Ukristo zaidi ya Dini. Ni zaidi ya Usabato na Uroma..tunaamini kua Yesu ndiye Mwokozi na njia ya kwenda mbinguni.
Na Yesu anasema; Wenye nguvu ndio watakaouteka ufalme wa Mungu.
Hawa ni wanadamu wote wanaomtafuta Mungu kwa Nia ya dhati kabisa mioyoni mwao wakizifuata njia. Hata kama wako katika imani isiyo sahihi. Mfano Wanaweza kua waislamu, wabudha, wahindu wayahudi nk. Mungu huwatafuta hao na kuwabadili ili wamgeukie Mungu wa kweli katika Kristo Yesu bwana wetu. Lakini wale wote wenye kufuata Dini zao kwa unafiki, Mungu atawatapika. Kwahiyo Usilamu, ubudha nk sio kikwazo kwa Mungu kuwafikia watu hawa maalumu na kuwageuza kumgeukia Mungu.
Kwakua Tunaamini kwa Mwanadamu Kumjua Mungu wa Kweli, Sio kwa Uwezo wake peke yake. Inahitajikai Mungu aingilie kati na ajidhihirishe kwake.
Na haya yapo kimaandiko ndani ya Bibilia.
Mf.
Siwezi kukubadili Dini yako ya Allah, ila Mungu mwenyewe anaweza. Sihitaji nikushikie Panga, bastola mabomu, nikulazimishe au nikupige Taqiyah na kitman ili umuamini Kristo. Kwakua ile kusema uongo ni dhambi tosha. Nachoweza nikukuambia Ukweli. Nawe kamwombe Mungu unavyojua wewe kwa unyenyekevu wako ili aweze kukuongoza yeye mwenyewe kwenye Kweli. Kwakua MUNGU ANASIKIA.