!
 
Wanajukwaa:

Dunia yetu inaendelea kushika kasi katika suala la Sayansi na Tekinolojia.Kwa siku za hivi karibuni,wanasayansi wamegundua kuweza kutengeneza Moyo kwa kutumia stem cells,ikiwa ni hatua katika kuelekea kutengeneza moyo wa binadamu,hali ambayo itasaidia katika kukabiliana na matatizo ya Moyo yanayowakabili wanadamu,kwa kiasi kikubwa, yale ambayo uhusisha mwanadamu kupoteza maisha, kwa sababu tu Moyo wa mgonjwa husika hauna repair au hauwezi kubadilishwa.Miaka kama kumi hivi iliyopita,wanasayansi walikuwa wamefanikiwa kutengeneza Moyo wa panya kwa kutumia hizo stem cells.

Kumbe,kwa tafiti mbalimbali zinazoendelea kufanyika sehemu mbalimbali duniani,ama ardhini au angani,zote zinalenga katika kuboresha maisha ya mwanadamu na hata kuongeza siku za kuishi kwake.Historia inao watu wengi sana ambao wamejihusisha na Sayansi kwa nyakati tofuati tofauti.

Leo,ninataka tumuangalie Mtume Muhammad kwa namna alivyoweza kujihusisha na suala la Sayansi kwa kile kinachosemwa ni kwa msaada wa Mungu.Kurani neno la Mungu;maneno ambayo Mungu akiisha kuyaandika huko Mbinguni, alikuwa anampatia Malaika Gabriel na malaika Gabriel akampatia Mtume Muhammad katika Nyakati tofauti tofauti na Muhammad kuyaweka katika maandishi,lakini kwa namna ya pekee,kwa mara ya kwanza kabisa ikiwa ni katika Pango lililoko katika Mlima Hira, Jabal an-Nour,huko Makka,ambako inadaiwa Mtume Muhammad alipokea ufunuo huo, kwa matatizo sana kwa sababu ya kutojua kwake kusoma na kuandika,Malaika Gabrieli alijikuta anamkaba.

Kwa njia ya ufunuo wa Kurani,tunafunuliwa mambo mengi ya Kisayansi ambamo Muhammad anatujuza jinsi mambo yalivyo.Kwa leo, ninawaletea jambo moja tu.Nalo ni juu ya namna Jua linavyokuchwa na kadri Mungu atakavyotujalia tutayaangazia na mambo mengine.


Kurani kupitia Sura al-Kahf (18: 83-86), inaeleza kwamba Jua huchwea katika chemchemu ya matope meusi mazito(dark Muddy spring):

“83-Na wanakuuliza khabari za Dhul- Qarnaini. Waambie: Nitakusimulieni baadhi ya hadithi yake.84 -Sisi tulimtilia nguvu katika ardhi na tukampa njia za kila kitu.85 - Basi akaifuata njia. 86 - Hata alipo fika machwea-jua aliliona linatua katika chemchem yenye matope meusi. Na hapo akawakuta watu. Tukasema: Ewe Dhul-Qarnaini! Ama uwaadhibu au watwae kwa wema.”

Wakati Muhammad akiwa ametupasha ukweli huo ambao aliandikiwa na Mungu, Ukweli wa kisayansi umebainisha kwamba Jua ni kubwa zaidi na lenye joto kali kuliko dunia.Na ikitokea kwamba Dunia inakaribiana na Jua,basi dunia itayeyuka kutokana na joto kubwa la Jua.

Ukweli mwingine,ambao pia Sayansi imetupatia ni kwamba Jua halitembei bali sayari mbalimbali ndio hulizunguka,ikiwemo Sayari yetu ya Dunia. Historia inaonyesha kwamba mtu wa kwanza kugusagusa habari za kuwa Jua lilikuwa halizunguki alikuwa ni Aristarchus (310-230KK).

Aristarchus alikuwa ni mwana-Astronomia wa Kigriki.
Yeye aliamini dunia ilikuwa katikati ya Mfumo wa Jua(Solar system) na sayari zingine (ikijumuishwa na nyota ambazo zilikuwa zimefungwa katika nafasi fulani) ndio zilizokuwa zikilizunguka Jua.

Hata hivyo, baadaye mwanasayansi,Aristarchus, alikuja kugundua kuwa sio dunia iliyokuwa katikati ya Mfumo wa Jua, bali ni Jua na hivi kwamba ni Dunia na sayari zingine ndizo zilikuwa zikilizunguka Jua.Ugunduzi wa namna hii ulipatikana miaka mingi sana (takribani karne tatu hivi) kabla hata ya Yesu Kristu kuzaliwa na karne tisa kabla ya Muhammad kuzaliwa.

