Gavana
JF-Expert Member
- Jul 19, 2008
- 33,637
- 8,947
Ulikuwepo wewe pangoni na zawadi uliyopata ni hii kwa kuwepo pangoni
HALI AU JIHA MBALI MBALI ZA NAFSI MOJA:
Kuhusu jambo la kwanza linalowezekana miongoni mwa hayo manne hapo juu hakuna haja ya kulijadili zaidi, kwani hamna siku hizi Mkristo yeyote ambaye angemwamini Yesu kuwa hali ama jiha moja ya Mungu kuliko kuwa nafsi moja maalum.
Wanaouamini utatu wanasisitiza kuwepo kwa nafsi tatu tofauti zilizounganika na zikawa moja.
Pindi mtu anapokubali habari hiyo ya nafsi moja yenye hali mbali mbali zikidhihirika wakati mmoja, papo hapo itikadi ya Utatu, yaani miungu watatu katika mmoja, inatokomea, pasipo kubakia utatu wowote kabisa.
Basi atakayebakia ni Mungu Baba ambaye kwa kuona huruma atakufa kwa ajili ya madhambi ya watu.
Na hiyo itakuwa ni hali ya kupita ya nafsi hiyohiyo. Hali mbalimbali siyo nafsi, wala jiha mbalimbali hazimaanishi dhati tofauti. Mtu yeyote anaweza kupitia hali mbalimbali bila ya kugawanyika katika wawili, watatu ama watu wengi.
Hivyo, kama Mungu akiamua kufa kwa ajili ya watu wenye dhambi, basi ni Mungu mwenyewe atakayekufa siyo hali zake fulani tu zitakazokufa.
Basi kuhusu habari tunayozungumzia, ile hali ya Mungu ambayo ilifanya kazi kubwa sana ya kutoa dhabihu yake kwa ajili ya watu wenye dhambi inaweza kufahamika kuwa kazi ya sifa moja tu yake. Hivyo, kama huruma ya Mungu peke yake ikihesabiwa kuwa 'nafsi' na nafsi hiyo ikapewa jina Yesu Kristo, hapo kile kilichokufa ni 'huruma' ya Mungu.
Upingamizi mkubwa ulioje huu ya kwamba huruma ya Mungu ikiwahurumia watu wenye dhambi inajiua. Hiyo inamaanisha ya kwamba Mungu hakubakiwa na huruma kwa siku tatu mchana na usiku.
Kumbukeni kwamba hapo Yesu hakuhesabiwa nafsi tofauti ya kujitegemea, bali ni sifa ama hali ya huruma ya Mungu ambayo
huruma hiyo ikadhihirika kwa sura ya mtu. Na mtu huyo kwa vyovyote ndiye Mungu mmoja asiyeweza kugawanyika. Basi
kama chochote kilikufa katika kisa hicho, hicho ni Mungu Mwenyewe ama ni sifa yake ya Huruma iliyofanya kazi kubwa
sana katika tukio hilo.
Basi hatuna hiari yoyote isipokuwa kuamini kwamba Huruma ya Mungu ilikufa ama Mungu Mwenye Huruma Mwenyewe Alikufa.
Matatizo mengi yatazuka kutokana na madai ya kwamba hali au sifa fulani inaweza kufutika kwa muda ama kwa kudumu. Habari
hiyo inaweza kueleweka vizuri ikilinganishwa na majaribu ya binadamu. Mtu anaweza kupoteza nguvu yake ya kuona au kusikia
kwa muda au daima, lakini mtu huyo bado atabaki kuwa yule yule mtu aliye hai.
Kifo cha nguvu moja ya mtu kwa hakika ni nusu kifo cha mtu huyo.
Hatimaye mwenye kupata hasara ama kusumbuka anakuwa mtu yuleyule