Hilo si swali ilaha [emoji117]
View attachment 863120 hata baba kassim ameonya [emoji117]
View attachment 863117 kwa vile wewe si muumini ndio sababu nakupotezea [emoji33] [emoji33] [emoji38] [emoji38]
Sifa kuu za mungu-mtu wa Ukristo kama zilivyohubiriwa na Paulo
Wakati tukiendelea kupata uchambuzi huu maridhawa juu ya mungu-mtu wa dini ya Kikristo, jambo lingine muhimu ambalo ningependa kuligusia ni kwamba, kulingana na maelezo ya Biblia tukufu, Bwana Paulo ninayemzungumzia hapa ndiye aliyekuwa mtu wa kwanza katika agano jipya kuandika nyaraka zake kabla ya waandishi wengine wa agano jipya kuandika Injili zao na nyaraka zao.
Aidha, Biblia inaeleza pia kuwa Bwana Paulo alipokuwa akiandika nyaraka zake hizo alikuwa akiandikia dini yake ya Ukristo (ya mungu-mtu huyo na ibada zake).
Waandishi hao wa agano jipya ambao imeripotiwa kuwa nao pia waliuandikia Ukristo ambapo walianza rasmi kuandika Injili zao na nyaraka zao kuanzia miaka ya 36 hadi 45 baada ya Paulo kuandika na kusambaza nyaraka zake hizo (rejea Biblia ya Wakatoliki Imprimatur, Mihayo, 1967 Tabora, kwenye maelezo juu ya nyaraka za Paulo na kwenye maelezo ya Injili mbalimbali).
Kwa shuhuda hiyo, ni wazi kuwa waandishi hao nao pia walikuwa wakiiandikia dini ya Kikristo ya Paulo.
Kwa hali hiyo, imedhihirika kuwa baada ya Bwana Paulo kuzichukua imani na ibada za watu wa mataifa (au wapagani) na kuziandika kwenye nyaraka zake na kudai kuwa zinamhusu Yesu (a.s.) kazi ya pekee iliyofanywa na waandishi hao ni kusherehesha maneno hayo ya Paulo kama yalivyo kwenye nyaraka zake.
Kwa maantiki hiyo, kama tulivyoona katika toleo lililopita kwamba
sifa kuu mojawapo ya miungu-Zeu na Herme ya wapagani kwamba
ni kufa, Bwana Paulo naye alifundisha kuwa mungu wake huyo (mungu-mtu) aliyemhubiri kuwa na desturi moja na miungu hiyo (ya wapagani) na kumwita "Yesu" kwamba naye vile vile anayo sifa hiyo (ya kufa), kwa kusema:
"Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali kwenye dhambi". (Warumi 5:8)
Hapa Bwana Paulo anafundisha wazi kuwa mungu wake huyo aliyemwita "Yesu" (Kristo) alikufa! Sambamba na mafundisho yake hayo, ili kuthibitisha kwamba waandishi wa Injili na nyaraka wa agano jipya kwamba mara nyingi walikuwa wakisherehesha nyaraka za Paulo, sifa hiyo (ya kufa) aliyonayo mungu huyo wa Paulo baadae nao waliishabikia ajabu, kwa kuandika kwa mapana na marefu; ambapo kila mwandishi aliandika kwa staili ya aina yake katika juhudi za kumpambia mungu wao huyo sifa yake hiyo (ya kufa), hali iliyoibua mgongano mkubwa kimasimulizi na kuwaacha wasomaji wasijue nani mkweli. (Tazama Injili ya Mathayo, Marko, Luka,Yohana na nyaraka za Petro, Yohana, Yakobo, Yuda na Ufunuo wa Yohana n.k.)
Na ndivyo hivyo hivyo waandishi hao walivyosheresha kwa unazi sifa ya kufufuka (ya miungu- Zeu na Herme) miaka michache baada ya 'mwalimu wao', Bwana Paulo kuandika katika nyaraka zake kwamba mungu wake huyo aliyemwita "Yesu" naye vile vile anayo sifa hiyo (ya kufufuka), kwa kusema:
"Mkumbukeni Yesu Kristo aliyefufuka katika wafu, wa uzao wa Daudi kama inenavyo Injili yangu". (2 Timotheo 2:8)
Kwa ufupi, haya ndio mafundisho ya Bwana Paulo yaliyo katika Injili yake yakiithibitisha sifa kuu nyingine ya kufufuka aliyonayo mungu wake huyo aliyemwita "Yesu", ambapo baadae waandishi wa agano jipya waliisherehesha kwa mapana na marefu. (Rejea Injili na nyaraka zao).
Sifa Kuu nyingine za Mungu huyo wa Paulo na Ukristo mwenye asili na desturi za miungu-watu ya wapagani, kwa uchache waandishi hao walizisherehesha katika Injili zao kama ifuatavyo:
Kuzaliwa na mwanamke (Tazama Luka 2:4-7)
Kuvikwa nguo ( Luka 2:6)
Kuona kiu (Yohana 19:28)
Kula na kunywa (Mathayo 11:19 na Yohana 4:7)
Kuvuliwa nguo (Mathayo 27:27-28)
Kupigwa (Mathayo 27:27-30)
Kulia machozi (Yohana 11:35)
Kuchoka (Yohana 4:6)
Kulala usingizi (Mathayo 8:23-24)
Kutokujua mambo yote (Mathayo 24:36)
Kuwa na ukoo (Mathayo 1:1)
Kwa uchache, hizi ndizo sifa kuu za mungu wa Paulo aliyemwita "Yesu" mwenye desturi ya kujigeuza kuwa mwanadamu sawa na miungu-Zeu na Herme inayoaminiwa na wapagani. Na kama tulivyoona katika sifa za kwanza za mada hii katika gazeti hili, Mungu-Yehova ameepukana mbali kabisa na sifa zote hizi.
Kwa shuhuda hizo, ni wazi kuwa mungu aliyemhubiri Paulo ambaye ndiye mungu wa Wakristo, siyo Mungu-Yehova ambaye ndiye Mungu wa Nabii Ibrahimu, Ismaili, Isaka, Yakobo, Nabii Yesu, Muhammad na Mitume na Manabii wake wengine wote aliowatuma duniani (a.s)