Mwanasayansi mwingine pia aliyekuja na mtizamo tofuati na wa Muhammad (kwa kadri ya ufunuo kutoka kwa Mungu) ni Jean Buridan (1300-1359/61). Huyu) anafahamika kama Mwanafalsafa Mashuhuri sana katika Ufaransa.Buridan alikuwa Mwalimu katika Kitivo cha Sanaa cha Chuo Kikuu cha Paris kwa kupindi chote cha maisha yake ya kitaaluma akimakinika hasa hasa katika masuala ya Logiki (Logic) na kazi za mwanafalsafa Aristotle.

Ni Bridan aliyeanzisha wazo juu ya kiitwacho Copernican Revolution katika Ulaya.Hili ni fundisho lililoleta mwangaza kutoka kuamini kwamba dunia ilikuwa imesimama sehemu moja katika ulimwengu na kwamba Jua ndio lilikuwa linaizunguka dunia (Geocentrism) hadi kueleweka kwamba kumbe Jua ndilo limesimama wakati dunia na sayari zingine zikilizunguka (Heliocentrism).

Kumbe, sasa kwa uchache,kwa mawazo ya hao wanasayansi wawili,tunapata picha kwamba Muenendo wa Jua kuchomoza na kutua sio jambo lililoanza wakati wa Muhammad.Na kama suala la Sayansi ya Mfumo wa Jua lilianza mapema kabla ya Yesu na Muhammad kuzaliwa, yeye Muhammad alipopewa ufunuo na Mungu, hakuweza kujiuliza iwapo ufunuo huo wa Mungu inakuwaje unapingana na ukweli wa mambo?Katika kutafakari ufunuo huu wa Mungu kwa Muhammad, nimejikuta nina maswali yafuatayo,ambayo naomba yatuongoze katika kujadili suala hili.Ni muhimu kujadili kwa sababu pengine Dunia inatufundisha vitu ambavyo havipo.Hivi kweli Mungu anaweza kumueleza Muhammad mambo ya uongo?Maswali mengine ambayo bila shaka hata wewe unaweza kujiuliza ni haya:

1. Hiyo Chemchemi ya matope mazito na meusi iko hapa duniani?Na kama haipo hapa duniani iko angani? Na kama iko angani iko sehemu gani?


2. Huyo Dhul-Qarnaini alikuwa ni kiumbe wa namna gani huyo aliyepewa uwezo wa kuona Jua linavyotumbukia katika matope?


3. Pamoja na kwamba wakati wakati wa Muhammad, labda Sayansi ya kwamba Jua halizunguki, isipokuwa dunia ndio hulizunguka Jua, ilikuwa haijafika katika maeneo ya ardhi ya Arabia, bado hata vizazi vya zamani sana havikupata kuwa na uelewa kama huo wa Muhammad kuwa Jua lilikuwa linatua matope meusi! Je,ilikuwaje katika Vizazi vyote hivyo hapo katikati(ikiwemo na Yesu mwenyewe ambaye Muhammad anamuelezea kama aliyekuwa na uwezo wa kufinyanga wanasesere na kuwapulizia uhai na wakawa ndege kamili), kabla ya Muhammad, akakosekana mtu mwenye uelewa wa kuliona Jua likizama katika matope meusi tofauti? Hivi wewe kwa sayansi hii ya Muhamma juu ya Jua kuchwea katika matope meusi haikupelekei kujiuliza yafuatayo:

· Je, Muhammad kusema mambo ambayo hakuwa nayo uthibitisho ilikuwa ni kutafuta tu kuonekana kwamba Mungu amempa ufunuo wa kipekee juu ya ulimwengu?


· Je, vizazi ya Kiarabu na dunia kwa ujumla baada ya kugundua kwa tafiti za kisayansi, ambazo zimethibitisha kuwa Jua huzungukwa na sayari mbalimbali, ikiwemo Sayari yetu ya dunia, vimuoneje, Muhammad na Uislamu kwa ujumla?


· Je,wanadamu wa vizazi vyote vinavyofahamu kuwa Jua halijawahi kuzama katika matope ama meusi,bluu au meupe, visimuamini Muhammad katika mambo mengine aliyoyasema au vimuchukulie kama mtu aliyekuwa anajaribu kupiga ramli ya jinsi mambo yalivyo?

Lakini swali la mwisho kabisa ambalo nitaomba ujiulize ni hili:Je,Ni kwa nini hadi leo baada ya kugundulika kuwa Jua halizami na wala halizunguki,ni kwa nini hadi sasa aya hiyo iko imesalia katika Kurani?Je,ni nani anasema uongo kati ya Mungu na wanasayansi juu ya suala la Jua?

Karibu kwa mjadala ili tupate kujua ukweli kwa faida ya maendeleo ya Dunia yetu.
UKIWEZA KUJIBU HAYA MASWALI UTAJUA MTUME MUHAMAD ANAKUPA SAYANS HALISI SIO UBABAISHAJ WA KIZUNGU.

1.Swali la kujiuliza n kwamba ulisha liona jua halizami????
na kama halizami huwa linaenda wap!!!

