The Qur’an Affirms the Following Biblical Doctrines Concerning Christ
Jesus Christ is the Son of Mary – Bakara 2:87
Jesus Christ is the Messiah – Ali-İmran 3:45
Jesus Christ is the Servant of Allah – Nisâ 4:172
Jesus Christ is a prophet – Meryem 19:30
Jesus Christ is an apostle of Allah – Mâ’ide 5:75
Jesus Christ is the Word of Allah – Al-i-İmran 3:3
Jesus Christ is the Word of Truth – Meryem 19:34
Jesus Christ is the Spirit of Allah – Tahrîm 66:12
Jesus Christ is a sign for mankind – Meryem 19:21
Jesus Christ is a witness – Nisâ 4:159
Jesus Christ is a mercy from Allah – Meryem 19:21
Jesus Christ is great (eminent) – Al-i-İmran 3:45
Jesus Christ is righteous – Al-i-İmran 3:46
Jesus Christ is blessed – Meryem 19:31
Jesus Christ did miracles – Bakara 2:87
Jesus Christ was led by the Holy Spirit – Bakara 2:253
Jesus Christ was born of a virgin – Al-i-İmran 3:47
Jesus Christ guides to the truth – Al-i-İmran 3:49
Jesus Christ healed people – Al-i-İmran 3:49
Jesus Christ raised the dead – Al-i-İmran 3:49
Jesus Christ would die for unbelievers – Al-i-İmran 3:55
Jesus Christ was resurrected from the dead – Al-i-İmran 3:55
Jesus Christ ascended to heaven – Al-i-İmran 3:55
Jesus Christ is a life giver – Mâ’ide 5:110
Jesus Christ is holy – Meryem 19:19
Jesus Christ is coming again – Zuhruf 43:61
Jesus Christ knows the future – Zuhruf 43:61, 63
Jesus Christ is to be obeyed and followed – Zuhruf 43:63
UHAKIKA WA YESU
Naam, kila mmoja anayo haki ya kujichagulia Ukristo mmojawapo miongoni mwa Ukristo wa Kipaulo na Ukristo wa Yakobo Mwema na viongozi wengine wa kale wa Kikristo waliokuwa wanafunzi wa Yesu Kristo mwenyewe.
Lakini napenda kuhakikisha hapa habari hii ya kwamba Ukristo halisi uliendelea kusonga mbele kushikamana na imani katika Umoja wa Mungu na ukajiweka kando kabisa na bidaa zilizozuka baadaye zilizozalisha upayukaji na matatizo ya itikadi ya Kikristo kama vile Yesu kuwa Mwana wa Mungu, Utatu, Dhambi ya Asili, Wokovu, kuhuika Yesu kimwili baada ya kufa na kadhalika.
Fikara za viongozi wa zamani wa Kanisa, Yakobo Mwema akijulikana zaidi kati yao, zilikuwa nyofu na halisi zisizokuwa na upingamizi wa ndani wala hitilafu zilizofichikana nyuma ya wingu la moshi la siri.
Mtaala wa historia ya Imani ya Umoja wa Mungu katika Ukristo unahakikisha pasipo shaka ya kwamba Umoja wa Mungu usiofanywa kuwa mgumu kueleweka na kelele za utatu, uliendelea kuwa imani safi na rasmi ya Kanisa halisi la Kristo.
Tafadhali kumbukeni ya kwamba sina lengo la kuwaingiza Wakristo katika imani yoyote nyingine isipokuwa tu kuwaongoza kwenye imani halisi ya Kristo mwenyewe.
Hili ni jaribio halisi la kuwakaribisha Wakristo warudi nyuma na kuiamini imani na amali safi ya Yesu isiyochanganyikana na
mambo mengine yasiyotakikana.
Hili ni jaribio aminifu kwa kuondoa yaliyobuniwa na kuleta mahali pake mambo ya kweli ya Ukristo - mambo ya kweli ambayo kwa hakika ndiyo mazuri kama yalivyo ya hakika na yanatuliza akili na moyo.
Siyo hekaya za kubuniwa kumhusu Yesu Kristo zilizoubakiza Ukristo tangu miaka karibuni elfu mbili na kuusaidia kupona miito ya akili na busara inayodumu ya kuzidi kwa sababu ya maendeleo ya sayansi, wala haukubaki kwa sababu ya itikadi ya kubuniwa
ya Utatu.
Kilichobakiza ukweli na kiini cha Ukristo ndiyo dhati na mafunzo ya Yesu Kristo. Sio uungu wa Yesu bali ni matendo yake bora matakatifu yanayovutia ili mtu afungamane nao.
Uti wa mgongo wa Ukristo hasa ulikuwa ni yale masumbufu na subira na uvumilivu kwa ajili ya shabaha njema na kukataa kwa uaminifu majaribio yote ya kikatili ya kumlazimisha yeye kugeuza kanuni zake. Bado ni mzuri na wakupendwa hata leo jinsi ulivyokuwa hapo kabla.
Huo umeziathiri kwa nguvu sana fikira na nyoyo za Wakristo hata kwamba wamebakia kufungamana na Yesu na wanaonelea kufumba macho yao wasiangalie hitilafu za kiakili katika Utatu na kadhalika ni afadhali kuliko kutengana na Yesu.
Utukufu wake hasa umo katika hakika hii ya kwamba yeye akazishinda nguvu za giza zilizokula njama kumtiisha ijapokuwa
yeye alikuwa mnyonge sana wala si zaidi ya kuwa binadamu.
Ushindi wa Yesu ni kitu wanachopaswa watoto wa Adamu kushirikiana katika hicho kwa fahari. Sawa na nadharia ya Waislamu, yeye alikuwa miongoni mwa kizazi bora sana cha Adamu.
Yeye aliwafunza wanadamu kwa mfano wake wa kuvumilia alipokabiliwa na usumbufu mkali na uchungu mwingi sana.
Ushindi mkuu wa Yesu ulikuwa kutokujisalimisha na kukaa imara katika hali ngumu sana ya majaribio makali. Ni maisha yake ya uchungu na usumbufu yaliyookoa wanadamu na yalimfanya ayashinde mauti. Kama yeye angelichagua kufa kwa hiari, kitendo chake hicho kingelikuwa sawa na kujaribu kuyakimbia hayo mateso.
Mtu anawezaje kulihesabu tendo hilo kuwa ushujaa? Hata wale wanaojiua kwa kulazimika, kitendo chao pia kinahesabika kuwa cha woga tu.
Kushirikiana katika shida maishani ni afadhali kuliko kuzikimbia kwa njia ya kujiua.
Hivyo wazo la dhabihu kuu ya Yesu kwa kukubali mauti kwa ajili ya binadamu ndiyo maono matupu yasiyo na kiini mle ndani.
Ubora wa Yesu, twasisitiza tena, ulikuwamo katika kujitolea kwake sana katika maisha mazima. Katika maisha yake yote yeye
alishindana na vishawishi bila kulegea na kuyabadilisha maisha ya uchungu kwa maisha ya raha. Alisema aliyoamrishwa kusema, si zaidi wala si kidogo kuliko aliyoambiwa na Mungu kusema.
Yeye alimwabudu Mungu maisha yake mazima, naam, alimwabudu Yeye peke yake, na hakumtaka yeyote mwenye kufa kuinama mbele yake wala mbele ya mamake au mbele ya Roho Mtakatifu.
Hiyo ndiyo hakika ya Yesu ambayo tunawakaribisha Wakristo wa madhehebu yote na imani zote kuirejea.