Hujui KUSOMA gavana [emoji117]
View attachment 885377 pia baba yako hakukuonya [emoji]
View attachment 885380 ndio sababu ni muongo na kudhani dhania kila siku [emoji117]
View attachment 885384
NAFSI MBALI MBALI ZENYE SIFA TOFAUTI KABISA
Kama Mungu Baba, Yesu na Roho Mtakatifu ni nafsi tatu zenye sifa mbali mbali kabisa ambazo katika hizo hazishirikiani zote tatu, hapo hizo tatu haziwezi kuhesabiwa kuwa 'Tatu katika moja' na 'Moja katika tatu'.
Utatu unaweza kuunganika ukawa umoja hasa hapo tu ambapo nafsi zote tatu zinakuwa na mienendo ile ile na sifa zile zile na kazi zile zile na nguvu zile zile za aina moja wala hamna hata sifa moja maalum inayoitenga moja na nafsi nyingine mbili.
Hiyo inaweza kufananishwa kiasi fulani na watoto watatu waliozaliwa kutokana na mimba moja ambao wanafanana sana sana kabisa, hata fikra zao, maono yao na kazi za viungo vyao vinaafikiana mno hata kwamba majaribu ya kila mmoja wao ni majaribu ya wote hao kikamilifu bila tofauti yoyote.
Kama ndivyo ilivyo, hapo Utatu wa Mungu, Mwana na Roho Mtakatifu utaweza kueleweka zaidi. Lakini bado tatizo litabaki kuhusu miili mitatu yenye nafsi hizo tatu zinazofanana kwa kila jiha kikamilifu.
Lakini hiyo haiafikiani na wazo la Kikristo juu ya Utatu.
Mtu akiangalia mara ya pili analazimika kuwaza picha ya mwili mmoja wenye nafsi tatu mle ndani. Lakini umoja huo wa watatu unaweza kuzingatiwa hapo tu ambapo mwili mmoja ukiweza kuwa na nafsi tatu ndani yake, jambo ambalo linazua matatizo mengi.
Naam, kwa kuwa Mungu hana mwili, kwahiyo mithali ya mwili wa kibinadamu ilivyoshauriwa nyuma haifai. Twajua sana ya
kwamba Mungu hana mwili, lakini bado tatizo litabakia kuhusu dhati tatu za kiroho zilizo kama wale watatu waliozaliwa kutokana
na mimba moja wanaofanana, wanaokuwepo mbalimbali lakini wanaungana katika mambo mengine yote.
Tatizo jingine litakalowakabili hao watatu wa kukisiwa ni namna wanavyohusiana wao kwa wao katika habari ya ibada. Je, nafsi
zote tatu za 'Tatu katika Moja' zinaabudiana zenyewe kwa zenyewe? Je, zote hizo zinapokea ibada za viumbe vyao, lakini
haziabudiani zenyewe kwa zenyewe?
Ingawaje Yesu Kristo anatajwa mara kwa mara katika Agano Jipya akimwabudu Mungu Baba na anawasihi wengine pia kumwabudu Yeye.
Lakini haikuelezwa kuhusu Roho Mtakatifu akimwabudu Mungu Baba. Tena hamna kabisa habari ya Yesu kujaribu kuwaelekeza wengine kumwabudu yeye wala kumwabudu Roho Mtakatifu sawa na taarifa ya Agano Jipya.
Mtu anakanganywa na kutokutajwa kuabudiwa kwa Yesu na Roho Mtakatifu katika Agano Jipya, lakini habari ya Mungu Baba
kuabudiwa imetajwa mara kwa mara.
Ijapokuwa ni desturi ya kawaida ya Wakristo kumwabudu Yesu kuwa 'Mwana wa Mungu' pamoja na kumwabudu Mungu Baba, hata hivyo hamna taarifa yoyote iliyohifadhiwa katika maandiko ya kwamba mwanafunzi yeyote wa Yesu Kristo aliwahi kumwabudu yeye, ama Yesu akawaelekeza kufanya hivyo katika muda wote aliokaa ardhini.
Hata kama yeye angelifanya hivyo, maswali mengi yasiyoweza kujibika yangezuka. Ndivyo ilivyo hali ya Roho Mtakatifu, yeye naye hakumtaka yeyote kumwabudu yeye.
Kwa nini? Ile hali imekwisha chunguzwa tayari kiasi fulani ambako hao walikuwa 'Tatu katika Moja' katika maana hii ya kwamba
utambuzi wao wa kuwapo kwao ulikuwa mmoja juu ya kugawanyika katika hali ama jiha tatu. Dhati ya aina hiyo haiwezi kiakili kuhesabiwa kuwa 'watu watatu katika mmoja'. Aidha, hali ama jiha haziabudiwi, wala hazijiabudu.
Kwa kuwatambua kuwa watu watatu tofauti, wanalazimika kujijua wanakuwapo kwa kujitegemea. La sivyo, suala la kujitaja ama kuwataja wengine kwa kusema 'Mimi', 'Wewe' na 'Yeye' halizuki asilani.
Utatu ukitumika kwa dhati moja humaanisha sifa tu basi. Na sifa kwa kweli hazina kikomo, haziwezi kuwa tatu tu. Tujue tusijue,
Mungu anazo sifa nyingi teletele.
Kwa kumalizia mazungumzo haya, nasisitiza mara nyingine ya kwamba suala la wao kuabudu wao kwa wao linaweza kuzuka
hapo tu ambapo hao wangekuwa watu watatu wenye madaraka mbalimbali na sifa tofauti.
Katika shauri hiyo, mmoja tu ataabudiwa na wengine wawili wakiwa wenye daraja dogo watatazamiwa kumwabudu yeye.
Hilo lakubaliwa, lakini ule 'Umoja katika utatu' utatoweka.
Hamna njia yoyote ya kuwa na 'Tatu katika Moja' na 'Moja katika Tatu', zote mbili hizo, wakati huohuo mmoja.