2.Je mchana likipungua makali huwa linakuwa limezama au yanaenda wap?

3.kwannn asubuhi jua ni moderate.mchana ni kalisana na usiku halipo?

Jiulize kama lingekuwa halizami bas kwann ukali wa jua la asubuh si mkali kama mchana?

Kwann yote yasiwe the same kwa ukali?

Hahaa sasa naona u get my point kwann rasul(saw) anakufunulia sayans isiyo na mashaka ndan yake.

4. TAMBUA TU: jua kutozama cjui dunia kujizungusha katika muhimili.
HIZI NI THEORY TUU SIO KWAMBA NDO UKWELI ULIVYO. HILI NI JOPO LA WAZUNGU LILIKAA CHINI LIKABUNI HIVYO .NENDA FORM ONE UKAANGALIE HIZI HABAR KOTE WAMEKUAMBIA THEORY TU HZ.

ukiweza kujib haya maswal naweza kukupa details kiundan sasa.

Then nkakujibu na maswal mengine ulo uliza
 
Hiyo sio hoja tena! Washauri sasa na Waislamu wafanye ammendments katika Kurani kuondoa hiyo aya?

Kiranga, mbona unajadili kwa kufanya makosa ya kimantiki? Hili unalofanya hujui kama ni Fallacy of False Assumptions? Huwezi kusema kama Muhammad alisema uongo basi iwe defense yake iwe ni kwamba nayo Vatikan ilimu-condemn Galileo! Hebu jaribu kuwa makini na mijadala ya kisomi mkuu!
Nani kakwambia namtetea Muhammad hapa?

Wewe ndiye mtu unayejiita mwerevu? Kwa sloppy thinking hii ya kunisema nafanya false assumption wakati wewe ndiye unafanya false assumption kwamba namtetea Muhammad hapa?

Unajua kusoma wewe?

Wewe mbona unafanya double standard?

Unaisema Quran kwa kuwa na uongo. Nakubaliana nawe. Quran ina uongo wa kitoto. Sikubishii hapo.

Sasa mbona nikikwambia na Biblia nayo ina uongo wa kitoto hivyo hivyo unakimbia mjadala?

Au uongo unauona ukiwa kwenye Quran tu, ukiwa kwenye Biblia unakuwa si uongo, unageuka ushairi?
 
UKIWEZA KUJIBU HAYA MASWALI UTAJUA MTUME MUHAMAD ANAKUPA SAYANS HALISI SIO UBABAISHAJ WA KIZUNGU.

1.Swali la kujiuliza n kwamba ulisha liona jua halizami????
na kama halizami huwa linaenda wap!!!

2.Je mchana likipungua makali huwa linakuwa limezama au yanaenda wap?

3.kwannn asubuhi jua ni moderate.mchana ni kalisana na usiku halipo?

Jiulize kama lingekuwa halizami bas kwann ukali wa jua la asubuh si mkali kama mchana?

Kwann yote yasiwe the same kwa ukali?

Hahaa sasa naona u get my point kwann rasul(saw) anakufunulia sayans isiyo na mashaka ndan yake.

4. TAMBUA TU: jua kutozama cjui dunia kujizungusha katika muhimili.
HIZI NI THEORY TUU SIO KWAMBA NDO UKWELI ULIVYO. HILI NI JOPO LA WAZUNGU LILIKAA CHINI LIKABUNI HIVYO .NENDA FORM ONE UKAANGALIE HIZI HABAR KOTE WAMEKUAMBIA THEORY TU HZ.

ukiweza kujib haya maswal naweza kukupa details kiundan sasa.

Then nkakujibu na maswal mengine ulo uliza

Naona wewe ndiye wakati Muhammad anapewa ufunuo kule pangoni ulikuwa pamoja naye.Wewe ni mjuzi kabisa wa Kurani.Hongera kwa sayansi ya Kiarabu mkuu!
 
Mimi nashindwa kumuamini Mohammad kwanza wakat anapokea revelations ushahidi hakuna alikuwa peke yake
2 hakufanya miujiza zaidi ya kupaa na farasi(hakuwa na shahidi aliemuona) tofauti na Yesu aliemfufua Lazaro watu wakishuhudia
Aliuliza tufani ziwani watu wakishuhudia
Akitembea juu ya maji watu wakishudia
Alinisha watu 5000 hii ni miujiza isio na shaka kwanin Mohammad alipokea maandiko pekee yake bila ushahidi tutakuamini vipi?
Sema tu hujui brother. Unachokisema hakipo hivo.
Hakupokea akiwa pekeake broo.
Kasome vzr.

Uislam si din ya kusoma juu juu ukaja apa kuandika comment.

Unahitaj deep investigatio na intesive reading ndo utaweza bro.

Mtaaibika jmn. Uislam kila kinachoandikwa mule dunia inafanya research mpka leo wana prove n kwel.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom